Waberoya,
Hao mabepari wenyewe wamekwama. USA walipewa uhuru wa watu/mashirika binafsi kujifanyia kila kitu wanavyotaka wenyewe. Nini kimetokea?
Msiandike kwa kutumia mfano mmoja. Angalieni mbele na nyuma na ndipo mje na hizo zenu za kutetea kufa kwa Azimio la Arusha. Mwinyi na Mkapa walitakiwa kurekebisha yale tu ambayo kwao wanaona yanafanya uchimi ukwame. Pia unaporekebisha si kuwa ubadili kila kitu. Unafanya kwanza majaribio na kidogokidogo unaangalia umetoka wapi na umefikia wapi. Wachina wanafanya hivyo hadi leo kwa mafanikio makubwa. Wangelitangaza kuwa wako HURU kama sisi tulivyofanya, nafikiri leo wangelikuwa na vita na machafuko ya kila aina.
USA kimegoma na mwisho serikali imerudi na kusema itakuwa inaweka mkono wake kila sehemu ili walau wafahamu nini kinaendelea kwenye mashirika. Ilishindikana nini kuwapa Watanzania hata kama kwa Mkopo mashirika yote na serikali ibaki kuwa mwangalizi tu na kuchukua kodi. Leo hii haya mashirika yangelikuwa yanaongozwa/kumilikiwa na wazawa na sidhani kama yangelikuwa yamekufa.
Siyo siri kuwa wapinzani wa NYERERE walifanya makusudi kuyauwa mashirika ili tu kuonyesha Azimio la Arusha ni la ovyo. Walipokipata wanachokitaka, wakaliingilia Azimio la Arusha na kuliuwa kwa ndani na kuacha mwili wake nje (jina) ili mtu akisema, wawe wadai kuwa ahhh, AD bado ipo hai kabisa na inaendelea vizuri sana. Too sad.
Ndiyo maana Nyerere anasema "wenye akili tukajua AD imekufa". Yaani hata Miiko ya viongozi? Nakubaliana na member mmoja hapo juu kuwa AD iingizwe kwenye Katiba ya nchi hasa kile kipengele cha Miiko ya viongozi. Haya ya juzi kumsikiliza Mkono na Genge lake wakitetea kuwa CCM inatakiwa iwe na mafiga matatu yaani Wakulima, wafanyakazi na Wafanya biashara, kwa kweli ni kichekesho. Wafanyabiashara wenyewe ni CCM ambao hata unashindwa lini wameanza kuwa wafanyabishara zaidi ya kuwa na pesa za ufisadi.
UJAMAA na Kujitegemea: Wayahudi waliweza sana kuanza na hii system. Imewasaidia sana sana. Sisi tumekwama sijui ni Miafrika ndivyo tulivyo au viongozi wetu?
Huwezi ukafananisha ujamaa wa Nyerere na hao wachina, warussia n.k ,. Ujamaa wa Nyerere ulikuwa ni hybrid ya hizo siasa na influence ya watu wengi
Hakuna sehemu pia ninayosuggest kuwa Ubepari ni bora, mind yangu haijawekwa kwenye kapu kuwa kama si ujamaa basi ni ubepari!
Nyerere na waasisi wengine wa siasa ya ujamaa ya Tanzania, still they have credit to gain, wanastahili sifa na heshima zao na hasa kuwa na siasa ya ujamaa na kujitegemea ya kwetu sisi! Nyerere angeiga wachina angekuwa dictator!
My argument katika dunia ya leo, na kizazi cha leo, cha watu millioni 45 we have to sit down na kuona AD ilikuwa na uzuri upi, na kasoro ipi! lazima tujue pia nature na tabia zetu watanzania wa leo, lazima tuangalie influence ya globalisation, climate change, terrorist, ambayo hatuwezi kujitoa kwayo, lazima tuangalie je Kujitegemea kunakosemwa kulikuwa na vision ipi, malengo yapi?
Hakuna siasa 100% perfect kama JKN aliweza kutoka na siasa yake, we dont have people ambao wakasimama na kusema lets take Nyerere's idea na kujumlisha na idea zingine na tufuate hivi kwa leo hii.JKN idea will never be our compass.
Kurudi nyuma na kulilia AD ni sawa na kurudi tulipofeli, AD is katiba? ni biblia au Quran? watu leo hii wameiba hawapelekwi jela wala kurudisha mali zetu ni kwa sababu ya AD haipo?? i dont get it!
Hata leo hii JKN angekuwa hai , na tukampa nchi tena, his mind today lazima ni tofauti na nyakati hizo. We need to start now and make our future! siamini kabisa kuwa system za dunia hii ni ubepari na ujamaa tu. Tumefikia hapo, tumekwama hapo na kuamini ubepari mzuri kwa sababu hatujafanya assignment zetu vizuri.
Kulilia AD ni kupoteza muda, kama hakuna anayeweza kupima mafanikio ya siasa hii na imebaki fiction, then ndiyo kufeli kwenyewe huko, hatuihitaji story nyingi wala sababu, ambazo tunazo kila siku na hazikosekani!
Kama leo hii mtu bado anaona pamoja na hii kitu kufail still anaona ni bora zaidi, basi tuna matatizo mengi na makubwa ambayo lazima tuyatatue hayo ili kufikia ujamaa na kujitegema, kwa namna nyingine JKN alitoa idea ambayo pengine it will work next century! we have big big problems na matabia yetu haya ili kuishi kwenye hilo azimio!
However, I am still thinking whether kama matatizo ya leo ni kutokana na sera ya ujamaa!
If this is our mind, lets Kikwete and his partner plunder our wealthy because AD IS DEAD na yeye siye aliyeliua!
I believe in Law, order and JUSTICE.
I believe every human shall work and improve our society and the universe siyo kwa sababu mtu fulani kasema ni kwa sababu tumezaliwa tukijua hilo!
Ninachokataa ni kuwa kuna watu hawataki kungalia failure ya hizi siasa, hatutaki kukaa chini na kusema JKN and so and so walikosea hapa na walipatia hapa., na sisi leo tuchuke idea znuri za JKN na kuacha makapi na kuungansiha na hali yetu ya sasa na kusonga mbele!