Mjadala ni mzuri
Hata hivyo nina maswali kadhaa kama ilivyo ada yetu hapa JF kwenye mijadala mototo....However,i don't know about many of us,mimi huwa nina tabia ya kuupitia mjadala wote kabla sijaposti ama kutoa maoni/mchango wangu kwenye mada husika....Na kila nilipokuwa nikipitia page after page,maswali ambayo ambayo yalikuwa yakiibuka kichwani mwangu na ambayo nilitaka kuwauliza baadhi ya members yamekuwa yakijibiwa,ila kuna ambayo bado...
Ndugu Waberoya;
Umetoa msisitizo kuwa AD liingizwe kwenye sheria na wengi wanaonekana kukubaliana na wewe.Hata hivyo naomba kusahihishwa,"AD haikuwa mojawapo ya sources za sheria za nchi?" Nasema hivyo kwasababu najiuliza kama kweli AD lilikuwa haliwabani viongozi mafisadi then AZ lilikuwa la nini? Je AZ halikuwa foundation ya kubadili baadhi ya sheria zilizowabana viongozi kujilimbikizai mali?ie sheria ya maadili ya uongozi? Ninashangazwa sana pale unaposema kuwa warithi wa mwalimu ie Mwinyi na genge lake hawakuwa wasanii,either walifanya kwa makusudi ama bahati mbaya,wao tofauti na mwalimu ni usanii,na utapeli dhidi ya wananchi period!
Ukisoma kwa makini hotuba ya Rais mstaafu Mh Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwa wazee wa Dar na Taifa kwa ujumla(wazee wa ccm) ilikuwa ni hotuba ya kisanii na ya kinafiki! Ya madai kwamba ili twende na wakati basi viongozi ni Rhuksa kujilimbikia mali,huku akitumia mabadiliko ya vitu kama kima cha chini cha mishahara,ambapo kulikuwa na takwimu zilizowekwa kuhusiana na kujilimbikizia mali kinyume na kazi unayofanya,wao walichofanya ni kuiondoa hiyo cap moja kwa moja na wala si kui analyze na kuona kama ni shifting ifike wapi,yani ni kiasi gani kina constitute kujilimbikizia mali,hakuna mipaka ya tafsiri ya "Kujilimbikizia mali" na pia hakuna tofauti kati ya mali anayoipata kiongozi na mali anayoipata mwananchi wa kawaida,binafsi naamini kama unataka mali basi usijishughulishe na uongozi wakati wa kutafuta mali hiyo kwasababu ni lazima utumie ofisi ya umma kufanya hivyo na migongano ya kimaslahi inakuwepo!Hata hivyo ukitaka kujua ni usanii,kwenye hotuba yake hiyo alisema ni situation mbili tu zitakazowaruhusu viongozi wawe na nyumba za kupangishia;moja ni kama wamehamishwa kikazi kwenda mkoa mwingine ama kama kuna ulazima wa kupangisha baadhi ya vyumba ili kuwafanikisha kwenye ulipaji wa deni kama ulichukua mkopo,lakini kiukweli si ni mtoto wake amerithi nyumba za kupanga?mtoto wake naye si kiongozi?na kama Jasusi anavyosema kuwa alirithi kutoka kwa baba yake?je yeye mwenyewe kama si unafiki mbona alifanya tofauti na mwalimu?Ukipata mali ukiwa kiongozi ni lazima usema umepata vipi!
Je mwalimu alishindwa kuwa na apartments za kupangishia watu na mali lukuki?Kiukweli viongozi hawana haja ya kujilimbikiza mali kutokana na nature ya kazi zao,na kama wakifanya hivyo na tiafa likapata maendeleo,bado wataenziwa na hawatakuwa na shida,shida inaletwa na ubinfasi na kutokujali kwa viongozi mafisadi kwasababu system nzima ikiwa corrupt basi hakuna heshima kwenye uongozi kama usipojilimbikizia mali.
Kwa kifupi naamini AD lilikuwa kikwazo kwa mafisadi na ndio maana wakalikalia kikao huko Zanzibar....Hivyo Myinyi anapoibuka sasa na kusema kuwa hakuliuwa AD,nina amini kuwa anazeeka vibaya,kwasababu nashangazwa kwanini unafiki wake haumuumbui!Kama amesahau kwasababu ya uzee,then na wasaidizi wake nao wanamsaidia kusahau,huku na wao wakisahau kuwa Tanzania ya sasa ni ya tofauti kwa kiasi kikubwa.
Tulipokwama:
Tulipokwama sisi ni kutolenga kwenye solution...Na hivyo labda swali langu la pili linalokwenda kwa Mag3 litakuwa mojawapo ya changamoto ya ku analyse wapi na kwanini tumekwama....
Ndugu Mag3; Kama ilivyo kwa Ndg Jasusi,ulikuwepo Mnazi Mmoja mnamo mwaka 1967,kwanza awali ya yote "shikamoo Mzee" Lol! Ukweli heshma ya JF iko juu! Na mara nyingi nimekuwa nikiona JF kama licha ya ukweli kwamba ni kioo cha jamii yetu,pia ni kisima cha hazina ya fikra za kimapinduzi,pengine hata hadhi ya kama Nationa Archives....Mkuu pamoja na wengineo kama Rev Kishoka,MKJJ,Abdulhalim,Sikonge,Jasusi nk,maoni yako ni mazito,specifically kwenu waumini wa AD kama nilivyo mimi.....Tofauti yetu however ni kwamba wakati AD likitolewa mwaka 1967, kulikuwa na mwamko wa kisiasa kwa vijana wakati huo,hata hivyo kama sijakosea pia umeimply kuwa you was some sort of a rebel coz hukutaka kushiriki,i believe you had a cause....Ulichofanya kwa wakati huo,yani kwenda nje ya nchi na kutafuta maisha ndicho wanachofanya vijana wengi hata sasa,yani kuanzia huo mwaka 1967 hadi sasa,vijana wengi wanafanya yale yale,kukimbia nchi kusaka life,je ni zipi hasa sababu zilizokufanya ukazira?
Tunajuwa kuwa AD lilianzishwa mara baada ya viongozi kuanza kujilimbikizia mali na wananchi kuanza kugawanyika kimatabaka nk,na Mag3 inavyyonekana ulifurahishwa na idea nzima ya AD,je ni kwanini hukutaka kushiriki?Ni kipi kilikukatisha tamaa?Certainly wananchi wa sasa ama kizazi chetu,binafsi bado nawalaumu viongozi wetu kwasababu wanachofanya ni kinyume cha mapenzi ya wananchi...Tofauti na wakati wenu ambapo inaonekana wananchi walikubaliana na AD moja kwa moja,ila still kuna vijana kama nyie mliokuwa rebels licha ya kuona kuwa idea inafaa,Je ni kwasababu umuhimu wa AD haukuonekana kwa wakati ule kama ilivyo sasa?
Nilikuwa bwana mdogo kipindi cha mwinyi especially miaka ya tisini baada ya AZ na kwa ukweli licha uelewa wangu ndogo bado niliona usanii wa wazi wa viongozi wetu,na nilikuwa nikishangazwa licha ya kuwa bwana mdogo kuwa ni kwanini viongozi hao bado wanachaguliwa,kipindi hicho pia mwamko ulikuwepo na Mrema ndipo alipokuja....Ni ukweli hata mwalimu mwenyewe aliuona usanii na ikampelekea kuandika kitabu hususan Uongozi wetu na hatma ya Tanzania.
Hivyo wazee wetu Jasusi na Mag3 ambao mlikuwepo mwaka 1967,na mnaonekana kukubaliana na AD,lakini pia mkionekana kuwa mlikatishhwa tamaa na mambo flani flani na pengine kuwa sababu ya kutokushiriki moja kwa moja kwenye utekelezaji wa azimio ambalo lilionekana kama mkombozi wa watanzania dhidi ya unyonyaji na ufisadi...Nina amini pia sababu zenu zinaweza kuwa tofauti na zetu sisi vijana wa kizazi hiki kwasabau AD lilianzishwa mara baada ya viongozi kuanza kujilimbikia mali na hivyo matabaka kuanza na chuki miongoni mwa wananchi,ni wazi basi AD lilikuwa kipenzi cha wananchi na hatua ya kutia moyo na hivyo mapenzi dhidi ya viongozi wetu yakazidi na mwamko wa kisiasa ukawepo,tofauti na sasa ambapo hata viongozi hawajali kabisa,na ambapo ni wazi kuwa vita ni kati ya maslahi ya watawala dhidi ya maslahi ya wananchi ambayo ana constitute maslahi ya Taifa.
Wazee wetu; Pia kama mnayozumgumza yanatoka moyoni,basi sifa moja kubwa mliyonayo ni kutokuwa wanafiki,kwasababu licha ya wengi kutoshiriki kwenye utekelezaji wa AD,bado walioshiriki ndio waloliuwa,hence unafiki kwasababu bado wanadhani sisi "Hamnazo' Nitakalomlaumu mwalimu ni kama kweli hakutaka ushauri,lakini kama wanayoyafanya viongozi hawa na wengineo waliokuwa washauri na wanafunzi ndiyo haya,bado najiuliza ni ushauri gani huo walimpa mwalimu,na certainly kama haya wanayoyafanya ndiyo walimshauri mwalimu,then hata kama ingekuwa mimi ningeitwa "haambiliki!" Honestly,kwa mtaji huu utasikiliza ushauri huu si ufisadi?ninaamini kabisa tabaka la viongozi waliomrithi mwalimu ndilo lilitulet down watanzania...Na hapo ndipo nakuja kwenye pointi ya tatu....
Reverand Kishoka:
Hapo ndipo pointi bado inaendelea kuhusiana na wapi tumekwama,tumekuwa tukitofautiana wengi wetu humu ndani,wengine wakisema kwa sababu miafrika ndivyo ilivyo basi vongozi hawana haja ya kulaumiwa,mkuu Rev. Mimi msimamo wangu bado uko pale pale,na ninaona kuwa tunakubaliana kwa kiasi kikubwa kwasababu wengi wetu sasa wana conclude kuwa tatizo ni uongozi,licha ya kwamba bado kuna wanaosema na wananchi pia.
Tukiangalia kwa makini,mafanikio ya AD ndio exactly what its letting the declaration itself down,yani umoja na udugu uliojikita kwenye misigi ya "Amani" matunda hayo ni ya AD,na matunda hayo ndiyo yametunyima uthubutu wa kujaribu mabadilko kwa hofu ya kukosekana kwa amani inayoletwa na umoja na udugu huo....Ukiangalia kiundani,mafanikio ndio weaknesses,viongozi wanajuwa kuwa mafaniio hayo ndiyo weakness na wakati sisi tunajuwa ndio mafanikio period,kwa hivyo kama mwenye kuona mafanikio hayo ndio weakness na akaamuma kutumia weaknesses hizo ambazo machoni mwa wananchi zinaonekana kama mafanikio,ndio hapo mkorogo wa kisanii unapoanza.
Ni lazima tukae chini tutafakari kweli tuona ni wapi tumekwama,na tukiangalia kwa makini tutaona ni kwenye uongozi,tutizame nini haswa maana ya umoja na udugu kwenye maslahi ya Taifa,wananchi tuliassume kuwa usawa uko hata kwenye nia,yani wote tuna nia sawa,na bado tunaamini kuwa nia yetu ni sawa na nia za viongozi,hilo ukweli ni kwamba lilifutwa na azimio la Zanzibar,sasa hivi wananchi na hadi waelewe kuwa ni maslahi yao vs ya viongozi.
Mzee Mwinyi alisema kuwa ni muhimu kwenda na wakati,kwamba tusije tuka "pelea" mara baada ya "kupwa kwa bahari" Hata hivyo ukweli ni kwamba wananchi ndio samaki walioachwa wakapelea maana azimio la Zanzibar linahusu maslahi ya viongozi,na hivyo hapo vita ndipo ilianza rasmi,ila wananchi kwa kutapeliwa hawakujua kuwa huo ndio mwanzo wa ule umoja unaoletwa na haki na usawa kupotea,kifikra wananchi bado wako huko,vitendo tofauti vinaanza kuwaonyesha mambo ya tofauti,hakuna tena cha Taifa,ni "mimi mimi mimi!" "Me myself and i" hakuna aliyeko kwenye ofisi ya umma kwa maslahi ya umma,sasa ukitizama kwa undani solution pekee inaweza kuwa mapinduzi,kama inavyoonekana pia kuwa baadhi yetu tunaanza kukubaliana na hilo,hivyo binafsi siwalaumu wananchi kwa kiasi kikubwa na pia siamini kuwa miafrika ndivyo ilivyo!Naamini kuwa viongozi wetu wanautumia udhaifu wa kisiasa,kiuchumi na hata kijamii,dhaifu ambazo causations zake zinaenda all the way back to maybe slavery....
Hitimisho langu kwasasa;
Wakati nikisubiri majibu kutoka kwa members niliowauliza maswali,bado siamini kama wanavyosema members wengine sijui mazuri ya mwinyi whatsoever....Najiuliza ni yapi hayo?maana once youre wrong from the beggining with the basics,basi always you're all the way wrong.
Mara zote usanii na utapeli huwa na dalili za mazuri,unaweza kudhani ama kuona kuwa everthing is right na still ukawa absolutely wrong!Kuchukua a wrong way haina maana hakuna dalili kwamba uko right,ama kwamba hautafika karibu na destination,tatizo utakalogundua however,ni kuona wazi kuwa uko in a wrong destination,yanayoonekana kwamba ni mazuri yataonekana njiani,lakini mkishafikaka ndio mtajuwa kuwa mazuri hayo yaliwalenga wale waliokuwa wakitaka kwa makusudi tufike kwene wrong destionation,huku wakitudanganya kuwa we're still in a right way,na tukiangalia around tunaona kama vile tuko in a right way ama kwamba mwenye kutu mislead alikuwa na nia nzuri,(ie Mwinyi)hata hivyo nia nzuri kwa wananchi haiwezi kuwa na matokeo tofauti na maslahi ya wananchi wenyewe na bado ikawa nia nzuri kwa wananchi,na kwahiyo udugu,amani na umoja vinatulazimisha tuamini kuwa nia ya viongozi hao ni nzuri na wenye kusema tofauti hawataki umoja wetu,ni lazima tujiulize huo umoja tunaouzungumzia ni wa aina gani?
Mbona wamarekani wana umoja lakini hawana huo udugu lakini bado wana maendeleo?Tukishaondoa ule udugu wa kuoneana haya mbele za sheria za nchi,hatutafika,umoja wetu ni lazima ujikite zaidi kwenye malengo ya kitaifa na si individual basis,ni heri nijenge mazingira bora ya kizazi kijacho kuliko kuwa na umoja na fisadi!
Tabaka tulilokuwa tukilipiga vita kabla hata ya uhuru ndilo tabaka ambalo ndugu zetu kabisa wameamua kulichukua against us,hili linapelekea vita sasa kuwa ya tofauti,ni kama vita ya terrorisma,ambapo wamo miongoni mwetu,tofauti iliyoko sasa ni kwamba wanajilinda kwa kutumia system na dola the same way tabaka la kikoloni lilivyofanya.
Tujiulize mwaswali ya msingi as this mjadala goes on......What is it gonna take kumwondoa mkoloni mweusi?How do we fight this war?Je kwanini wale wanaoonekana kuwa ndiyo walikuwa na nia nzuri na taifa kama kina Mag3 na Jasusi hawakupata nafasi ya kushiriki kwenye ujenzi wa taifa,je nini haswa kiliwakwamisha...?
Wote tunakubali pia kuwa miiko ya viongozi ni muhimu iwepo,tatizo ambalondilo lililopelekea yaliyotokea mwaka 1967,swali ni kwamba sasa ni kipi tutakachofanya cha tofauti kama tukiirudisha miiko hiyo?
Binafsi i believe tunahitaji uongozi mpya kabisa ili kuweza just kuanza kufikiri wapi pa kuanzia....Waberoya yeye anasema kuwa AD liingizwe kwenye sheria za nchi,jambo ambalo nimejaribu kulitolea ufafanuzi based on ma knowledge on it,naweza kuwa wrong na hivyo ninasubiri maoni ya members wengine,hata hivyo kama sikosei kuna pahala Sikonge alisema kuwa sheria ya kunyonga haizuui watu kuuwa!
Hilo halina maana kuwa tusiweke sheria kali dihidi ya mafisadi,ila ni kwamba hata sheria zilizopo zinatafutiwa namna ya kubadilishwa,kusema tusiwalaumu viongozi ni unafiki uliopindukia!
Kupunguza mazingira yanayochangia mauwaji ni bora kama vile sheria hizo dhdi ya wauwaji,kama alivyosema mzee Mkandara,kwamba badala ya kujenga mazingira ya kumaliza uzalianaji wa mbu,sisi tunajikita kwenye uzalishaji wa neti, biashara zaidi ya utu?hayo ndiyo manufaa ya kujikita kwenye ubepari bila tafiti kwasababu viongozi wetu wako hapo kwa maslahi binafsi,sasa hao wenye kutengeneza pesa kutokana na biashara ya uzalishaji neti watataka mbu ziishe kweli?Kama ni kiongozi mwenye kiwanda hicho atataka mazingira yasafishwe na kuboreshwa kwa manufaa ya nani?ubepari si ndio huo wa kutengeneza magonjwa ili mtengeneza na dawa za kuutibu simply kwasababu ya "Uzalishaji"?
Rather "utekelezaji" wa sheria ndio muhimu,kama viongozi wako busy kutengeneza sheria zinazohalalisha ufisadi,then hatutaona mabadiliko,unless tuwapate viongozi wapya wenye nia ya kweli na utawala wa kisheria unaozingatia miiko ya uongozi,na kuwa na sheria ambazo ziko juu na si wengine kuwa juu ya sheria hizo,haijalishi sheria zinasema nini kama viongozi ama watu flani flani wako juu ya sheria hizo!
Kwa kumalizia ndugu waberoya,kama nilivyosema hapo nyuma,sheria zina sources zake,nikupe mfano wa Taifa la marekani ambazo primary sources zake ni katiba yenyewe ya marekani,federal satatutes and treaties,federal administrative law,federal case law,state constitution,state statutes,local ordinances,state case law nk.
Kimsingi sheria za maadili ya viongozi ndizo haswa zilitokea kwenye miiko ya uongozi,kimsingi sheria hizo za kupingana na maadili ya uongozi,ziliingizwa na mafuriko ya utandawazi kwa kupitia usanii wa azimio la Zanzibar.
Kama viongozi wetu walifanya usanii huu kwa makudi basi Mungu lazima atawapatiliza.Time will tell!Kama wasipojirudi na kushirikiana na wazalendo wa kweli mwisho wao unaweza usiwe mzuri maana theres no way forwrd before fixing di shyt first and foremost,we're stuck,ni heri kama tungekuwa tuko in a right direction,basi tungeweza kuignore and deal with it in a different situation,tatizo we're stuck kwasababu we're absolutely in a wrong way...Usanii certainly una kikomo na wakati ndo huu.....Theres no way forward without a change of direction.,or atleast go back to basics and build upon it!AD lirudi lfanyiwe marekebisho and "F" AZ !