Sikulaumu wewe, bali namwombea apumzike salama

Sikulaumu wewe, bali namwombea apumzike salama

Dah pole sana mpendwa wangu.Kwa NEEMA na REHEMA tu utafanikiwa kupata hitaji lako.
 
Precious precious Kibaha,long time. Nilipita hapo 1999-2002 then 2002 -2005,napata picha maisha ya likizo yalivyokuwa. Kachingwe Kaselenge na Kayenga,good memories.

Nilisoma na watu wenye majanga km yako ndugu,suala ni kutokata tamaa tu. Misaada itakuja na itaisha,shule utasoma na itaisha lakini maisha bado yapo mbeleni. Usikate tamaa daima. Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako daima kwa maombi. Yeye ndie atakayefanya njia yako,naamin umesikika na kusomeka vyema kwa members.

Nakuombea usiku huu wa leo maana nami niko njia panda kwa namna yangu.

daaaah!!!! mkuu si ndo tupo hapa ila ayo majina yameishia 2012
 
mkuu kila nikicheki nahisi huna uwezo wa kuja kibaha so nahis wazo langu la mwanzo ni gumu anyway ngoja tutumie namba yako.....!!!!
 
Hii thread imenitouch sna ,nikiwa kama kijana mwenye kujua matatizo ya watu na kufeel pain the same way as he's nimeumia sna. Napenda sna kumsaidia huyu Raelish. Kama kuna njia ya jins ya kumsaidia naombeni kufaham plz. Mimi nipo tayari kumchangia kiasi kidogo cha pesa. Find me out on (luogaJr@gmail.com)
 
MKUU pole sana ila mfadhili wako hajafa ndugu yangu ni anarudi kwao mpe ukweli kuhusu maisha yako naamini atakuelewa maana wenzetu wanaoenda sana kutimiza ndoto zao ikiwa alikuwa na ndoto ya kukusaudia mpaka mwisho atafanya hivyo maana saivi dunia ni kama kitongoji mungu atakusaidia usijali kulia sana sio dawa MKUU komaa we ni mwanaume lazima upambane
 
Napata faraja kubwa kutoka kwenu, nitatuma vielelezo vyangu ili mnisaidie ndugu zangu. Maisha ya dunia hii Yana changamoto mpaka muda mwingne unashndwa kujua ni kwann
 
Nmetuma vielelezo tayari. Nasubiri kinachofuata.
 
mkuu raelish,

pole sana na matatizo, mwenyezi mungu akuwekee wepesi na upate nafuu haraka na kwa amani.

Naomba nichukue nafasi hii kwa kuomba radhi kwa kuchelewa kujibu, hasa kwa wale ambao walikuwa wamenishtua nihusike kwa namna moja ama nyingine. Nimeshawasiliana na raelish kwa kutuma pm, ili atimize baadhi ya vielelezo ili iwe rahisi kujua ni msaada aina gani anahitaji na wa kiasi gani itusaidie sisi kama wanajamvi kukusanya kwa nguvu hiyo.

Nawashukuru na wale wote walio onyesha nia ya kutaka sana kusaidia. Mara baada ya kumaliza mawasiliano na raelish nitatoa mrejesho mara moja ili tuendelee na nia ya kuwa msaada kwa kiasi fulani katika maisha yake. Maelezo zaidi yatakuja baada ya kujibiwa na raelish. Asanteni.

Pamoja sana!


=======

uongozi wa jamiiforums umejiridhisha na kuafiki kwamba matatizo ya raelish ni genuine. Hivyo basi, utaratibu wa kuchangia utafanyika kama ifuatavyo;

kwa wale walioahidi msaada wa kifedha, na hata wasioahidi ila wameguswa na wangependa kushiriki kwenye hili, wanaweza kufanya hivyo kwa kutuma kiasi cha pesa kupitia m-pesa, namba ya simu: 0757 525 366 (jina litakalotokea ni obedi mnzava).

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa nyote mlioshiriki na mnaoendelea kushiriki katika zoezi hili.

- majina ya walioahidi kuchangia mpaka sasa ni;
julius malema jr nyalotsi mokoyo miss chagga idimulwa alinda kipilipili billie clemency kitulo rugaijamu dagii mtusiasa rosebud freeland deogratius n niester


wengine pia mnakaribishwa.

uongozi wa jf unalisimamia jambo hili kwa karibu na kwa umakini sana mpaka mwisho wake. Na litakapofikia, basi mrejesho utaletwa hapa.

asante.
asante kwa taarifa...
 
Nitachangia fedha tarehe 29 June., kijana usome kwa bidii na utakapokuwa mtaalamu wa hiyo fani uhudumie watu kwa unyenyekevu, bidii, bila kutanguliza rushwa.
Kila la heri, nafikiri michango itatimia na Ada utapata.
 
Nitachangia fedha tarehe 29 June., kijana usome kwa bidii na utakapokuwa mtaalamu wa hiyo fani uhudumie watu kwa unyenyekevu, bidii, bila kutanguliza rushwa.
Kila la heri, nafikiri michango itatimia na Ada utapata.

Ahsante, nitazingatia
 
Mungu azidi kuwabariki ndugu zangu wote wanaohusika kwa namna moja au nyngne kunisaidia, Mungu awakumbuke
 
duuh! moyo wng umeumia san kwan ni ujumbe mzito san machozi yamenitoka kwan nataman nikuchangie lakin sina chochte nimeumia san
 
Mungu akupe nguvu kaka, haya yana mwisho, mtegemee Mungu muda wote, hautajutia kupitia haya unayopitia.
Hapo mbeleni utaweza kuangalia alipokutoa na kumsifu yeye kwa pale atapokufikisha ila tu usiache kumwamini na kumtegemea
 
Ahadi ni deni, kama nilivyosema huku nyuma kuwa mpk J5 nitakuwa nimetuma..Nina furaha kukujulisha kwa nimetuma.. Kwa pamoja tutashinda. AshaDii , Raelish
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom