Kijana Raelish
Pole sana na mikasa uliyokumbana nayo na unayoendelea kukutana nayo. Elimu yako ikusaidie zaidi kutokea hapo. Sisi wengine, tunaamini mwenye elimu huweza kukabiliana na changamoto, hivyo huzifurahia zaidi kwa kuwa inampima kiwango chake cha kuweza kutatua matatizo yanapotokea.
Kwa sasa, hitaji la ada ni kubwa zaidi kwa kuwa muda unakwenda na huwezi kufanya chochote coz hukujiandaa vema..
Mimi nimeshatuma nilichojaaliwa, na nakuombea ufikie lengo mapema. Ni Imani yangu kuwa walioguswa ni wengi na watakaojitokeza kukuchangia ni wengi pia wakiwemo wakuu Julius Malema Jr Nyalotsi Mokoyo miss chagga Idimulwa Alinda Kipilipili Billie CLEMENCY Kitulo Rugaijamu dagii MTUSIASA rosebud Freeland Deogratius n niester.
Shime ndugu zangu mliosalia, Tujivunie kumsapoti kijana wetu kwa hali aliyonayo.
Kwa Mungu tutazikuta zikiwa ni amali!
Nasubiri sana uwasiliane namim, maana nina hamu ya kujua kinachoendelea ili nijiridhishe kama shule ipo au ndo basi niingie mtaan tu nikaungane na walimwengu, nakata tamaa.Mkuu Raelish,
Pole sana na matatizo, Mwenyezi Mungu akuwekee wepesi na upate nafuu haraka na kwa amani.
Naomba nichukue nafasi hii kwa kuomba radhi kwa kuchelewa kujibu, hasa kwa wale ambao walikuwa wamenishtua nihusike kwa namna moja ama nyingine. Nimeshawasiliana na Raelish kwa kutuma PM, ili atimize baadhi ya vielelezo ili iwe rahisi kujua ni msaada aina gani anahitaji na wa kiasi gani itusaidie sisi kama wanajamvi kukusanya kwa nguvu hiyo.
Nawashukuru na wale wote walio onyesha nia ya kutaka sana kusaidia. Mara baada ya kumaliza mawasiliano na Raelish nitatoa mrejesho mara moja ili tuendelee na nia ya kuwa msaada kwa kiasi fulani katika maisha yake. Maelezo zaidi yatakuja baada ya kujibiwa na Raelish. Asanteni.
Pamoja Sana!
=======
Uongozi wa JamiiForums umejiridhisha na kuafiki kwamba matatizo ya Raelish ni genuine. Hivyo basi, utaratibu wa kuchangia utafanyika kama ifuatavyo;
Kwa wale walioahidi msaada wa kifedha, na hata wasioahidi ila wameguswa na wangependa kushiriki kwenye hili, wanaweza kufanya hivyo kwa kutuma kiasi cha pesa kupitia M-PESA, Namba ya Simu: 0757 525 366 (Jina litakalotokea ni OBEDI MNZAVA).
Tunatanguliza shukrani za dhati kwa nyote mlioshiriki na mnaoendelea kushiriki katika zoezi hili.
- Majina ya walioahidi kuchangia mpaka sasa ni;
Julius Malema Jr Nyalotsi Mokoyo miss chagga Idimulwa Alinda Kipilipili Billie CLEMENCY Kitulo Rugaijamu dagii MTUSIASA rosebud Freeland Deogratius n niester
Wengine pia mnakaribishwa.
Uongozi wa JF unalisimamia jambo hili kwa karibu na kwa umakini sana mpaka mwisho wake. Na litakapofikia, basi mrejesho utaletwa hapa.
Asante.
AshaDii, kwa bahati mbaya sikuuona huu uzi mapema. Samahani huenda tayari mmeshalifanya ila sio mbaya nikifahamishwa kwamba mkakati mzima umekaaje?
Raelish kwenye maelezo yake kasema ada ya mwaka huu imeshalipwa. Ningependekeza tukaweka wazi hapa mihula inaanza lini na kwisha lini na malipo yanayotakiwa hadi atakapomaliza chuo. Hili ni zoezi endelevu, kuna mtu anaweza asiweze kumsaidia leo lakini kesho akawa na huo uwezo.
Hii itasaidia kuhakikisha ndugu yetu anakua na uhakika wa kumaliza chuo. Naahidi kutoa mchango wangu jambo utakua mdogo lakini namshukuru Mungu kwa kunijalia kupata chochote katika shughuli zangu.
Mungu awabariki wote walioonyesha moyo wa kumsaidia huyu jamaa yetu na wale ambao tayari wameshafanya hivyo.
Raelish, Samahani kwa kuwa kimya siku nyingi, na samahani pia kwa kukuangusha kwa kushindwa kuwasilisha katika hili.
Ni washiriki wengi waliahidi kutoa michango kuweza kusaidia. Nasikitika kusema kwamba ni mtu mmoja tu aliyetuma pesa kiasi cha shilingi laki moja na wengine wote walioahidi wapo kimya.
Samaritan, hujachelewa mkuu, bado unaweza kuchangia. Ninaomba tutumie siku 6 kukumbushana ili Raelish akabidhiwe Jumatatu ya tarehe 21 September 2015.
Naomba niwakumbushe @Julius Malema Jr, Nyalotsi, Mokoyo, miss chagga, Idimulwa, Alinda, Kipilipili, Billie, CLEMENCY, Kitulo, Rugaijamu, dagii, MTUSIASA, rosebud, Idimulwa.. maana mlionesha kuguswa na wengine kuahidi.
Naombeni ushirikiano wakuu.
Pamoja Saana!