Sikulaumu wewe, bali namwombea apumzike salama

Sikulaumu wewe, bali namwombea apumzike salama

Toa jina full la chuo ...majina yako full unayotumia chuoni. .namba za mawasiliano za chuo na akaunti namba ya chuo na majina yote ya mkuu wa chuo...usituelewe vbaya matapeli ni wengi mjini wadau apa ni wengi tutachanga usome kutoa ni moyo si utajiri ata Mungu anasema tumjaribu kwa matoleo wadau tumsaidie mwenzetu baada ya kujiridhsha

mkiaandaa utaratibu unikumbushe na mimi.
 
mimi naomba watu tunaowaamini ndio watutengenezee muongozo wa namna ya kuchangia wakiwa na uhakika wa huyu mtu. Invisible tunawategemea.
haya mambo ya mtandao mimi siyaamini kabisa.

nilishalizwa m1 yangu katika harakati za kutenda wema.
 
Last edited by a moderator:
Taarifa zangu zote nimeziweka ndugu zangu
 
Mkuu Mokoyo kinachotakiwa wadau wahakikishiwe huyu ni muhitaji kweli..
 
Last edited by a moderator:
Siku zinazidi kusonga, nami bado navuta subira.... Ahsanten wote mnaoonesha kujali, Kuna watu wanawasiliana nami moja kwa moja kupitia simu yangu, wabarikiwe sana. Na Kuna ahad mbalmbal napokea, na michango kadhaa watu wanaonesha kuniunga mkono,. Sina namna nzuri ya kuwashukuru ndugu zangu,. Ni Mungu mwenyewe awakumbuke. Amina.
 
Pia nawatakia mfungo mwema ndugu zangu waislamu, mnikumbuke ndugu yenu katika maombi yenu.
 
Mokoyo mimi nitatoa msaada pale tu tukipata uhakika wa huyu mtu ni muhitaji . nadhani Invisible atueleze
 
Last edited by a moderator:
Pole.maisha ni mapambano.wako wenye shida zaidi yako usijione uko peke yako.ni kwa sababu watu hawatangazi matatizo yao.
 
Binafsi nawiwa kumsaidia huyu bwana Invisible fuatilieni mtupe mrejesho tuchange,tena kupitia JF M pesa akaunti.
 
Last edited by a moderator:
Mungu azidi kuwabariki, ndugu zangu. Nipo tayari kutoa ushirikiano ili kuondoa wasiwas juu yangu. Ahsanten
 
Yaaah kila mtu ana njia zake kt maisha
 
Pole kwa matatizo uliyoyapata lakini husisononoke sana maana kila jambo litokealo lina maana yake. Huwezi jua ni kwanini mwenyenzi Mungu aliamua kumpumzisha kaka yako.
Inaonekana kuwa ulimpenda kaka yako, na kaka yako alikupenda pia. Hivyo hawezi kukuacha peke yako huko naye na anaangalia kila unachofanya. Nafikiri Kaka yako angefurahi zaidi kama angekuona ukiwa ni mtu mwenye furaha si mtu wa kusononeka. Hivyo jaribu kutomlilia sana kaka yako bali fanya kile ambacho ungefanya wakati akiwa hai kingemfanya awe na furaha zaidi.


Swala la mchango: Niko tayari kuchangia chochote nilichonacho, ila ningependekeza Invisible au dada yangu AshaDii watuhakikishie kuwa huyu mtu anahitaji msaada kweli.

Mdogo wangu Raelish husituelewe vibaya ni kwa vile matapeli ni wengi na wengine tumeishatapeliwa sana hivyo tunachukua tahadhari. Tafadhali sana baada ya Invisble kuhakiki basi husisite kuni"mention" il nikuchangie chochote nilichonacho.

Pesa na mali ni vitu vya dunia tu tutaviacha.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom