Pole sana
Raelish huo siyo mwisho wa maisha,maisha bado yanaendelea na kwa kila jambo mshukuru Mungu kikubwa ni kutazama mbele usiangalie matatizo uliyonayo mwangalie Mungu atakuvusha tu wewe si wa kwanza wapo waliopitia makubwa zaidi na leo ni matajiri wakubwa wanaoheshimiwa na dunia nzima, chukulia hii kama changamoto au ngazi ya kukupandisha juu, hakuna kufanikiwa bila ya kudharauliwa kwanza.
Wenzangu wana JF tujitahidi kujitolea kwa chochote kile tulichonacho,mimi nina wazo kuliko wote tukatuma kila mtu kivyake ni bora ikakusanywa chote kisha akapewa kama vile tunavyokuwa tunafanya mfano ile ya Ocean road, Dada
AshaDii tunaomba utusaidie kuliorganize hili jambo, kaka yetu
Invisible tusaidie kufanya uhakiki wa hili jambo na kuzifatilia details zote kwa uhakika zaidi.