Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Kwa hiyo wewe umemuona khantwe ndio mke bora sawa tu ,kwanza humjui khantwe alivyo bora ungeniuliza nikwambie
Hapana miss nuru penye sifa sifia hiyo haimaanishi wewe si mke bora na yeye nimemsifia kwa uelewa wake tu mengine siyajui, una kawivuuuu!!!! safi sana
 
Aluuuu......... DAUDI 1 sikujua kama uzi huu wa gesti ni wa hadithi nilikuwa naupita tu, uweunaniboost ukitupia mpya. Asante sana.......duh jamani mama na mwana kushindania dudu!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Aluuuu......... DAUDI 1 sikujua kama uzi huu wa gesti ni wa hadithi nilikuwa naupita tu, uweunaniboost ukitupia mpya. Asante sana.......duh jamani mama na mwana kushindania dudu!!!!!!
Pole sana, dudu tamu ujue, karibu sana nitakuwa nakuita
 
We jamaa n boooonge la muandishi, yan imenipa mizuka naifuatilia mpaka nijue mwisho wao, kweli michepuko noma
 
NI SHIIDA!-19

ILIPOISHIA
Jicho lake likagongana na kichupa cha pafyumu. Pafyumu iliyokuwa ikimuumiza kichwa. Pafyumu ya UDV.
“Wee Juliana! Juliana?”
SEREBUKA NAYO SASA...

Aliita mama Juliana kwa ukali.
Ndiyo kwanza Juliana aligeukia upande wa pili huku akiendelea kulia kwa maumivu, maumivu yale ya kipigo kutoka kwa baba yake. Ilibidi Mama Juliana atumie nguvu za mikono na kumvuta kwa nguvu.
“Mama niacheee!!”

“Si nakuita we mwanaizaya! Kumbe ulikuwa ukinisikia hutaki kuitikia, si ndiyo?”
“Hapana mama, sijiskii vizuri mwili wote unaniuma!”
“Hata kama unakuuma, ujue Juliana!”

Mama Juliana akapunguza sauti na kuifanya isikike kwa chini ili mumewe asije akasikia kinachoendelea. Lengo lake ni kumuweka Juliana kwenye kumi na nane ajibu kila kitu kuhusiana na ile pafyumu aliyoitoa kwenye mkoba wake. Pafyumu ya UDV.
“Nakusikia mama!”

Juliana alijiweka vizuri. Hakuwa amebadili nguo tangu ametoka Bagamoyo alipokuwa na Bitungu. Alishusha miguu yake kwenye kitanda kisha akakaa.
“Nakusikia mama.”

“Mwanangu hivi kwa nini unapenda kufanya kitu kwa makusudi? Si nilikwambia usitoke?”
“Ndiyo mama ila walikuja marafiki za...”
“Hivi mara ngapi haohao marafiki zako wanakupotosha we bado unafuatana nao. Kwa nini wewe usiwapotoshe mpaka wao ndiyo wakufanyie hivyo. Halafu mwanangu mpendwa unajua kabisa baba yako ana hasira.
“Najua mama.”

“Kama unajua kwa nini sasa mwanangu unakosea!”
“Nisamehe mama!”
“Mimi nilishakusamehe hata kabla baba yako hajakuchapa na mkanda. Ila mwanangu naomba uniambie mimi kama mama yako.”
“Nakusikia mama.”
“Una mpenzi?”

Juliana alionyesha kushtuka. Alisogea kwenye kile kitanda. Woga ulimshika kwa muda huku macho akiyatoa.
“Hapana mama, bado najitunza!”
“Kweli unajitunza mwanangu Juliana?”

“Ndiyo mama wala usiwe na wasiwasi na mimi!”
“Sasa mwanangu usiku wote huu tangu mchana ulikuwa wapi?”
“Marafiki mama...”

“Haya hilo tuliache, mwanangu hii pafyumu nani aliyekununulia?”
Juliana alishtuka kwa mara ya pili. Aliona sasa huenda mama yake alimuona kipindi kile Bagamoyo akiwa katika kupanda bajaji katika ile gesti alipokuwa na Bitungu. Mama Juliana alimuonyeshea Juliana ile pafyumu.

“Mama hiyo niliinunua mwenyewe!”
“Wapi? Na nani alikupa pesa?”
“Nilijibanabana mama.”

“Hii ni pafyumu ya kiume mwanangu na wewe haikufai.”
“Nimekuelewa mama ila miye niliipenda harufu yake...”

Wakiwa katika majibizano, bila hata ya hodi mara baba Juliana akawavamia. Baba Juliana aliyekuwa ameshikilia simu mbili, moja yake moja ya mke wake. Kitendo cha kuingia akamkuta mama Juliana akiwa bado ameishikilia ile pafyumu huku akiwa amemnyooshea Juliana.

“Ina maana huyo mpuuzi bado hajalala siyo?”
“Jamani! Nina maongezi naye kidogo ila atalala tu.”
“Na hiyo pafyumu uliyoshika ndiyo maongezi yanaingia vizuri siyo?”
“Hapana mume wangu.”

“Embu leta, leta!”
Baba Juliana akaiwahi ile pafyumu na kumpokonya mkewe. Akawa ameshagundua kuwa ni ya kiume.
“Haya mnaweza kunieleza hii ya nani?”
Wote kimya...
“Si naongea na wewe mama Juliana?”
“Mume wangu embu basi punguza hizo hasira.”

“Msinichanganye? Ni nani anayetumia pafyumu ya kiume kati yako na Juliana?”
Juliana aliendelea kutetemeka. Alijihisi kojo kumtoka kwani tayari kitumbua kilikuwa kimedondoka katikati ya mchanga, aliona ni bora alivyogundua mama yake kuwa ni ya kiume kuliko alivyogundua baba yake.

Alikuwa katika kusitasita huku akitaka kusema ukweli wote kuhusu uhusiano wake na mama yake pamoja na Bitungu ili litakalotokea litokee.
“Hiyo pafyumu alin...”

Kwa haraka mama Juliana alichezwa na machale. Akamuwahi Juliana kabla hajamalizia kuongea.
“Mume wangu hii hapa nimeipata huko kwenye vikoba nasikia ni nzuri kwa mabinti hasa mtoto wetu huyu, ndiyo nikawa nimemletea kama atapendezwa na harufu yake nimuachie.

“Unasemaje mama Juliana? Ina maana ushaniona mtoto siyo? Haya sawa umemletea mwanetu safi! Embu nielekeze ni wapi wanapouza pafyumu ikiwa robo?”

Kabla mama Juliana hajajibu, simu ikaita. Baba Juliana akaangalia mkononi na kugundua ni simu ya mama Juliana ndiyo ilikuwa ikiita huku jina likiandikwa Bitu. Akaichukua na kuipokea kisha akakaa kimya bila kuongea.
***
Muda wote Bitungu alikuwa hana raha. Aliwaza sana maneno aliyoambiwa mara ya mwisho na mama Juliana. Maneno juu ya pafyumu. Akili zote zilimuhama na kuona huenda anajuana na Juliana.
“Haiwezekani? Lakini kwa nini aniulize habari za pafyumu?”

Alijiuliza Bitungu na kujijibu mwenyewe kisha akainuka pale kitandani na kuelekea kwenye meza ambapo aliiweka ile pafyumu yake ya UDV. Alipofika hakuona chochote.
“Ina maana kuna mchezo nafanyiwa au? Sasa itakuwa wapi?”

Bitungu aliendelea kujiuliza mwenyewe. Alichokifanya aliichukua simu yake na kuanza kupiga namba ya mama Juliana. Iliita bila kupokelewa hadi ikakata, akajaribu kupiga kwa mara nyingine tena ikapokelewa.
“Mpenzi wangu mbona hupokei simu yangu? Embu niambie pafyumu yangu ya UDV uliichukua?”

Tobaaaaaa!!!!!! mtu kaumbukaaa tuungane jumamosi kupata uhondo huu
 
Aluuuu......... DAUDI 1 sikujua kama uzi huu wa gesti ni wa hadithi nilikuwa naupita tu, uweunaniboost ukitupia mpya. Asante sana.......duh jamani mama na mwana kushindania dudu!!!!!!
Serebuka nayo hapo juu
 
Back
Top Bottom