Simulizi: Kisasi cha Haki (13+) - Sura 2

Simulizi: Kisasi cha Haki (13+) - Sura 2

Babas Babas

New Member
Joined
Oct 12, 2026
Posts
2
Reaction score
1
KISASI CHA HAKI
Mtunzi: Mr Babas
Mawasiliano: +255 758 276 010 Whatsapp pekee

Tulipoishia sehemu ya kwanza,Walipokaribia getini getu alisikia akiitwa nyuma yake alipogeuka alikua ni karlosy akiwakimbilia ghafla gari ilikuja na kumgonga karlosy kisha kuondoka.

Sehemu ya Pili

"mama angu karlosy" getu aliongea kwa maumivu huku akikaa chini,suzi alimkimbilia karlosy alipotupwa na gari,

"karlosy! karlosy!" suzi alimuita karlosy,alipoona kimya alianza kumsukuma kifuani kuona kama ataamka kwa maana hakuwa na kidonda wala kutokwa na damu,"karlosy! karlosy! karlosy!" Suzi alipiga makelele akilia huku watu wakisogea eneo alilopo karlosy,na walinzi wa geti la chuo walisogea kumtazama,

"amekufa?" kijana mmoja mchoma chipsi aliuliza watu waliomzunguka,

"mtoeni huyo binti sasa" mzee mmoja alisema,akaja mama mmoja na kumuinua suzi kisha kutoa khanga yake akaikunja na kumuwekea karlosy kichwani,

"nimepiga simu polisi watafika sio mda hapa" mlinzi alisema,

"sasa wewe unaanza kupiga simu polisi baada ya kupigia ambulance ije" mama aliyemshika suzi alisema kwa hasira,

"mama huruhusiwi kumpeleka muanga hospitali kabla polisi hawajajiridhisha" mlinzi alisema,yule mama akatoka kwa hasira na kuita bajaji,

"bajaji! bajaji! njoo mwanangu, mbebe yule kijana tumpeleke hospitali" mama mmoja kwa jina la mama magreth aliyekuwa na saluni karibu hapo alimwambia dereva bajaji,bila hiyana dereva bajaji alimbeba karlosy chapu na kumpeleka hospitali wakiwa pamoja na suzi na getu,

"wanangu poleni ni rafiki yenu ee?" mama magreth aliuliza kwa sauti ya kuliwaza,

"ndio mama" suzi alijibu,

"yani wale wajinga eti sheria! Sheria gani!mtu afe tunamuangalia tu" yule mama alisema

"ndo walivyo mama sijui ni sheria za wapi hizi yani mpaka polisi wafike ndo wathibitishe kama kweli sijui!" dereva bajaji alichangia,walipofika hospitali yule mama alitoka na kuongea na daktari mmoja kqa sekunde kadhaa kisha kikatoka kitolori cha kubebea wagonjwa wakambeba karlosy na kumpeleka wodini,

"nyie nitaomba mkae nje kidogo ili tumpe matibabu" daktari alisema,

"sawa hamna shida daktari" mama magreth alijibu,

"asante sana mama tunashukuru kwa msaada wako" getu alisema kwa sauti ya upole iliyonyong'onyea,

"msijari hata",baada ya dakika kadhaa walionekana polisi eneo la hospitali baada ya maongezi na wahudumu wa hapo walionganisha mpaka wodi aliyolazwa karlosy na kuwakuta mabinti wawili pamoja na mama,polisi mmoja kwa jina la johnson alikuwa akimfahamu mama magreth na kumsalimia,

"aaah mama kwema" johnson alisalimia,

"mbaya mwanangu ninamgonjwa hapa" mama magreth alisema,

"aah pole ndo huyu aliyepata ajali?" johnson aliuliza,

"ee ndo huyohuyo ila nashangaa naambiwa siwezi mleta hospitali mpaka mfike, angetufia?" mama magreth aliongea kwa hisia,

"aah yani hapo mama siwezi kukuelezea maana hizi sheria tumezikuta sie,lakini hali ikoje?"

"ndo tunasubiria hapa daktari amesema tusubiri hapa" mama magreth alisema,

"aaaha basi sawa na hawa mabinti?" johnson aliuliza,

"hawa ndo walikuwepo mda wa hiyo ajali" mama magreth alijibu

"anha basi naomba mkitoka hapa mje kituoni tuchukue taarifa,

"sawa" getu na suzi walijibu,baada ya muda kupita daktari alitoka,

"vipi mwanangu hali ikoje?" mama magreth aliuliza,

"tunashukuru mungu hali iko sawa sasa" daktari alisema,

"eeh asante mungu" mama magreth alisema,"sasa wanangu naomba niwakimbie kidogo mtakua mnanipa taarifa sawa,mnipe na namba zenu za simu"

"sawa" suzi alijibu na kuchukua simu ya mama magreth na kuandika namba zao,baada ya hapo waliruhusiwa kuingia ndani kumuangalia mgonjwa,

"karlosy pole" getu alisema lakini karlosy alikua akimtazama tu kutokana na kutoweza kuongea kwa muda huo, baada ya kumuangalia mgonjwa mida ya saa nne usiku getu pamoja na suzi walitoka ili warudi hostel kupumzika,

"sasa wazazi wake tutawapataje tuwape taarifa??" suzi aliuliza huku wakiwa wamesimama nje ya ile hospitali,

"ngoja tufike hostel nitoe laini niweke kwenye simu yangu ili tuwapigie" getu aliongea kwa kujivuta na macho yake yakiwa yamevimba,

"aaha kumbe simu yake unayo,umefanya jambo la maana sana" suzi aliongea huku akipepesa macho kama atapata boda wa kuwapeleka hostel,wakiwa wamesimama hapo simu ikaanza kuita aliekua anapiga ni mama magreth,

"haloo" suzi aliitika,

"bado mpo hospitali??" mama magreth aliuliza,

"ndio ila ndo tunatoka turudi hostel" suzi alijibu huku akisogea mbele kuangalia bodaboda,

"msiondoke nipo karibu hapa,nakuja kuwachukua niwapeleke" mama magreth alisema,

"sawa tutashukuru sana" suzi alijibu na kukata simu,

"amesemaje??" getu aliuliza huku akimtazama suzi,

"anakuja kutuchukua" suzi alijibu na kukaa kwenye kibaraza cha hospitalini,dakika chache badae gari iliingia hospitalini hapo na muda huohuo gari ya lecturer joseph iliingia,na lecturer joseph baada ya kuwaona alisimamisha gari na kushuka kuwafuata,

"nimepata taarifa ila nilikua mbali,nikasema nikifika naonganisha moja kwa moja hospitali,vipi lakini mgonjwa anaendeleaje??" lecturer joseph alisema huku akiwatazama,

"tunashukuru Mungu anaendelea salama" getu alijibu baadaa ya kuona suzi kapigwa na butwaa kwa ujio wa lecturer huyo,

"jambo jema" lecturer joseph alisema huku akimuangalia suzi,mara nae mama magreth alishuka na kuwafuata,

"habari" mama magreth alimsalimia lecturer joseph huku akimtazama kwa makini,

"salama" lecturer joseph alijibu,

"mama,huyu ni lecturer chuoni kwetu" getu alimtambulisha lecturer kwa mama magreth huku suzi akiwa mpole kama pilitoni,

"anha nashukuru kukufahamu" mama magreth alisema akimpa mkono lecturer joseph,"sasa tuondokeni" mama magreth alisema,

"aah hamna ngoja niwapeleke tu" lecturer joseph aliitikia huku akiwatazama kuona watasemaje,

NB:FULL ipo whatsapp na vipande vitazidi kuja ndani ya jukwaa letu.

Asante kwa upendo usio kifani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom