Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Daudi1 tuletee basi???wewe umeng'ang'ania ile ya missed call tu hii umeipa kisogo
 
Last edited by a moderator:
Nyie subirini mpaka magazeti ya shigongo yatoe ndo ataipakia!
 
Wakuu msihangaike sana kusubiria! Hivi hamkumbuki kilichotokea kwenye zile stories mbili "tanga raha" name " mpangaji"? Mtasubiri sana
 
NI SHIIDA!-17

ILIPOISHIA
Mama Juliana aliishiwa pozi, ujanja wote wa maneno ulikuwa umeshamwishia, alishindwa kujiongeza zaidi ya kuamua liwalo na liwe. Aliichukua simu yake na kuanza kumpigia Juliana kwa papara huku akiiweka loud spika ili wote wajue eneo alipo.
SEREBUKA NAYO SASA...


Mikono yake ilionyesha wazi kutetemeka hasa maeneo ya vidoleni, muda wote baba Juliana alikuwa pembeni yake akimuangalia tu. Simu iliita mpaka ikakata yenyewe, akajaribu zaidi ya mara mbili lakini bado haikupokelewa.

“Sasa atakuwa ameenda wapi Juliana huyu?”
“Hayo maswali usiniulize mimi, ninachotaka kwanza mlango ufunguliwe kisha ndo mnijibu vizuri kwa nini mnaondoka tena na funguo zote!”
“Jamani baba Juliana! Si nilishakwambia funguo zangu zipo ndani!”
“Fungua sasa!”
“Nitafunguaje?”

Baba Juliana bado alikuwa na hasira kali. Alichokifanya ni kujisogeza kwenye ukuta na kutaka kukaa kwa mara nyingine, kabla hajakaa wazo likamjia. Akajiongeza!
“Naenda kumuita baba Latifa!”
“Wa nini?”

“Aje aubomoe tu huu mlango!”
“Halafu ukishabomolewa?”
“Tunaingia, anaurudishia!”

“Jamani baba Juliana embu kuwa mvumilivu basi hata kidogo, Juliana kama ametoka si atakuja kuliko kuanza kumuita baba Latifa aje avunje.”
“Ndo nishasema sasa!”

Baba Juliana hakutaka kusikia lolote zaidi ya kunyanyuka na kuongoza moja kwa moja mpaka kwa baba Latifa ambapo alimkuta na baada ya dakika chache alirudi naye kwake akiwa na vifaa vyote vya kubomolea mlango.

“Fanya uwezavyo, uvunje tu tuweze kuingia halafu utaurudishia!”
“Haina shida bosi!”
“Hapana baba Latifa, Hapana usiuvunje!”
“Wee mwanamke! Embu muache baba Latifa auvunje huo mlango.”
“Baba Juliana kwa nini hutaki kunisikiliza mkeo!”

“Mimi si ndo baba Juliana, baba mwenye nyumba? Haya fundi vunja nimesema na kama pesa nakulipa mimi wala si huyu mwanamke?”

“Baba Juliana? Haiwezekani hata kidogo kuuvunja mlango, haiwezekani”
Mama Juliana alishindwa kumdhibiti baba Latifa. Akaamua aache baba Latifa auvunje kisha wakaingia ndani na kufikia sebuleni moja kwa moja huku wakimsubiri Juliana.
***
“Sweet! Sweet! Embu amka!” alisikika Bitungu akimwamsha Juliana. Juliana ambaye usingizi ulikuwa umemchukua baada ya kupigishwa gwaride la kufa mtu.
“Hee! Kwani saa ngapi sasa hivi?”

“Saa tatu kasoro usiku, ujue tumepitiwa na usingizi halafu mlio nilioutegesha kwenye simu kumbe nilikosea kurekebisha muda!”
“Unasemaje Bitu!”
“Simu sweet!”

“Simu eeh! Umenifanyia makusudi Bitungu mpenzi wangu, ona sasa na funguo za nyumbani ninazo, mama hawezi kunielewa!”“Funguo! Ina maana umeondoka na funguo za nyumbani kwenu? Lakini si atakuwa nazo nyingine!”

“Wee humjui tu mama yangu, siku moja utamuona! Mama aliniachia nyumba na miye nikajifanya mbishi kwa ajili ya mapenzi yako, nikafunga na kuja na ufunguo, hizo hapo kwenye kimkoba changu.”

Juliana aliongea kimtego huku Bitungu asijue mama yupi anayezungumziwa. Aliinama chini kisha akakiinua kichwa na kuangaza kwenye kile kimkoba na kuanza kuuangalia ufunguo wa nyumbani kwao. Akahamia kwenye simu ambapo aliichukua na kukutana na missed call zaidi ya nne zote zikiwa zimetoka kwa mama yake.

“Nimekwisha mimi, nimekwisha leo!”
“Umekwisha kwa kipi?”“Ona sasa! Kumbe alikuwa akinitafuta kwenye simu!”
“Fanya basi uvae, uende fasta!”

Juliana hakutaka cha kusikiliza tena, hata kuingia bafuni kujimwagia maji aliona ni kazi kubwa zaidi ya kuchukua nguo zake na kuvaa haraka-haraka, akaitumbukiza ile simu kwenye kimkoba chake kisha akatoka nduki bila hata ya kumuaga Bitungu vizuri.

Mpaka inafika saa nne na nusu Juliana alikuwa nje ya nyumba yao. Taa zote za ndani zilikuwa zimewashwa na hakuelewa vizuri imekuwaje wakati funguo anazo.
“Au mama alikumbuka kuchukua funguo zake?”

Alijiongelesha Juliana huku akipiga hatua mdogomdogo kuelekea mlango wa mbele. Akiwa katika mwendo wa kunyata, wazo likamjia. Wazo la kuelekea dirishani kwa wazazi wake na kusikilizia kujua kinachoendelea. Alipofika kimya kilikuwa kimetanda na wala taa hazikuwa zimewashwa hivyo akabadili wazo na kuelekea sebuleni moja kwa moja. Kabla hajafika kwa mbali akasikia sauti za wazazi wake wakiteta!

“Hadi sasa, hakuna cha huyo Juliana wako wala nani? Kwa hiyo mlitaka kunilaza nje hadi sasa hivi, kama nisingepata wazo la kumchukua baba Latifa avunje ingekuwaje?”
“Baba Juliana jamani si yameshakwisha!”

“Hayawezi kuisha hadi nijue Juliana yupo wapi hadi sasa hivi? Na utakuwa unajua hutaki kuniambia tu!”
“Najua chochote nitakachokwambia bado utaniona muongo tu, subiri labda akija!”

Juliana alizidi kuogopa. Alitamani arudi zake Bagamoyo akajichimbie na Bitungu waliendeleze gwaride kuliko kuingia ndani ambapo aliona kumeshachafuka. Akili yake ilizidi kuchemka huku mkono wake mmoja ukiwa umekishikilia kitasa cha mlango tayari kwa kukifungua.

“Juliana?” aliita baba Juliana kwa hasira baada ya kuhisi kitasa cha mlango kimetikisika.
Je baba Juliana atamfanyaje Juliana?
Juliana atasema ukweli alipokuwa?
 
NI SHIIDA-18

ILIPOISHIA
Akili yake ilizidi kuchemka huku mkono wake mmoja ukiwa umekishikilia kitasa cha mlango tayari kwa kukifungua.
SEREBUKA NAYO SASA...

Juliana alisita kufungua kile kitasa, akabaki ameduwaa huku mkono akiurudisha.
"Nani unayefungua mlango kama siyo Juliana?" alisikika baba Juliana.
"Mh! Baba Juliana?, hata mlango haujafunguliwa unafikiria Juliana tu!"
"Ndiyo! Sa we' unafikiri atakuwa nani?"

"Sidhani kama atakuwa Juliana, embu ngoja nikafungue."
Mama Juliana aliinuka na kusogea hadi mlangoni kisha akafungua ule mlango na kukutana uso kwa uso na Juliana. Juliana aliyeonyesha kutetemeka asijue la kufanya.
"Haya ulikuwa wapi?"
"Mama nil..."

Kabla Juliana hajaanza kujitetea, baba Juliana naye aliinuka kwenye kochi na kuwafuata pale mlangoni.
"Pumbavu wee ingia ndani mwenyewe!"
"Baba ndiyo naingia lakini...."
"Lakini nini? Nimesema ingia..."

Juliana aliingia huku wazazi wake wakiwa nyuma yake. Aliongoza moja kwa moja hadi kwenye kochi kisha akaketi huku akishikashika vidole vyake vya mikononi.
"Niambie ulikuwa wapi na kwa nini uliondoka na funguo?" alianza kuhoji mama Juliana kwa ukali.
"Mama niliondoka na marafiki zangu walikuja kun..."
"Kimya! Ishia hapo hapo! Na ufunguo ukauacha wapi?"
"Nilijua nitawahi kurudi."

Juliana akiwa katika kujitetea. Yale majibu yalimkera sana baba yake. Alichokifanya aliongoza chumbani kwake moja kwa moja na kurudi akiwa na mkanda wa suruali kisha akataka kumvaa Juliana.
"Nipishe mama Juliana! Nipishe nimuadhibu mpumbavu huyu."

Roho ya huruma ilianza kumuingia mama Juliana. Akajikuta amemkumbatia Juliana ili aepukane na kipigo cha mkanda kutoka kwa baba yake. Akiwa bado katika kumkumbatia mama Juliana akahisi kitu puani mwake. Harufu kali ya ‘pafyumu' kutoka kwa Juliana ikamuingia puani, akamwachia Juliana kwa hasira.

"Muadhibu, mpige tu pumbavu huyu!"
Baba Juliana alimvaa Juliana na kuanza kumpiga mfululizo. Juliana alijitahidi kujifunika kwa mkoba wake lakini kichapo kilikuwa kikimuingia vilivyo.
"Baba nisamehe, sitorudia tena! Nisamehe!"

Baada ya kumpiga kwa muda, baba Juliana aliutupa ule mkanda pembeni.
"Haya nenda chumbani huko."

Muda wote mama Juliana alikuwa amepigwa na butwaa. Kuanzia Juliana anapigwa hadi anamaliza kupigwa bado alikuwa hajielewielewi, ile harufu ya pafyumu aliyoisikia kwa Juliana ilimpagawisha.
"Ina maana alikuwa kwa Bitu wangu?" aliwaza na kuwazua lakini bado hakupata jibu.
"Bitu kumbe msaliti kwangu? Kujitoa kote kule mpaka Bagamoyo ananisaliti bado?" Akili ya mama Juliana bado ilikuwa haipo sawa.

"Na wewe vipi?" alihoji baba Juliana baada ya kumuona mama Juliana amezubaa mwenyewe.
"Hapana mume wangu, namfikiria huyu mtoto kwa jinsi alivyobadilika, yaani Juliana wa kutujia usiku namna hii?"
"Wee si ndo uliyemdekeza, na huu ni mchezo wenu wa kurudi muda huu wala hakuna cha kujitetea hapo."

"Hapana mume wangu."
"Na huyo mtoto ana bahati naumwa la sivyo ningemuua leo."
Baba Juliana bado alikuwa katika hasira. Aliondoka pale sebuleni na kuelekea chumbani kwake huku akimuacha mama Juliana peke yake pale sebuleni.
Alichokifanya mama Juliana ni kukaa kwa muda kwenye kochi kisha akaichukua simu yake na kuanza kutuma meseji kwa Bitungu.

"Mambo baby wangu! Nilifika salama, nakuwaza sana hadi nakosa raha!"
Akaituma na baada ya muda, Bitungu akaijibu.

"Hata mimi Sweet wangu, siwezi kuisahau mechi ya leo. Si unakumbuka hata uwanja tuliochezea, yaani hapa nimejilaza hoi sijiwezi natamani ungekuwepo ungenikandakanda kwa maji ya vuguvugu."
Mama Juliana aliisoma meseji hiyo na kuiangalia mara mbilimbili kwa hasira za juu. Akajiongeza kuwa huenda Bitungu amechoka zaidi kwa kukutana na Juliana japokuwa hakuwa na hakika zaidi ya kuifananisha harufu ya pafyumu. Akamwandikia tena Bitungu meseji.

"Baby wangu hivi ile pafyumu yako inaitwaje tena? Maana nimeipenda harufu yake nataka kesho nikainunue ili nikiwa naitumia niwe nakukumbuka."
Mama Juliana alikuwa mjanja wa maneno, aliweza kuyaungaunga na kumdanganya Bitungu. Akaingia kwenye mstari na kumjibu.

"Waaaaooh! Sweet wangu, ina maana leo hii umeisahau? ile inaitwa UDV."
Meseji ikamfikia mama Juliana. Ikamuuma sana baada ya kujua ni UDV ambayo harufu yake ni ile aliyoisikia kwa Juliana. Alichotaka kujua ni kupata uhakika wa jina la pafyumu. Aliondoka pale sebuleni na kuongoza moja kwa moja hadi chumbani kwa Juliana. Akamkuta amejitupa kitandani huku akiendelea kulia kwa uchungu.

"Wee Juliana? Embu acha uchuro wako hapa!"
Aliongea mama Juliana huku akifuata mkoba ule wa Juliana na kuanza kupekua ndani yake. Jicho lake likagongana na kichupa cha pafyumu. Pafyumu iliyokuwa ikimuumiza kichwa. Pafyumu ya UDV.
"Wee Juliana! Juliana?"
Je nini kitaendelea? tuungane jumatano wiki ijayo......
 
Back
Top Bottom