Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

NI SHIIDA!-16

ILIPOISHIA
Kitendo cha Bitungu kuongozana na Juliana hadi chumbani, Juliana alimuwahi na kumsukuma hadi kitandani na kuanza kumshambulia kwa mabusu kadhaa. Wakiwa katika mahaba mazito mara simu ya Bitungu ikaita...
SEREBUKA NAYO SASA...


Kabla Bitungu hajaipokea ile simu, Juliana akawa ameiwahi na kuishika huku akitaka kubonyeza kitufe cha kupokelea.“Nooo! Nipe simu yangu mpenzi!”
“Hapana sikupi mpaka nijue anayekupigia.”

“Sasa sweet tumefikia huko! Najua tu watakuwa ni wafanyakazi wenzangu tu, nipe pliiz!”
“Hata kama!”
“Nipe basi!”

“Nimekwambia sitaki, embu kwanza.”
Juliana alikuwa wa kwanza kujua aliyekuwa akipiga simu ile ya Bitungu. Jina ambalo lilikuwa limeseviwa katika ile simu lilikuwa limemshtua vilivyo. Alichokifanya ni kuangalia tena ile namba mara mbilimbili na kugundua kuwa ni mama yake ndiye aliyekuwa akipiga, akaikata kisha akampa Bitungu.
“Shika lisimu lako!”

Harakaharaka Bitungu aliichukua na kuangalia aliyekuwa akipiga lakini kabla hajapokea ikawa tayari imeshakatika. Hasira zikamshika baada ya kugundua aliyepiga ni mama Juliana, akabaki akimtolea macho Juliana kwa hasira.
“Umeridhika sasa!”
“Kwa kipi hasa?”

“Si umekata simu ya mfanyakazi mwenzangu!”
“Mfanyakazi mwenzako?”
“Ndiyo! Unajua alichokuwa akitaka kuniambia?”
“Ujue mpenzi sipendi kabisa nikuudhi na hata wewe uniudhi.”
“Kumbe unajua hilo! Kwa nini uniudhi?”
“Nisamehe basi!”

“Haya nimekusamehe, tupumzike basi!”
“Bitu...”
“Niambie!”
“Mi sitaki kupumzika bwana! Natamani nikukumbatie muda wote tu!”
“Najua mpenzi lakini leo tulikuwa na kikao cha muda mrefu, hapa nilipo nimechoka sana mgongo kwa kuinama kuandika. Acha tupumzike kwanza na hata akili yangu haijakaa sawa...
“Hivi kweli Bitu unanipenda?”
“Ndiyo kwani vipi?”

“Hapana mtu unayempenda huwezi kumwambia hivi!”
“Lakini...
“Lakini nini?”
Wakiwa katika maongezi huku Bitungu akiwa hana dalili ya kucheza mechi ya aina yoyote kutokana na uchovu aliokuwa ameupata baada ya kumaliza kucheza mechi ngumu ya mchangani na mama Juliana. Kila akijaribu kujiweka vizuri ndiyo kwanza alikuwa akichokozwa na Juliana.

“Ujue Bitu... nahitajika kurudi nyumbani na hii yote nimekuja kwa ajili yako kwa nini unifanyie hivi... kwa nini uutese moyo wangu jamani, nielewe mpenzi...”
“Sweet, nakuomba kesho uje nitakuwa free kabisa!”
“Basi hata mara moja nirudi nyumbani inatosha!”
“Mara moja nini?”

“Mara moja umuagize mwanajeshi wako afanye mashambulizi.”
Bitungu aliendelea kuwa mgumu hali iliyomfanya Juliana aendelee kuumia zaidi kila akikumbuka alivyokuwa akishuhudia mechi kati ya Bitungu na mama yake.

Mechi waliyokuwa wakiichezea mchangani tena wakiwa na jezi. Baada ya kusumbuana kwa muda, Bitu aliamua kumkubalia Juliana ambapo alimuweka sawa na kuanza kufanya mashambulizi ya kupima uwezo wake wa kulicheza gwaride kabla hajavua rasmi magwanda na kuingia vitani.
***
Usiku ulizidi kuingia. Hadi inafika saa mbili za usiku si mama Juliana wala Juliana waliokuwa wamefika. Siku hiyo baba Juliana alijuta kurudi mapema kwani tangu saa kumi na mbili za jioni alikuwa nyumbani akiwasubiri. Homa aliyokuwa akiisikia ilimfanya kuachana na pombe siku hiyo na kuwahi kurudi ambapo alikuta milango yote ya nyumbani kwake ikiwa imefungwa. Hatimaye mama Juliana akatokea na kumkuta mumewe akiwa amekaa kibarazani kwa hasira.

“Umetoka wapi sasa hivi?”
“Baba Juliana ndiyo salam kweli hiyo?”
“Sitaki salam, kunigandisha muda wote na simu umezima ndiyo nini?”
“Simu imezima?”
“Ndiyo! Umeamua kunizimia simu siyo?”
“Hapana sijazima simu, siyo hii hapa iko on?”
“Sipendi upumbavu mama Juliana, haya nifungulie mlango.”

“Kwani umefungwa? Nilimuacha Juliana, au atakuwa ndani amepitiwa na usingizi?”
“Angekuwa amelala tangu saa kumi na mbili si angenifungulia, nimegonga mpaka nimechoka. Ujue msiniletee ujinga!”

“Hapana mume wangu, miye funguo zangu za akiba zote niliziacha nikijua nimemuacha Juliana na nilimwambia kuwa asitoke narudi naelekea kwenye vikoba.”

“Leo mtaniambia vizuri mlikuwa wapi, haiwezakani mnifanyie ujinga wa namna hii kwa kunigandisha, kumbe siku zote ninazochelewaga kurudi nyumbani mnajiachia namna hii siyo?”
“Hapana mume wangu!”
“Hapana nini?”

Mama Juliana alijitahidi kudanganya lakini ndiyo kwanza baba Juliana alizidisha ukali. Hakutaka kusikia lolote zaidi ya kufunguliwa kwanza mlango halafu aelezwe ukweli juu ya Juliana alipo. Woga ulishaanza kumshika huku akitetemeka mwili asijue afanye nini ili mlango ufunguke, akili ya haraka aliichukua simu yake na kutaka kutoka eneo lile.

“Embu ngoja niiulizie hapa jirani kwa mama Latifa,”
“Uulizie nini wakati kote nimeshaulizia wamesema hakuna ufunguo na mtu wa mwisho kuonwa akitoka alikuwa Juliana.”

Mama Juliana aliishiwa pozi, ujanja wote wa maneno ulikuwa umeshamwishia, alishindwa kujiongeza zaidi ya kuamua liwalo na liwe. Aliichukua simu yake na kuanza kumpigia Juliana kwa papara huku akiiweka loud spika ili wote wajue eneo alipo.

USICHOKE KUFUATILIA UHONDO HUU...............
 
Duuuh loud speaker tenaa??? Halahala yule mtoto asije kuropoka.....
 
Huku kukatana stimu sasa lini tena.kama vipi piga kimya tu.
 
Back
Top Bottom