Siku moja na Sir Andy Chande

Rest in Peace our fallen HERO, Sir Andy Channde.
 
JokaKuu....muandike sasa historia ya Tanzania. Kuna watu wenye nia ya kuipotosha

..asante.

..mimi siyo mwandishi, ila napenda kusoma historia.

..nimebahatika kusoma Kitabu cha maisha ya Andy Chande.

..walikuwa matajiri wakubwa kabla mali zao hazijataifishwa.

..Andy Chande ameoa kwenye familia ya Madhvani, matajiri( sugar estates & brewery)wakubwa Uganda.

..Madhvani nao walitimuliwa toka Uganda na Iddi Amin miaka ya 70.
 
Mama Janguo ni mtu wa Kigoma kama Asha Baraka
 
William...
Hapana haifai kuleta hayo kwenye taazia si uungwana.
Mimi nimemweleza Chande kwa ile siku moja.

Bado unayo nafasi na wewe ukamweleza vyema kupita mie kwa kuwa
ulifanyanae kazi Unga Limited.
Mohamed: soma kitabu cha Chande kinajieleza vizuri. Hayo Mashirika kama THA na TRL n Unga Limited yana historia ndefu na taratibu thabiti yalikuwa almost elitist, ya kikoloni. Bodi hizo zilikuwa ni kama baraza la maaskofu hawezi akaingia kila tom dick and harry. Nilistuka ulipodai kijana mdogo uingizwe Bodi just like that, ndipo nikakumbuka wewe na Dau ni "siasa kali" umechukua nafasi kupenyeza mnyukano wa "club" yenu na "club" ya chande (ambayo kama ungeendelea ungeisukuma kwa Nyerere). Yaani naamini kabisa there was no such Board meeting at all, ni nafasi tu umeitumia kujenga club yako huku ukinogesha ajenda. Kwenye kitabu cha Sykes umeongea mengi sana mazuri lakini hukuongea jinsi baada ya kutaifishwa mabenki na biashara kuu kuna wahindi wazalendo walibaki kumsaidia Nyerere kuongoza NBC, GAPEX, TMC, na biashara zingine: kina Jamal, Haridas, Chande, Kassum nk. Kama Chande anakuuma kiasi hicho ungemtaja kwenye kitabu chako kwa sababu alishiriki sana harakati za ukombozi huo, lakini he was in the wrong "club". Samahani kama nimekosea lakini ulinistua kusema uliachiwa uingie kikao cha bodi.
 
Pia Mzee Janguo alikuwa mkurugenzi ''relwe'' na pia katibu mkuu wizara fulani kama sijakosea,hao watoto wake walikuwa wakipaishwa sana kwenye Twanga na Mzee wa Farasi ,pamoja na marehemu Banza mtoto wa Sinza
Kwenye video ya Tunda special ya Muumin Mwinjuma yupo Idd Janguo pia na micheni yake kutoka Texas.

Na video za awali za Twanga Haji Janguo naye aliuza fuvu kwenye zile video akiwa na kamarade Ally Choki.
 
William...
Unaandika vizuri na nakuelewa vyema.
Sina sababu ya kusema uongo.

Niliyokueleza ndivyo ilivyotokea.
Si hilo tu.

Nimewahi vilevile kuwa katika ''delegation,'' ya Bandari iliyokwenda Lusaka,
Zambia kuhudhuria mkutano ambao wajumbe ni wakurugenzi.

Kulikuwa na Kamati ikiitwa Transport Coordination Committee ambayo
ilijumuisha THA, TAZARA, TRC na wengine sikumbuki maana miaka imepita
hawa ni watumia bandari na wasafirishaji kutoka Zambia, Malawi na Congo.

Tulikuwa na mikutano tukifanya Malawi na Zambia kila baada ya muda hivi na
ikizunguka kati ya nchi hizo.

Azma ya mikutano hii ilikuwa kujaribu kuleta ufanisi Bandari ya Dar es Salaam
kwa kukutana mara kwa mara na kujadili matatizo ya usafirishaji wa mizigo.

Waliokuwa wanahudhuria vikao hivi katika nchi hizo ni Mkurugenzi Mkuu,
Mkurugenzi wa Masoko na Mkurugenzi wa Utekelezaji.

Ikatokea kuwa Mkurugenzi wa Masoko Dr. Dau alikuwa Ulaya na ofisi ninakaimu
mimi.

Kwa adabu za ofisi nilimpelekea mkubwa wangu taarifa ya mkutano wa Lusaka
na nikamfahamisha kuwa napeleka taarifa kwa ''travel agent,'' atayarishe tiketi yake
ili yeye atue Nairobi na hapo aunganishe ndege moja kwa moja hadi Lusaka badala
ya kuja Dar kwa hofu ya kuchelewa kikao.

Jibu lililokuja kwangu kutoka wa Dr. Dau ni kuwa yeye ofisi ameniachia nakaimu kwa
hiyo nitimize wajibu wangu.

Mimi nilisafiri na wakurugenzi hao niliokutajia hapo juu kwenda Lusaka kwenye
mkutano ule.

Iko picha tumepiga Pomodzi Hotel Lusaka niko bega kwa bega na wazee wangu
wakurugenzi.

Kwako lipi kubwa hili la Chande au hili la Lusaka?
Nina mengi.

Hayo ya kutoeleza utafishaji wa mabenki nisingeweza kuyaandika katika kitabu cha
Sykes kwani si mahali pake.
 

Kitabu hiki cha Chande nilikinunua Arusha Jumatano Juni 2008 kwenye Sulllivan Summit.

 
Kwa hakika Dr Dau ni sehemu muhimu ya maisha yako, sasa nimeelewa vizuri ni kwa nini ulitaka daraja la Kigamboni liitwe Dr Dau bridge lakini Magufuli akaamuwa liitwe JK Nyerere bridge.
 
Kwa hakika Dr Dau ni sehemu muhimu ya maisha yako, sasa nimeelewa vizuri ni kwa nini ulitaka daraja la Kigamboni liitwe Dr Dau bridge lakini Magufuli akaamuwa liitwe JK Nyerere bridge.
Matola sijataka daraja liitwe Daraja la Dau. Vipi ninaweza kuwa na fikra kama hiyo?
Nilichosema ni kuwa hapa Dar sisi wenyewe kwa wenyewe tunapolitaja daraja lile huwa tunaliita "Daraja la Dau," na hii ni katika maskhara.
 
Matola sijataka daraja liitwe Daraja la Dau. Vipi ninaweza kuwa na fikra kama hiyo?
Nilichosema ni kuwa hapa Dar sisi wenyewe kwa wenyewe tunapolitaja daraja lile huwa tunaliita "Daraja la Dau," na hii ni katika maskhara.
Mzee wangu hata mimi ni wa Dar japo ni kinda, nimezaliwa ocean road, na siye wenye uchungu na pesa zetu daraja lile tunaliita NSSF bridge.

All in all nimeshafahamu undugu wa damu baina yako na Dr Dau, hata ningalikuwa mimi mimi aliyeniinuwa ni lazima nimuheshimu, na nina uhakika hata wewe kama huna roho ya choyo basi kwa ukaribu ambao ulikuwa nao na Dr Dau pamoja na DG Janguo basi nina uhakika una hazina kubwa ya vijana hapo bandarini ambao uliwaingiza kazini.
 
Kweli mkuu, alionesha uzalendo wa hali ya juu. Ila kuna hili suala la kuwa Freemasson linanichanganya kidogo. Hadithi nyingi tunazisikia kuwa hii jamii ni ya kishirikina na kazi zao hutegemea kuuwa watu ili kutoa makafara hivyo si watu wazuri. Sasa huyu Chande alikuwa mzalendo kiasi hiki na hakumtoa kafara Mwalim baada ya kutaifisha mali zake. Hapo ndo pananichanganya. Ufafanuzi kwa anayeelewa hii jamii kwa usahihi tafadhali.
 
Mkuu....unanikumbusha kauli iliyojaa masikitiko, toka kwa raisi wa awamu ya 3...kwamba watanzania wameachana na utamaduni wa kujisomea....!
 
Kaka yangu, Kadhi Mkuu....uhakika na ukweli utaupata tu, kwa wewe mwenyewe kujisomea....google, ingia soma, pata tafsiri yako mwenyewe, ikitokea tafsiri yako ikawa sawa na unayoyasikia kwa "wajuvi wa mambo", vema, lkn ikiwa ni tofauti, simama ktk kile ulichokisoma....
 
Sasa tunaomba simulizi ya baba yangu Mzee Janguo nae atupashe juu ya mjadala huo baada ya wakurugenzi kutolewa nje.
NB. Namjua vizuri mzee Jangu ni MTU muungwana na muumini Mkubwa Wa uislamu tena swala tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…