Narudia tena, hakuna , hakuna! aliyewahi kuthibitisha pesa za Kawawa, Nyerere au Amir Jamal nje ya nchi.
Kumsikia Kambona akisema hakufanyi kuwa ukweli
Nani alitegemea Kambona ataongea jambo zuri kuhusu Nyerere kwa ugomvi wao?
Hadi anafariki, hakuna aliyewahi kuthibitisha madai akiwemo Kambona mwenyewe
Vijana wa leo wanasikia tu na kuamini, walioishi zama hizo wanajua ukweli
Kuna Anour Kassum,alikuwa waziri na moja ya wizara alizodumu ni Madini na Nishati. Leo kama angekuwa sawa na 'fisi' tulio nao, tusingekuta hata mchanga wa kujaza katroli. Nani alikuwa na ufahamu wakati huo?
Tuwape heshima waliotumikia Taifa tukalikuta lilipo, tuache hadithi za kuzusha tu
JokaKuu