Siku moja na Sir Andy Chande

Siku moja na Sir Andy Chande

offeB1LrOwzYffOkPLXMXFT6wk-lcgEJ0fOTFR_Avs1sc4M9Zf3kL48JLYExOYeTgyNhqE7hfll7od2HcGkmDBgF0hOKdTyl4WmmUGyktNkRKcrGagYfl7xcBNhwKGG9IbO9yZpPDAyehlAa9b2kJ8rPy79afm10bPoyIaTQzONe5_T0tAN1qL_YJHQ-hLJWgmTeCWeVTmuNImX8TQ-JUkNm-ikylHDq0DkmPxsjeXtOkETY5kwU89tRPQHR4f7Hkka3t4MvGrOk0KDYlNH6_xifRdt4WEb5UbD8frfxXyzxHBQ7tqDrk2tjoJv3A_DbonxvE17kzriow0ehQ4ALKTkkodpRzkSkgAPzqEsHGRLoMMQ2OfqfWeQSk81PBBUN8K9yBiH2VvPYnTzjP0uO01HTVpO0IH9tUmMeGKqyzD5MQQUqT1NJ6KPMeq7f9nGZgUIPw2FTfvonTAAot1H2LrowlSb2vor27-l4eJzwwtsaLsI-qtMxbnkkjQ7Yrn1TUb8X-Omp1qwYQlptSYW3JR5wCbenCKD_h8TobEpziGpwld_eDwBKhooV9rZmsabWdhzUwjqVA0gS8XG6Q8m81BLJPJtSRgOxW-8C_DKNxg6gnIqZpkH0fg=w318-h380-no

Ilikuwa katikati ya miaka ya 1990 nikiwa afisa mdogo Makao Makuu ya Tanzania Harbours Authority (THA) katika Idara ya Masoko iliyokuwa ikiongozwa na Dr. Ramadhani Kitwana Dau. Idara hii ilikuwa idara ndogo kwa maofisa ndani yake na ndiyo kwanza imeanzishwa.

Mimi nilipewa uhamisho kutoka Idara ya Biashara kwenda Idara ya Masoko kwa kile nilichoelezwa kusaidia kuanzisha idara mpya. Lakini ukweli ulikuwa mkurugenzi alikuwa anasafiri sana nje ya nchi na pakawa hapana mtu idarani angalau wa kuishikilia idara kwa muda. Lakini palikuwa na sababu nyingine. Ala kuli hali Dr. Dau alikuwa tukifahamiana. Kipindi hiki Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi alikuwa Andy Chande na Mkurugenzi wa Bandari wenyewe tukipenda kumuita DG yaani Director General, alikuwa Athmani Janguo.

Ikasadifu kuwa Bodi ya Wakurugenzi inakutana chini ya Mwenyekiti Andy Chande wakati Mkurugenzi wa Masoko Dr. Dau yuko nje ya nchi na ametoa ‘’notice,’’ kuwa nafasi yake atakaimu Mohamed Said. Yote yaliyotakiwa kutolewa taarifa kwa Bodi alikuwa kayatekeleza hivyo kazi yangu itakuwa kufanya, ‘’short presentation.’’

Bandarini walipita wenyeviti wengi wa bodi lakini ukurugenzi wa Andy Chande ulikuja na habari nyingine. Taarifa zilikuwa zikivuja na kutufikia maofisa wadogo ilikuwa mabosi wetu walikuwa wakihenyeshwa na Chande kiasi cha kulowesha vitambaa kwa kufuta jasho. Nikiri kwa kusema kuwa habari hizi wakati mwingine zikitufurahisha maofisa wadogo kwa kusikia kuwa wale waliokuwa wanatufanya sisi katika viti vyetu tuone kama moto umewashwa chini yake Mungu katulipia na sisi kwa wao kupata saizi yao wa ‘’kuwanyanyasa.’’

Tukisikia habari kuwa Chande alikuwa hachukui posho ya kikao. Tukipata habari kuwa mkurugenzi akichelewa kikao hamruhusu kuingia. Yaani yeye mwenyekiti akiingia Board Room na kukalia kiti chake cha enzi haingii tena mtu. Ilimuradi madereva wakikaa katika magari yao kusubiri mabosi wao habari zilikuwa Chande hivi Chande vile.

Bila shaka hawa madereva walikuwa wanazinasa habari hizi kwa kuwasikia mabosi wao wakizungumza wakati wakiwaendesha. Juu ya hayo yote kila mfanyakazi wa bandara alikuwa anajua kitu kimoja kuhusu Chande nacho ni kuwa alikuwa tajiri kufru.

Haya mambo ya Freemasons wakati ule yalikuwa bado siri kubwa ila mimi nikijua kuwa Chande alikuwa Freemason na nilijua kwa sababu mzee wangu mmoja na yeye alikuwemo kwenye ‘’club,’’ hiyo kama mwenyewe alivyopenda kuiita na hakuwa akimpenda sana Chande. Alikuwa akinambia, ‘’Natamani nimfanyie ugomvi Chande lakini siwezi kwa kuwa tuko ‘’club,’’ moja na sheria zetu zinatukataza kugombana wenyewe kwa wenyewe.’’

Huu ugomvi wao haukuwa wa leo ulianza miaka mingi nyuma toka enzi za kupigania uhuru wao wakiwa TANU na siasa zao za Afrika kwa Waafrika. Siasa ambazo Nyerere na TANU walizishinda. Ikawa sasa kila Chande akichaguliwa katika nafasi na Nyerere nikifika ofisini kwa mpashaji wangu habari itakuwa hiyo.

Ikawa sasa nimemfahamu Chande kutoka kwa mwanachama mwenzake wa hiyo ‘’club,’’ yao. Siku moja nikamuuliza mzee wangu, ‘’Hii ‘’club,’’ yenu ni ‘’club,’’ gani?’’ Akanitazama usoni huku kakunja uso akaniuliza, ‘’Wewe unaitakia nini?’’

Sikuuliza tena hilo swali lakini iko siku akanitajia.

Nikiwa nimeelemewa na habari za Chande nikawa sasa najitayarisha kuingia katika kikao cha Bodi ya Mamlaka ya Bandari Chande akiwa Mwenyekiti wake.

Bandari maofisa tukishonewa Kaunda Suti kama sare ya kazi. Haikuwa lazima uvae kila ukija kazini lakini kwa yale niliyosikia kuhusu Chande siku ile ya Bodi nilikuwa katika sare kwa kuzingatia kuwa kamba hukatikia pabovu.

Kichekesho kikubwa katika hili ni kuwa mimi nilikuwa ofisa mdogo mno na naamini hajapatapo ofisa wa ngazi yangu kukaimu nafasi kubwa ya ukurugenzi. Ilikuwa hakuna mantiki na ni jambo lisilowezekana. Lakini kwa kuwa nilikuwa idarani hapakuwa na jinsi ila nikaimu nafasi ya ukurugenzi na hivi ndivyo nikajikuta nimeingia katika bodi pamoja na wakurugenzi wa idara mbali mbali ambao kwangu ni mabosi wakubwa na hata umri wamenipita kwa mbali sana.
Nimetulia kwenye kiti na wakurugenzi wenyewe na mara Chande akaingia Board Rom kafatana na Mkurugenzi Mkuu Athmani Janguo.

Kikao kikaanza.

Ikawa Mwenyekiti Chande na Athmani Janguo wananong’ona sauti ziko chini lakini aliyekuwa anazungumza ni Chande.

Wakurugenzi wametulia tuli.

Baada ya mazungumzo yao kule mbele Mkurugenzi Mkuu akatuamuru sote tutoke tusibiri hapo nje. Naam. Si bure liko jambo niliiambia nafsi yangu. Wakurugenzi wote wakawa wamesimama nje wamewaacha Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wako ndani bila shaka wanaendelea mazungumzo muhimu.

Pale nje tukisubiri nawaangalia wazee wangu. Walikuwako waliovuta sigara na kupuliza moshi juu hewani na walikuwapo pia waliokuwa wanauma meno kwa ghadhabu.

Ilikuwa wazi wamefedheheshwa kwa kutolewa ndani ya Board Room na kusimamishwa nje kwenye, ‘’corridor.’’ Kwangu mimi hii ilikuwa mfano wa wanafunzi watukutu wakiotokewa darasani na mwalimu. Madirisha yalikuwa wazi yakiingiza upepo wa Bahari ya Hindi lakini wazee wangu naona walikuwa wanahisi joto maana wakijongea madirishani na kuchungulia nje kuiangalia Dar es Salaam Port.

Haukupita muda mrefu tukaitwa ndani. Kilichokosewa kikaelezwa kwa wakurugenzi na Mkurugenzi Mkuu akaahidi kuwa kitarekebishwa na kurejeshwa kwenye kikao siku ya pili.
Ilipofika zamu ya Idara ya Masoko kufanya ‘’presentation,’’ Mkurugenzi Mkuu Athmani Janguo akamwambia Mwenyekiti wa Bodi Andy Chande kuwa yeye ndiye atawasilisha.

Allah alikuwa kapokea dua zangu.

Vibweka vya Chande vilikuwa havijesha.

Kwa kawaida posho ya Wakurugenzi huwa inatolewa wakati kikao kinaendelea. Mgawaji anapita kwa wakurugenzi mmoja mmoja anagawa bahasha.

Chande pale mbele alipokuwa amekaa akaona bahasha zinatolewa akasema, ‘’Hapana kutoa fedha tunatoa fedha kwa watu wanaofanya kazi. Acha kugawa.’’

Sikuweza kuamini masikio yangu.

Ikanidhihirikia kuwa kumbe yote niliyokuwa nayasikia kuhusu Mwenyekiti Chande kumbe kweli.
Lakini baada ya kikao tuko ofisini tunaendelea na kazi mgawaji akatuletea bahasha zetu. Siku ya pili Bodi inaendelea lakini Mkurugenzi wa Masoko Dr. Dau akawa kesharudi safari.

Bismillah kuona sura yake tu baada ya salamu nikampa taarifa ya kikao cha bodi jana na yote mengine ya biashara mpya kwangu yalikuwa hayana umuhimu.

Dr. Dau akanambia,’’Hivi asubuhi hii wakurugenzi wote tumeitwa kwa DG kuna kikao kabla ya kikao cha bodi.’’

Baadae Dr. Dau alinambia kuwa Mkurugenzi Mkuu aliwaambia kuwa hajapata kuhisi vibaya kama alivyohisi jana.

Tulipokuwa wadogo nilikuwa nikimsikia mama yangu akisema kila anapomhadithia mtu aliyekuwa na mengi ya kueleza kuhusu yeye, ‘’Chini kunakwenda watu.’’

Siku yangu moja na Andy Chande ilitosha kumwelewa na kujua kwa nini juu ya yeye mali yake Kengele Tatu (sasa National Milling Corporation) kutaifishwa bila ya fidia hakutetereka, hakukimbia nchi wala hakugombana na Mwalimu Nyerere wala na serikali akabaki nchini na akaanza biashara nyingine na akatajirika pengine kupita pale mwanzo. Huku akifanya biashara zake alikuwa pia akitumikia bila kinyongo nafasi kadhaa alizokabidhiwa na nchi.

Hakika chini kunakwenda watu.
Asante kaka kwa simulizi,Andy Chande,Rajani,Kassum ,Amir Jamal ni wazalendo hasa kuliko hata sisi Wamatumbi tunaojifanya ndio wenye nchi na hawa pamoja na utajiri wao kutaifishwa wakabaki marafiki wa Mwalimu JK Nyerere,hawakukimbia wakabaki hapahapa ingawa wengine wamezikwa Canada lakini bado historia ya nchi hii haitawasahau-Pia uandishi wako ni murua unavutia kwa mtiririko ni kama Mohamed Ganzel yule mwandishi maarufu wa riwaya wa miaka ile.Asante mkuu kwa kutoa darasa kuhusu Sir Andy
 
Tunaomba utueleze kuhusu hiyo club
Hiyo club ipo miaka mingi makao yake yapo opp na Kilimanjaro Hotel na ni siku hizi tu ambapo watu wanaiona Freemason kama inahususiana na mambo ya kichawi na utajirisho ,na kuonekana kama club ya siri,nijuavyo mimi nilianza kuijua Freemason miaka mingi na huyu Sir Andy Chande alikuwa mara nyingi yeye na wenzake wakitoa hata misaada kwa vikundi mbalimbali kama vile ilivyo Msalaba Mwekundu,katika miaka ile hatukusikia hayo mabaya yanyosemwa kuhusu FM hivi sasa na hiki ni exclusive club utamkuta mume wa Malkia wa Uingereza,maraisi na ni miaka mingi huko nyuma,siku hizi eti hutangazwa na waganga kwa kubandika matangazo kuwa watawaingiza watu kwenye FM ,huo ni upotoshaji na dhana nzima juu ya Freemason,hapa Tanzania wapo wengi wanachama wa hiyo club ni matajiri kama ilivyo kwa club nyingine exclusive kama Msalaba Mwekundu,Red Crescent n.k
 
Mkuu huyu Amir Jamal naye mzalendo?,nikisikia alivyokuwa wizara ya fedha aliiba mifedha mingi na kwenda kujificha Canada?..
 
Sijaelewa hii story maudhui yake nini ?
Kwani unadhani Daud Bashite alipenda kupata division zero wakati same class kuna vipanga vimepiga division one point seven?

Wewe ni Bashite tu, sasa machapisho aliyoandika Mzee Mohamed Said kwa kingereza si ndio utatoka kapa kabisa?

Kwanza kama wewe ni mtu wa mashambani, humjui Mzee Janguo wala humjui Dr Ramadhani Dau kwa hakika thread hii kaa pembeni hutoelewa kitu.
 
Jenguo huyu alikuwa mbunge wa Kisarawe kwa miaka makumi kadhaa??
Sasa nimeelewa "urafiki' wa Mzee Said na Dau ulisarujiwa wapi haswaa
Leo ndio siri imefichuka, ni wazi Dr Dau amewabeba sana ndugu zake katika imaani hasa huyu Mzee Mohammed Said, karani ambaye alikuwa na access ya kuingia hadi board meeting.
 
Si utani wale watoto walianza kula bata long time, ninakumbuka miaka ile ya awamu ya kwanza holiday walikuwa wanakwenda London.
Kwa kifupi those days bandari ilikuwa ni mali ya Mzee Janguo na kabla wapemba hawajatuharibia kujilipuwa tulikuwa tukienda UK kama unavyokwenda South Africa tu kwa sasa bila kuomba viza ubalozini, sasa kama manoti unayo ni kwa nini weekend usilikwee BA to Heathrow London? Mambo yamebadirika sana.
 
Mkuu huyu Amir Jamal naye mzalendo?,nikisikia alivyokuwa wizara ya fedha aliiba mifedha mingi na kwenda kujificha Canada?..

..Amir Jamal aliteuliwa kuwa Balozi wa Tz Geneva (mashirika ya UN) kati ya 1988 mpaka 1993.

..akiwa huko aliugua na kuamua kwenda Canada kujiuguza chini ya uangalizi wa wanawe.

..mauti yalimkuta akiwa Canada na akazikwa hukohuko.

..nilitaka kuweka taarifa kwa Amir Jamal hakutoroka nchini.

..Serikali ilimfanyia kumbukumbu baada ya kifo chake na kama sijakosea Benjamin Mkapa wakati huo akiwa Waziri alimuwakilisha Waziri Mkuu Cleopa Msuya ktk tukio hilo.
 
Hiyo club ipo miaka mingi makao yake yapo opp na Kilimanjaro Hotel na ni siku hizi tu ambapo watu wanaiona Freemason kama inahususiana na mambo ya kichawi na utajirisho ,na kuonekana kama club ya siri,nijuavyo mimi nilianza kuijua Freemason miaka mingi na huyu Sir Andy Chande alikuwa mara nyingi yeye na wenzake wakitoa hata misaada kwa vikundi mbalimbali kama vile ilivyo Msalaba Mwekundu,katika miaka ile hatukusikia hayo mabaya yanyosemwa kuhusu FM hivi sasa na hiki ni exclusive club utamkuta mume wa Malkia wa Uingereza,maraisi na ni miaka mingi huko nyuma,siku hizi eti hutangazwa na waganga kwa kubandika matangazo kuwa watawaingiza watu kwenye FM ,huo ni upotoshaji na dhana nzima juu ya Freemason,hapa Tanzania wapo wengi wanachama wa hiyo club ni matajiri kama ilivyo kwa club nyingine exclusive kama Msalaba Mwekundu,Red Crescent n.k
Ile pale nyuma ya Kilimanjaro hotel ni Temple tu kamwe wenyewe huwezi kuwaona hata siku moja wakiingia jengo lile.

Kuna watu kichwani wamejaa fungus, Freemason ndio wenye Rotary club na Lions club.

Kwa mtu ambaye yupo hapa mjini kitambo anajuwa vyema charity zilizofanywa na club hizi.

Tatizo kubwa la Watanzania ni poor IQ na slow learners.
 
Mkuu huyu Amir Jamal naye mzalendo?,nikisikia alivyokuwa wizara ya fedha aliiba mifedha mingi na kwenda kujificha Canada?..
Amir Jamal ni mmoja wa Wazalendo wa nchi yetu.

Ametumikia nafasi mbali mbali na aliaminiwa sana na Mwalimu

Baada ya kustaafu alihamia Canada ambako umri wake uliishia hapo

Mwalimu Nyerere na Benjamin Mkapa walikutana chuo cha IFM katika kuomboleza na ndiyo siku Mwalimu alianza kumshawishi Ben kuhusu Urais

Kuhamia Canada si kwasababu ya kuiba kama watu wanavyozusha. Si kweli hata kidogo

Pumzika kwa Amani Amir Jamal, Mzalendo na Mwananchi

JokaKuu
 
Asante kaka kwa simulizi,Andy Chande,Rajani,Kassum ,Amir Jamal ni wazalendo hasa kuliko hata sisi Wamatumbi tunaojifanya ndio wenye nchi na hawa pamoja na utajiri wao kutaifishwa wakabaki marafiki wa Mwalimu JK Nyerere,hawakukimbia wakabaki hapahapa ingawa wengine wamezikwa Canada lakini bado historia ya nchi hii haitawasahau-Pia uandishi wako ni murua unavutia kwa mtiririko ni kama Mohamed Ganzel yule mwandishi maarufu wa riwaya wa miaka ile.Asante mkuu kwa kutoa darasa kuhusu Sir Andy
Mfianchi,
Ahsante kaka.
 
Back
Top Bottom