Ninapomuona mtu anamponda Jiwe ninabaki namshangaa na kumuona hana akili kabisa.
Mosi,Huo uhuru wa habari ndio ulikuwa kipaumbele kwa watanzania? Upuuzi mtupu! Watu wanakufa huko vijijini kwa kukosa huduma bora za afya na umasikini alafu kuna mtanzania mmoja mpuuzi analeta fyokofyoko zake.
Pili,Hakuna kikosi kazi kilichoundwa na Magufuli zaidi ya uchafuzi na propaganda za kisiasa, Na hata kama kingekuwepo watanzania waliona ni sawa kwa kuwa baadhi ya watu walijiona ni muhimu kuliko maisha ya watanzania wengine hususan wale masikini waliopo vijijini kwa kuendekeza siasa zisizo na tija!
Tatu, Tanzania ni nchi masikini.Nyerere alisema maadui wa taifa ni ujinga,umasikini na maradhi ninyi wanasiasa mnaendekeza upuuzi mwingine kutuondoa watanzania katika focus! Nenda vijijini watanzania wanafurahia huduma bora za afya,elimu bure maji kila kona! Kama alikuwa muuaji basi alikuwa muuaji mzuri!
Nne, Chato ipo nje ya Tanzania?
Mwisho Mwendazake alikuwa mwiba kwa wanasiasa uchwara walioendekeza siasa za midomoni na kutafuta ulaji kwa jina la siasa.Ni heri hata kama aliwapiga risasi baadhi yao ili kuokoa maelfu ya wanawake waliokuwa wanafia njiani kuelekea hospitali kujifungua kutokana na ubovu wa miundombinu! Ujenzi wa SGR,Flyovers,barabara,madaraja,ndege...n.k zote ni kwa ajili ya watanzania!
Ahsante Baba!