SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,193
- 8,009
Kuna mambo Watanzania inabidi tupevuke kwenye masuala haya ya mpira. Kumekuwa na hii kasumba ya kuwachukulia wachezaji kama mayai hivi. Yaani tunataka wacheze mechi moja kwa wiki, kabla ya mechi yoyote ya kimataifa hamtaki wagusweguswe hata kwa wiki mbili mkiogopa eti watachoka au kuumia. Madhara yake tumekuwa na ligi yenye ratiba za hovyo na zisizoeleweka.
Kwa siku kadhaa kumekuwa na vilio kutokana na wachezaji wa Simba na Yanga kuitwa timu ya taifa wakati timu zinajiandaa kucheza mechi za robo fainali ya CAFCL (na nadhani Yanga ndiyo wanalialia zaidi halafu wakati huo huo wanalalamika kwa nini Dickson Job hajaitwa).
Ukiangalia ratiba ya Bafana Bafana, kuanzia wiki ijayo watakuwa Algeria kucheza mechi 2 za kirafiki na katika kikosi kilichoitwa kuna wachezaji 7 wa Mamelodi Sundowns walioitwa na hawa ni wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Mamelodi na siyo kina Kennedy, Manula, Mwamnyeto au Mzize ambao hawana uhakika kwenye vikosi vya kwanza vya timu zao.
Afrika Kusini anacheza mechi ya pili ya kirafiki na Algeria tarehe 27/03 huko Algeria, yaani siku 3 kabla ya kukabiliana na Yanga. Hii pia ina maana hawa wachezaji hawatakuwa na wenzao katika kipindi chote cha kujiandaa kucheza na Yanga na kuna uwezekano mkubwa watakuja moja kwa moja Dar kujiunga na wenzao. Kwa ratiba hiyo ina maana wanaweza kupata siku moja tu ya kufanya mazoezi na wenzao.
Kuna kitu cha kujifunza hapa.