peche luke
JF-Expert Member
- Sep 8, 2013
- 365
- 106
Tatizo sio zanzibar, tatizo ni muungano huu tulio nao ambao upo mparaganyiko haujulikani kichwa wala mguu, kwa mfano zile sector ambazo haziko katika orodha za muungano, zinashindwa kujiendesha kimataifa kutokana na muungano wenyewe, mfano suala la michezo, sio suala la muungano, Watanganyika wakachukua timu ya Tanganyika na kuitambulisha kama tanzania, ZFA imeshindw akupata usajili FIFA kutokana TFF tayari inawalihsa tanzania, Yaani Jamuhuri ya muungano wa tanzania, pale kunapotea misaada katika suala la micheza kutoka kimataifa zanzibar haipati chochote kutoka TFF.
Kuhusu jina sijui tutafute 'jiki' maana itachukua muda sana kutakat, limechafuka sana. Tani 30 za bilioni 125 zitamshtua kila mtu na hapo JMT itaingia tu.Mkuu Nguruvi3
Kuna watu ndani ya SMZ wanajua undani wa tatizo hili na sishangazwi kuona waziri mhusika kutoka SMZ anakuja na majibu mepesi kama aliyoyatoa; tatizo hapa sio faini tatizo ni kuharibiwa kwa jina la Tanzania kwenye medani za kimataifa; $500, 000 sio kitu kabisa; huu muungano hauna faida hawa watu hawana shukrani kama unakumbuka walipopata hisia kuwa Zanzaibar kuna mafuta waziri mhusika siku ya pili yake aliweka wazi mafuta sio suala la muungano; hivi sasa wamenyamaza kimya kwasababu hawana uhakika na mafuta yenyewe ila wana uhakika kuna gesi Mtwara na mikoa ya kusini wanasubiri wale pesa ya gesi kama walivyokula ya almasi ya mwadui; pamba ya Shinyanga; Katani ya Tanga hawa sio wenzetu choyo kimewatala!
Tunawatakia heri sana katika maendeleo. Kama wangetumia bendera ya znz kungalikuwa na tatizo gani? Kama wangelipa ada zao IMO kungalikuwa na tatizo gani? Leo SMZ si ingesafirisha tani za bangi bila hofu na kwa mamlaka kamili!!Wewe unataka nini hela ni ya waznz na wataendelea kutumia jina la tz mpaka mtakapo waachia nchi yao munaogopa mendeleo ya znz kwanini na tanganyika yenu wezi watupu
Basi waachieni tu
Mkuu Nguruvi3
Kuna watu ndani ya SMZ wanajua undani wa tatizo hili na sishangazwi kuona waziri mhusika kutoka SMZ anakuja na majibu mepesi kama aliyoyatoa; tatizo hapa sio faini tatizo ni kuharibiwa kwa jina la Tanzania kwenye medani za kimataifa; $500, 000 sio kitu kabisa; huu muungano hauna faida hawa watu hawana shukrani kama unakumbuka walipopata hisia kuwa Zanzaibar kuna mafuta waziri mhusika siku ya pili yake aliweka wazi mafuta sio suala la muungano; hivi sasa wamenyamaza kimya kwasababu hawana uhakika na mafuta yenyewe ila wana uhakika kuna gesi Mtwara na mikoa ya kusini wanasubiri wale pesa ya gesi kama walivyokula ya almasi ya mwadui; pamba ya Shinyanga; Katani ya Tanga hawa sio wenzetu choyo kimewatala!
Well said mkuu. Nianze na ulipomalizia, wengi hapa jamvini tumeshatoa ushauri wa namna Zanzibar wanavyoweza kuwa na mamlaka kamili. Wazanzibar wamekataa na kufuata njia zile zile wanazolaumu.Kauli ya Waziri wa Mawasiliano na Miundo mbinu wa SMZ, Rashid Seif Suleiman ya kuvilaumu vyombo vya habari vya Tanzania BARA ilinishangaza sana.
Ni kweli kabisa kuna kitu viongozi wetu waasisi wa 'muungano' walikiona kama kilikuwa ni cha muhimu sana kuziunganisha nchi zetu, lakini vile vile makosa ya kutokuelimishwa na kutoshirikishwa kwa wananchi wengi katika kufikia uamuzi huo ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuwa chanzo cha mitikisiko na utegemezi katika 'muungano'.
Imedhihirika kuwa viongozi wakuu waliokuja baada ya marehemu Sheikh Abeid Amani Karume na pia Wazanzibari wengi hawakutaka kuendelea kuwepo muungano na kwa sababu hiyo ilibidi viongozi wetu wawabembeleze kihoja na ilipobidi pia yalitumika mabavu ili waendelee kuwepo mwenye 'muungano' . Hii ilipelekea wananchi wengi wa Zanzibar na pia wachache wa bara kuamini kama viongozi wakuu wa bara walikuwa na ajenda fulani za siri ambazo kuzitimiza ilibidi tuwaombe na kuwashinikiza Wazinzibari waendelee kuwepo kwenye 'Muungano'.
Fikra na mitazamo hii imekuja kujisimika zaidi pale badhi ya viongozi wakuu wa Zanzibar walipotiwa misukosuko pale walipohoji uwepo wa muungano na manufaa yake.
Kwa sasa wanafanya kila wanachotaka bila kujari mshikamano, sheria na taratibu za nchi wakidhani kuwa Tanganyika inawahitaji sana zaidi ya wao kuihitaji Tanganyika.
Hata kujitoa kwao katika sheria za Jamhuri ya muungano zinazohusu usafiri wa majini za mwaka 2003 na kuunda sheria zao za bahari na usafiri na kuwa chini ya Zanzibar Maritime authority((ZMA) mwaka 2006 ilikuwa ni katika mwendelezo wa fikra hizo.
Waswahili wanasema, mdharau mwiba mguu huota tende!.
Tumezidharau na wakati mwingine kuzipuuzua chokochoko za 'muungano' kwa muda mrefu huku tukiwadekeza Wazinzibari kwa kuwapa kila kile wanalichokuwa wanakitaka na matokeo yake kwa sasa tunayaona. Kwa sasa imekuwa chao ni chao lakini chetu pia ni chao na wakati mwingine wanataka wakichukue chote.
Tulianza muungano vibaya na inavyoonekana pia tutaachana nao vibaya, na kwa maana hii, dawa ya muungano kwa sasa siyo serikali tatu kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali ni kuachana kabisa na muungano ili pande zote zipate ukweli halisia kama kuna umuhimu katika muungano. Hatutakuwa wa kwanza wala wa mwisho katika kuvunja muungano kwa sababu kuna nchi zimevunja muungano na zikapiga hatua zaidi za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hata katika ndoa, watu wanapokinzana sana, huwa wanafikia maamuzi ya kuachana ili kujipima na kuona umuhimu wa wao wakiwa pamoja au wakiwa single (space) na wakipatwa na reality, wengi wao hurudiana tena.
Mkuu Nguruvi3, unakuwa kama hujui kupenda!, Mke ukimpenda, unamhudumia kama jukumu lako ikiwemo kumlisha, kumvisha, kumtunza na kumpendezesha, na sio hayo tuu, kwa sababu una mpenda, unampa kila anachokita, hata kama wewe hukipendi!, mfano anapenda ubuyu, utamletea hata kama wewe huupendi!.Kuhusu jina sijui tutafute 'jiki' maana itachukua muda sana kutakat, limechafuka sana. Tani 30 za bilioni 125 zitamshtua kila mtu na hapo JMT itaingia tu.
Umeendeleza mjadala zaidi maana suala la ZMA liliondolewa wakijua wazi kuwa ada hawalipi wao.
Ni mbinu hizo ndizo ziliwashawishi waondoe mafuta, leo hatusikii mafuta tena bali wanasubiri gesi ya bomba kama umeme.
Baraza la mitihani wameondoa katika mambo ya JMT, lakini wanataka nafasi za upendeleo (zitengwe) kwa watoto wao.
Sijui kuna uwiano gani kiasi cha kuamini kuwa NECTA na baraza lao wantahini sawa sawa? Kuna uwezekano wakatoa A ambazo ni sawa na D lakini kwavile wana nafasi maalum who cares.
Nadhani upo umuhimu wa kuandaa mitihani ili kujiridhisha kama wana viwango na utaratibu wa nafasi maalum sasa basi. Wana Chuo kikuu, kingine wamejengewa na JMT kupitia chuo cha kivukoni na baraza lao la mitihani. Hakuna sababu ya kugombania nafasi na Watanganyika, ikibidi na watahaniwe.
nzitunga ,katika kamati zote za znz zinazoshughulikia muungano kama ya maridhiano na BAKAZA, UAMSHO n.k. hakuna kamati hata moja iliyowahi kuweka mezani hesabu za kuendesha serikali iwe moja, mbi, tatu au mkataba.Na wanzibar wanaona jambo moja tu!!!! Misaada, wanaamini baada ya muungano watapata misaada kwa jina la ZNZ. Mengine yote hawayaoni.
Kwa hiyo ndugu, mimi naona tunachelewa tu, Tunataka Tanganyika yetu. Ili muweze kupata misaada yenu ya FIFA, na misaada mingine mingi tu itakayowasaidia kuishi kwa raha mustarehe. Sisi tunataka Tanganyika yetu ili tufanye kazi kwa bidii na tule jasho letu wenyewe.
Kama mimi ningekuwa mkulu, you would get your beautiful Tanganyika now! Right now!
Tumewaachia wakaanzisha ZMA, wakawa na bendera yao. Sasa kwanini wanasajili meli kwa jina la JMT na bendera yake ikiwa walikataa mwaka 2003 na kuanzisha mamlaka yao mwaka 2006? Hatuna shida na mambo yao lakini bangi zinapokamatwa kwa jina la Tanzania ni tatizo letu sio lao. Umeona hapo? Meli zikivusha mizigo ya Iran tunawekewa vikwazo sisi si zanzibar.
Gharama za uasajili wa meli ni zetu, mapato ni yao, umeona?
Hili ni tatizo letu tutake tusitake, lakini je ni sisi tumelisababisha?
Hoja yako ipo wapi kuhusiana na bandiko? Je, umeelewa maana halisi au kusudio la bandiko?Wadanganyika punguzeni umbulula,kwanza rejesheni tanganyika yenu ndipo mropokwe.
asari wenyewe mnachingia mmoja,bado mnapiiiga keleleacha upumbavu hivi pale mnapoipeleka jmt yako katika vita unafikiri wazanzibari tunakubalianb na hayo take the consequencies