Sikia maajabu haya ya Mwalimu wa shule ya Kata

mkuu, tatizo sio kukosea SMALL GRAMMATICAL ERROR bali ninachoangalia ni aina ya kosa na limefanywa na mtu mwenye kiwango gani cha elimu. tusifichane...mwongeaje huyu inaonekana kiingereza chake ni kidogo sana ukilinganisha na levo ya elimu aliyofikia. kosa hili lingefanywa na mwalimu wa shule ya msingi isingekuwa taabu ila linapofanywa na mhitimu wa chuo kikuu, inaashiria kwamba kuna tatizo.

acha kufikiri irrationally kila wakati. Kama kweli unaijua hiyo lugha, uliijifunzaje? Siyo through mistakes? Kama ndivyo huyo mwalimu si bado yupo on process za kuimarisha lugha hiyo?.
Halafu ukome kuwadhalilisha au kuwasema waalimu wa msingi kwani ulicho nacho sasa ni jitihada zao. Ulianza shule ukiwa plain kwa brain yako na sasa tabularaza wewe unajitia kuwakosoa walimu wako wa awali na kuwaenzi hao wa chuo. Waombe radhi walimu.
 
TANO: wewe unaona alichokitamka msomi huyu wa chuo kikuu mwenye digrii ya daraja la kwanza ni sahihi? sio hatari kwa msomi kama huyu kuwafundisha wanafunzi wake kingereza kibovu?

SITA: tusiangalie tulipoangukia bali tuzingatie pale tulipojikwalia. mfumo wa elimu yetu ulivurugwa tangu utawala wa Nyerere na waliomfuatia wamezidi kuididimiza zaidi elimu yetu. hapa ndipo tunapaswa kuanzia kutatulia ubovu wa elimu hii mbovu tunayoirithisha kwa vizazi vyetu.

cc: FaizaFoxy

we jamaa mshamba sna kwani huyo mwalimu alikua anafundisha kiingereza? una jua maana ya content language? acha ul.ofa!!
 
Last edited by a moderator:
mwenyewe umesema shule ya kata,hata hivyo kajitahidi.wanafunzi wengi wa shule hizi hata kiswahili ni shida makwao.unamtoa mwalimu kigoma akafundishe wamasai wapi na wapi?
 
We can not speak as native speakers.Mi sioni ajabu huyo mwalimu cha msingi wanafunzi wameelewa na kama hawajaelewa msisitizo utawekwa kwa kiswahili.Mwalimu mwenyewe katoka kwenye mfumo huo huo wa kiswahili as a medium of instruction kwa miaka saba ulitegemea nini hapo.
 
Leo nimetembelea shule moja ya Kata nikashuhudia kituko cha mwaka kutoka kwa mwalimu mmoja shuleni hapo.

Mwalimu huyo amehitimu Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) hivi karibuni na akaajiriwa moja kwa moja kufundisha katika shule hiyo ya Kata. Wakati akiendelea kufundisha nilimsikia akiwauliza wanafunzi swali hili: WHERE DOES IT LOCATED? Inaonekana ni mwalimu wa somo la Jiographia, hivyo alikuwa akiwauliza wanafunzi wake wamtajie location ya kitu fulani kwenye ramani.

Jamani, hapa ndipo shule za kata zilipotufikisha. Ikiwa mhitimu wa Chuo Kikuu anaongea kiingereza kibovu kama hiki, tena mbele ya wanafunzi,mnategemea wanafunzi anaowafundisha watapata maarifa gani kutoka kwake? Chukulia huyu ni mwalimu wa Kidato Cha Kwanza, wanafunzi wake wanaoambiwa kila siku "SPEAK ENGLISH" wataiga kiingereza gani kutoka kwake? Si ndio atawapoteza kabisa?

Ikiwa walimu hawajui kiingereza unategemea nini kutoka kwa wanafunzi wao? Haya ndio madhara ya serikali yetu kuchanganya elimu na siasa. Tumekwisha hasa!!

:israel:

Hapo kwenye red, nawe umekosea kama mwalimu unayemsema!
 
We can not speak as native speakers.Mi sioni ajabu huyo mwalimu cha msingi wanafunzi wameelewa na kama hawajaelewa msisitizo utawekwa kwa kiswahili.Mwalimu mwenyewe katoka kwenye mfumo huo huo wa kiswahili as a medium of instruction kwa miaka saba ulitegemea nini hapo.

Hapana sikubaliani na wewe! Kuna basic english ambayo ukiikosea tu, unatia mashaka makubwa! Huwezi kusema kwa mfano: I did went ........ tukakusamehe!
 
Sasa wewe umejuaje kama alikua anafundisha Geography?. Je, hukujiuliza kwamba huenda alikua anafundisha English na hapo alikua anawasomea wanafunzi sentensi zenye makosa ili wayabaini hayo makosa kwenye hizo sentensi.
 
Mbona maana imeeleweka kwamba "ulienda".Bora iyo broken kuna wale hawawezi kuunganisha sentensi kabisa na shule wameenda.
 
acha kufikiri irrationally kila wakati. Kama kweli unaijua hiyo lugha, uliijifunzaje? Siyo through mistakes? Kama ndivyo huyo mwalimu si bado yupo on process za kuimarisha lugha hiyo?.
Halafu ukome kuwadhalilisha au kuwasema waalimu wa msingi kwani ulicho nacho sasa ni jitihada zao. Ulianza shule ukiwa plain kwa brain yako na sasa tabularaza wewe unajitia kuwakosoa walimu wako wa awali na kuwaenzi hao wa chuo. Waombe radhi walimu.

kwa hiyo unataka watoto wetu waendelee kulishwa matango pori mpaka lini?
 
we jamaa mshamba sna kwani huyo mwalimu alikua anafundisha kiingereza? una jua maana ya content language? acha ul.ofa!!

alikuwa anafundisha kwa lugha ya KIINGEREZA, kwa hiyo alitakiwa kuongea KIINGEREZA SANIFU ili asiwapotoshe wanafunzi wake
 
Labda kosa la mtoa mada ni kuita maajabu. Lakini jamani haliondoi ukweli wa kujitahidi na kujifunza lugha hii maana ni muhimu katika nyanda mbalimbali. Watanzania ni watu intelligent saana. Wakati mwingine tunakosa fursa kubwa zaidi za kikazi kwa sababu tu ya lugha. Mi nadhani endapo huko nyuma tulikosa fursa ya kujua kiingereza kwa ufasaha ni vema kutafuta fursa mbalimbali ili kujiendeleza. Nakumbuka wakati ilivyosemwa ajira zinafunguliwa kwa EAC countries tulianza kuhaha kuwa wanakuja chukua kazi zetu. Endapo tulikosea nyuma basi turekebishe ili elimu inayotolewa kuanzia shule za msingi iwe sahihi ili kuepuka bomu la hapo baadae na kuweza kupata fursa za kazi mbalimbali pia.
 
mwenyewe umesema shule ya kata,hata hivyo kajitahidi.wanafunzi wengi wa shule hizi hata kiswahili ni shida makwao.unamtoa mwalimu kigoma akafundishe wamasai wapi na wapi?

pamoja sana mkuu. afadhali umekuja unisaidie maana watu wananilaumu kwa kusema ukweli. sijui wanataka watoto wetu waendelee kulishwa sumu mpaka lini.
 
Hapana sikubaliani na wewe! Kuna basic english ambayo ukiikosea tu, unatia mashaka makubwa! Huwezi kusema kwa mfano: I did went ........ tukakusamehe!

umesema vizuri sana mkuu CHUAKACHARA. mhitimu wa chuo kikuu akikosea kiingereza rahisi kihivyo hatuwezi kumuacha kwa kuwa atazidi kuwafundisha watoto wetu broken english na hatimaye kuwaharibu kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Sasa wewe umejuaje kama alikua anafundisha Geography?. Je, hukujiuliza kwamba huenda alikua anafundisha English na hapo alikua anawasomea wanafunzi sentensi zenye makosa ili wayabaini hayo makosa kwenye hizo sentensi.

alikuwa anafundisha jiografia na alikuwa amechora ramani kwenye ubao.
 
Sidhani kama ni sahihi sana kuona kuwa ni sawa tu kwa mwalimu kufanya kosa hilo-kama watu wengi hapa jukwaani wanavyotaka kutuaminisha. Nimesoma mawazo ya mmoja wa wachangiaji, na niseme tu kuwa inasikitisha kuona mtu anajaribu kuhalalisha kosa eti kisa mwalimu aliyekosea ni wa somo tofauti na analokosolewa kwalo. Jamani, tuache kujipa moyo; kama ufahamu wetu katika jambo fulani ni mdogo, basi tufanye jitihada ili tuongeze ufahamu, lakini si vizuri kutetea kosa.
 
We can not speak as native speakers.Mi sioni ajabu huyo mwalimu cha msingi wanafunzi wameelewa na kama hawajaelewa msisitizo utawekwa kwa kiswahili.Mwalimu mwenyewe katoka kwenye mfumo huo huo wa kiswahili as a medium of instruction kwa miaka saba ulitegemea nini hapo.

Ni kweli kabisa, hatuwezi kuzungumza kama wenye lugha yao, lakini kwa kiwango cha kupotea katika kutengeneza swali alilokusudia kuuliza mwalimu husika, ambalo ukweli ni kuwa ni miongoni mwa maswali rahisi kuyatengeneza, napata mashaka kama kweli ni kuteleza kwa ulimi tu ndiko kumemfanya akosee. Ni kweli mfumo wetu wa elimu ni sababu ya sisi kuwa hivi, na wala si shida kivile mtu kutoimudu vyema lugha ngeni, lakini kwa kuwa ni lugha rasmi ya kazi basi sote tunapaswa kujifunza; maana hakuna ugumu wowote katika taaluma kama tukiwajibika ipasavyo.
 
tpaul,kama sitakosea utakua mpya kwenye tasnia hii.'ORAL LANGUAGE'INAMAKOSA KULIKO WRITEN.WAENDELEZWE KIMASOMO WALIMU.
 
Back
Top Bottom