Sijui nianzie wapi?

Sijui nianzie wapi?

Ushauri wangu
1. Cheki DNA unaweza kuwa unaumiza kichwa kulea watoto wa wanaume wenzio..kama kipimo kitaonyesha watoto sio wako..mpe mama yao awapeleke kwa baba zao.

2. Usimrudie...embu fikiria mtu anayetembea na wanaume ovyo..hizo ni bidii za kutafuta ngoma..sasa huo utu wake unatoka wapi..achana nae.

3. Maumivu ya moyo yapo na ni kwa sababu mlikuw wapenzi ..yataisha..

4. Kama DNA itaonyesha hao ni watoto wako weka utaratibu mzuri ,wa malezi..kama wana jf walivyoshauri.lakini yeye asihusike..atawapa maneno mabaya watoto..na hiyo itawaathir sana.

5. Hili ndio lingetangulia point zote hapo juu..muombe sana Mungu akuongoze
 
Mbaya zaidi kiongozi, wakati wa purukushani hii, huyu wife alishawahi kuwakimbia hawa watoto sio chini ya mara tatu. alidiriki kuondoka nyumbani zaidi ya siku sita, hiki hasa ndo kilichonifanya nisiwaze hata mara moja kumwambia aondoke kwangu. haikua rahisi na ni mengi sana nimeyaona sijayaweka hapa. najuta kumfahamu huyu mwanamke

ebu toa historia ya jinsi ulivyompata huyo mkeo.. kwa kifupi
 
Unaweza msamehe ila ukaamua kutoshare tendo, mkawa mnalea watoto wenu kila mtu chumba chake ila matumizi ya nyumbani hakikisha unatoa. watu waelewa wanaishi ivo ili kuwatunza watoto, japo yataka moyo

mmh ushauri mgumu mno
 
hapo ndipo mnaponikatisha tamaa na mimi kuoa aisee, maana na haya ya rafiki zangu ninayoyaona majanga, wacha niendelee kuwa hivihivi zikitokea nadinya au bora nichukue mwanamke take away, ukimcoka unatuma kama chupa tu, kisha mwenzako anakuja kuiokota.
 
Mkuu Kahema tuliza wahka ...its not the end of life !! You are still young at 35 yrs Life ndo taamu sana na wengi wanakutamaani !! tafuta kwa makini utapata na umpromise Love yako penzi jema akikaa na wanao vizuri!! utafanikiwa tu.... Halafu usifikirie ya nyuma ongoza mbele maisha yana songa mbele... "aliyemwaga mboga mwenyewe asikupotezee moods zako!! Hakuna kusamehesamehe..kwani hakuheshimu watoto wala hata ndoa yake!!

you made my night better
 
Wanajamvi,
natumaini muwazima wa Afya,
Nimeona nije kwenu walau mujue yanayonisibu, sio kitu kipya hapana, ila
kimeniweka kwenye mazingira magumu sana, japo najitahidi kufanya kila
linalowezekana walau upepo huu upite.

kifupi ni hivi Mama wa Watoto wangu (Mke) nimeamua kumrudisha kwao baada
ya kugundua hakua mwaminifu kwangu ie niligundua anamahusiano ya
Kimapenzi na Watu wengine Nje ya Ndoa, nilifanya uchunguzi wa kina
nakugundua uchafu huo, baada ya mikimiki ya hapa na pale alikiri mbele
ya wazazi wake kua yote niliyowaeleza ni ukweli mtupu. baada ya
mashauriano ya muda mrefu nilifikia uamuzi wa yeye aondoke kwangu. hili
halikua gumu sana kuamua kwa kila kitu kilikua wazi

So issue yangu kubwa ni nini nifanye baada ya hapa, ukizingatia
yafuatayo:

1. tuna watoto watatu , mdogo kabisa ana miezi 9

2. hawa watoto nawapenda sana na mpaka sasa naishi nao

3.mimi mwenyewe umri umekimbia am 35 yrs now

4. mama watoto kila siku anapiga simu kuomba msamaha( japo najua kabisa
jasiri haachi asili)

5. najiuliza hata kama nikitaka kuoa tena, will it be fair to my
children?

6. nina watoto 3, will it suit me kuoa mwanamke ambaye hajazaa? ataweza
kulea kwa upendo hawa watoto?

7.je nikioa mwanamke mwenye mtoto/watoto tayari si atataka naye awalete
waishi kwangu? huu mzigo utaniua

8.je ni haki niwapeleke boarding hawa watoto ili mi niishi peke yangu?
kiukweli nipo njia panda, tafadharini yeyote anayeweza nisaidia
kimawazo nitashukuru
asanteni!

maya amempenda sir chief akiwa na watoto watatu na ijumaa wanafunga ndoa. na maya atajifungua mapacho soooo jiongeze. ila pole inauma
 
Ushauri wangu
1. Cheki DNA unaweza kuwa unaumiza kichwa kulea watoto wa wanaume wenzio..kama kipimo kitaonyesha watoto sio wako..mpe mama yao awapeleke kwa baba zao.

2. Usimrudie...embu fikiria mtu anayetembea na wanaume ovyo..hizo ni bidii za kutafuta ngoma..sasa huo utu wake unatoka wapi..achana nae.

3. Maumivu ya moyo yapo na ni kwa sababu mlikuw wapenzi ..yataisha..

4. Kama DNA itaonyesha hao ni watoto wako weka utaratibu mzuri ,wa malezi..kama wana jf walivyoshauri.lakini yeye asihusike..atawapa maneno mabaya watoto..na hiyo itawaathir sana.

5. Hili ndio lingetangulia point zote hapo juu..muombe sana Mungu akuongoze

hili la DNA mnataka jamaa afe haraka aisee
 
hapana , nipo naye mimi. kwa hari ilivyokua haikua rahisi hata kumuacha huyo mtoto kwa mama yake kwani kulikua na kila dalili ya murder.

huyo mama sio mlezi wa watoto
hivi unaeza kumuacha mtoto wa miezo tisa kwa mme?
huyo km una vimali kidogo mrudie akuue hapo hamna mke niamini mimi
mtoto wa miezi tisa,una mume then unagongwa nje???we sio mzima weee
mnisamehe wadau nachukia sana mwanandoa kuzini na dhambi yake inahtaji kipaji kusamehe
 
mmh ushauri mgumu mno

hakuna ugumu hapo, ni maamuzi tu. kuliko kuachana wakae ivo hadi mtoto mdogo ajitambue then bidada asepe. habari ya kurudiana mimi naona UKIMWI live, mwanamke akizoea kutoka nje inahitaji nguvu ya ziada kumfanya aache hiyo tabia vinginevyo, haachi.
 
Asante, nitaufanyia kazi ushauri wako.
ila swala bado lipo pale pale, baada ya hayo yote then what shall I do? should I sacrifice my happiness so that my children are happy? or should I keep on searching till god say yes? totally confused.

MUNGU ni mwema hakupi jaribu bila ufumbuzi
sasa hivi focus kwa watoto kwanza huyo mke tupa kule wanao sio wa kwanza wala mwisho kulelewa na mzazi mmoja ht humu tupo wengi tumelelewa single parent famy na tumekua huyo mkeo hujitakii mema wewe kaka
 
Inawezekana my dia
Mi ndugu yangu walifanya hivyo though at the end of the day waliachana

ht mie anko yangu na anti angu walitengana vyumba two yrs ila mwisho wametengana toka 2002 hadi leo
so ht hao wakirudiana na hvyo huyo mdada ana mdudu wa chini ndo wakatengana vyumba siku mbili nyingi
ataleta thread hapa
 
Kama utaamua kumrudisha nyumbani mkeo, muhimize kuenda kwenye nyumba za ibada.
Pole sana
 
Hiyo 6&7 hebu rudia kwanza wewe mwenyewe.
Yaani unawaza kama ukioa huyo mwanamke akulelee watoto wako ila wa kwake watakua mzigo???

Suala la kuoa hapo bora ulifute tu. Kama itakulazimu sana kuwa na mke rudiana na mama watoto wako.
 
Mkuu dhambi ya uzinzi haisameheki huyo kashakua adui yako hashindwi hata kukuua kua nae makini sana endapo atarudi wahenga walisema mwanamke akiwa na hawara hawezi kuacha,nahisi maumivu yako moyoni mwangu,!!
 
Back
Top Bottom