Sijielewi...

Sijielewi...

Vannele

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2013
Posts
287
Reaction score
90
Imepita 4 months tangu niseme it's over to my boyfriend... na nimekuwa nikijisikia furaha ya ajabu hadi najishangaa...kwani uhusiano wetu ulijawa na humiliations nyingi kutoka kwake ambazo nimekuwa nikizivumilia kwa kuwa nilimpenda kwa dhati na niliamini huenda siku moja zingekwisha lakini haikuwa hivyo zaidi ilikuwa ni kujitesa na kujiumiza... Tatizo limekuja hv karibuni, najisikia nimekabwa na kitu hapa kooni kana kwamba kuna kitu nahitaji kusema lkn nashindwa, inafika kipindi huwa naona machozi yanatoka yenyewe bila kujitambua, wakati sina tatizo linalonisumbua... Mbaya zaidi leo nimeamka nikiwa na huzuni nyingi ambayo sielewi imetoka wapi au imesababishwa na nini... Nisaidieni mwenzenu... Ni nini hiki maana sijielewi.
 
kama bado una namba yake huyo jamaa ebu mpigie simu mwambie una shida nae. Hapo nadhani mkishaonana hiyo shauku ya kutaka kuongea jambo itaisha.
 
Humiliations zipi? Kumpikia? Kumfulia nguo? Au mangeu mwenzetu?mana wadada wa sku hizi hata kupika chakula hamkawii kusema humiliations
 
...acha kuyafanyia maigizo maisha yako,hiyo furaha uliyokuwanayo baada ya kuachana na huyo mpenzi wako ilikuwa si ya-kweli,likuwa ni furaha bandi ,sasa maigizo yamaisha umeanza kuuona ukweli...kaa chini na ufikiri kwa kina je uamuzi uliufanya ulikuwa sahihi,kama ulikuwa sahihi piga moyo konde songa mbele,kama utagundua ulifanya uamuzi kwa jazba na hasira,rudi kwa mwenzio umwombe radhi...
 
very good dada,hizo ni dalili zote za ushirikina,mtu anaefanyiwa ushirikina wa kimapenzi,anakua mnyonge sana trust me nimewahi kuona hii kitu sana,na kinachokukaba kwenye koo ni hali ya ushirikina pia,jitahidi sana kusali na kutokuonana na huyo jamaa ukimuona tu umerudi!
 
Namba yake nishadelete kwenye cm yangu na pia nafanya jitihada kuifuta kichwani maana sitaki kurudi nilipotoka... Niliteseka sana kwenye hiyo relationship Esii... Nataka nianze upya.
 
We acha mambo yako.....mtu ana msongo huyo we unamwambia karogwa......dawa pekee nu kuonana nae tu mzungumze yakaisha
 
  • Thanks
Reactions: naa
very good dada,hizo ni dalili zote za ushirikina,mtu anaefanyiwa ushirikina wa kimapenzi,anakua mnyonge sana trust me nimewahi kuona hii kitu sana,na kinachokukaba kwenye koo ni hali ya ushirikina pia,jitahidi sana kusali na kutokuonana na huyo jamaa ukimuona tu umerudi!
Inawezekana? Siamini ktk hilo...
 
...acha kuyafanyia maigizo maisha yako,hiyo furaha uliyokuwanayo baada ya kuachana na huyo mpenzi wako ilikuwa si ya-kweli,likuwa ni furaha bandi ,sasa maigizo yamaisha umeanza kuuona ukweli...kaa chini na ufikiri kwa kina je uamuzi uliufanya ulikuwa sahihi,kama ulikuwa sahihi piga moyo konde songa mbele,kama utagundua ulifanya uamuzi kwa jazba na hasira,rudi kwa mwenzio umwombe radhi...
Nina nia ya dhati kujitoa huko wala si maigizo Sabu...
 
Humiliations zipi? Kumpikia? Kumfulia nguo? Au mangeu mwenzetu?mana wadada wa sku hizi hata kupika chakula hamkawii kusema humiliations
Kazi za nyumbani sio issue kwangu... na bora ht ningetolewa mangeu...ila visa vyake ni zaidi ya ngeu...
 
Kuamka na huzuni ama kujisikia una fundo haihusiani na kuacha nae. Mfikirie in these terms, angeweza kufariki na huku angali anakupenda si ungeumia zaidi? Jiweke busy, toka na marafiki. Unaweza kumhadithia rafiki yako wa karibu msherehekee pamoja uhuru huu. Kulikoni ulie machozi ukiwa nae ni bora ulie ukiwa huru. Lia tu itasafisha macho yako na kuondoa dukuduku.
 
Kumliposha bills mwanamke ndio humiliation. Unamfanya jike dume. Lol
Humiliations zipi? Kumpikia? Kumfulia nguo? Au mangeu mwenzetu?mana wadada wa sku hizi hata kupika chakula hamkawii kusema humiliations
 
Imepita 4 months tangu niseme it's over to my boyfriend... na nimekuwa nikijisikia furaha ya ajabu hadi najishangaa...kwani uhusiano wetu ulijawa na humiliations nyingi kutoka kwake ambazo nimekuwa nikizivumilia kwa kuwa nilimpenda kwa dhati na niliamini huenda siku moja zingekwisha lakini haikuwa hivyo zaidi ilikuwa ni kujitesa na kujiumiza... Tatizo limekuja hv karibuni, najisikia nimekabwa na kitu hapa kooni kana kwamba kuna kitu nahitaji kusema lkn nashindwa, inafika kipindi huwa naona machozi yanatoka yenyewe bila kujitambua, wakati sina tatizo linalonisumbua... Mbaya zaidi leo nimeamka nikiwa na huzuni nyingi ambayo sielewi imetoka wapi au imesababishwa na nini... Nisaidieni mwenzenu... Ni nini hiki maana sijielewi.

ulimpenda kupita kiasi ndio sababu..
 
Namba yake nishadelete kwenye cm yangu na pia nafanya jitihada kuifuta kichwani maana sitaki kurudi nilipotoka... Niliteseka sana kwenye hiyo relationship Esii... Nataka nianze upya.

come to my side gal..
 
Back
Top Bottom