Ni kama umejaza tope kichwani mwako, kwamba huelewi chochote.
Kama CCM inazo sifa hizo unazoimba hapo, inaogopa kitu gani kuwepo na uchaguzi HURU na HAKI. Kila mpiga kura apige kuchagua mgombea yeyote anaye mtaka amwongoze. Hili kichwani mwako ni gumu sana kulielewa?
Hata hivyo, nataka uelewe kwamba haya yanayofanyika sasa CCM, kama chama hakihusiki. Huu ni mpango wa genge lenu linalolazimisha Samia abaki madarakani kwa gharama ya uhai wa waTanzania. Hili halina uhusiano wowote na CCM kama chama.
Mnakitanguliza chama kama lebo tu ya kufanyia uovu wenu.
Watu wa kudhibitiwa ni genge lenu linalotafuta kusababisha maafa kwenye taifa hili.