Sijawahi kushuhudia Tanzania ya aina hii

labda nkushauri, kula vizuri tafuta cha kuwapa watoto wako ukiwa haupo unachofanya saahv hakina manufaa yoyote ata tukikuweka wewe kama president mtoto wako hatorithi icho cheo, kwahio punguza pumba go and improve yourself hakuna sehem yoyote kuna haki, ata shetan aliitaman nafasi ya Mungu na kilimchomkuta ni historia
Huo ni ushauri wa kipumbavu, kwa sababu uwezo wa kukulisha wewe na vitoto vyako ninao. Kama utakuwa tayari kujiondoa kwenye hiyo mipango ovu juu ya Tanzania yetu, njoo kwangu, nitakupa msaada wa kuendesha maisha yako hadi kifo kikuchukue.
Umeelewa!
 
ukishaanza kuona mtu anaongelea pesa sana ujue ni fukara sana, matajiri wote wana tafuta njia za kuficha pesa kila sku, wewe tulia enjoy mihogo
 
Mara hii umesahau hapo juu uliyo yasema kuhusu hilo!
Huko kichwani kweli zinakutosha!
Na ujue sitanii, ni bora uje nikupe msaada, badala ya kutafuta haramu ya damu ya waTanzania.
 
hakuna sehem yoyote kuna haki, ata shetan aliitaman nafasi ya Mungu na kilimchomkuta ni historia
Sasa fikiria, mtu kama huyu kajivisha kabisa magwanda ya chama; halafu anajionyesha waziwazi jinsi alivyo mwovu mbele za watu!
 
toka ccm wapigwe 3 bila na mfugaji wa monduli wamepagawa yani wewe uibe kura usizisindikize na mtutu kura za wizi na haushindi njia pekee ni kumtumia jaji kikombe pale tume huru kuvuruga uchaguzi, kwakweli ccm mnatuonea watanzania kweli mimi na MBA yangu niende veta hapana kwakweli nitamuua alienilipia ada kwa msongo wa mawazo pumpizikeni kidogo madarakani mtarudi lakini mkiwa safi kwa sasa mwachieni uncle Tundu atuongoze na asuke mifumo ya nchi tunapigwa sana kimataifa na ndani yaani ccm wezi na mafisadi ndani ya nchi hawafungwi mtaweza wezi wa kwenye mikataba kutoka nje pumzikeni ccm.
 
Sasa fikiria, mtu kama huyu kajivisha kabisa magwanda ya chama; halafu anajionyesha waziwazi jinsi alivyo mwovu mbele za watu!
we elewa hakunaga kitu kinaitwa haki, wala democracy njaa tu inakusumbua
 
Mojawapo ya makosa wayafanyao watawala ni kuamini kwamba kila mwenye maoni/mawazo tofauti na wao ni adui, pia kuamini kwamba vyama vya upinzani ni vya kutokomezwa na kwamba wananchi hawana shida, na wao wanapendwa na wanakubalika sana na wananchi, kumbe wasichojua ni kwamba wananchi wengi ambao si wanachama wa vyama vya upinzani wameshaichoka serikali na chama chake ila hawajapata namna ya kuwaadabisha watawala, ni suala la muda tu. Kwa mazingira tuliyonayo sasa CCM imepoteza sifa ya kuwa chama cha siasa bali ni himaya ya kiuchumi na fursa za kibiashara kwa wanachama wake (Economic empire), hivyo wanaoikosoa serikali na chama tawala wanaonekana ni maadui si kwasababu za kisiasa bali ni tishio la kiuchumi kwa watawala. Wale wanaoitwa ‘viongozi’ hawana hata chembe ya sifa za uongozi bali wamepata fursa za kukalia nafasi za uongozi, lakini ni dhahiri wameshindwa kuongoza ila kwasababu za kiuchumi inabidi walazimishe kuendelea kuwepo madarakani - ni uchumi tu. Ndiomaana hao wanaoitwa ‘viongozi’ hawatoi suluhisho lolote katika kutatua changamoto za wananchi bali ni kujilimbikizia wao mali lukuki - sio siasa bali uchumi tu
Kujilimbikizia mali kupita kiasi
 
Si
Naomba nikiri kwamba, katika uhai wangu wa miongo ya kutosha kuitwa kikongwe, nimeshuhudia mambo mengi sana ya maana na ya hovyo ndani ya Tanzania.

Kwa miaka mingi Watanzania walikuwa ni watu ambao ndani kama zilivyo nchi nyingine waligawanyika na kutofautiana sana, kimitazamo, kimaslahi , kiimani na kiitikadi na kupitia tofaut hizo waliweza ku find their strengths wakaungana na kuwa wamoja na kishindo cha umoja na nguvu yao ilivuka mipaka ya nchi na kusikika kote barani Afrika.

Wao kwa wao ilikuwa ni kawaida kutofautiana, kugombana na hata kuchapana, lakini ilipotokea mtu wa nchi nyingine kujaribu kuingilia au ku take side, watanzania waliweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mtu huyu

Siku za karibuni, taratibu tulianza kushuhudia hali hiyo ikitoweka. Upendo wa Kinafiki ukachulua hatamu, hofu na chuki na ukatili navyo vikajichukulia nafasi.

Watawala wakaingiwa na hofu ya kupoteza madaraka, na hofu ilipozidi wakaanza kuwa makatili, wakatengeneza makundi ya watu kwa ajili ya kuumiza wengine. Wakatengeneza makundi ya vijana kwa ajili ya propaganda na matusi mitandaoni.

Nilishitushwa jinsi taarifa za hali ya matokeo ya mapigano kule Congo DRC ilivyokuwa zikipokewa nchini, ziwe zilikuwa za kweli au uongo nilishangazwa na hali ya kutojali kwa watanzania na kwa waliojali walionyesha kutamani iwe zaidi ya ilivyokuwa... nikadhani naota.

Sasa hivi limitokea hili la Wakenya kudukua mitandao ya taasisi nyeti nchini, na kutumia mitandao hiyo kusambaza taarifa za kusikitisha na zisizo rafiki ingawa zina ujumbe ndani yake.

Nchi imetikisika, lakini watanzania wanaoshangilia hili wanasikika zaidi kuliko wanaopinga. Watanzania wameshindwa kuungana, sasa hivi wanashangilia yeyote mwenye kuonekana kuwa na mbinu ya kuweza kuisumbua na kuiumiza serikali.

Vile vikundi vya propaganda na matusi vya mitandaoni vilivyotengenezwa na Chama na Serikali navyo hawasikiki katika wakati huu, wanepoteana.

Naililia Tanzania yangu, nchi imegawanyika sana, wananchi wake siyo wale tena ambao akitokea mvamizi walikuwa wakiweka ugomvi na tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mvamizi, sasa hivi wanaombea kabisa mabaya yashuke mapema, wapo tayari kutoa msaada kwa wavamizi itakapohitajika.

Kuna kitu kinatakiwa kufanyika, ila kwa sababu za kihistoria au za kukosa maono, tutashupaza shingo.

Hekima na Busara viwaingie watawala ili kuiweka nchi pamoja. Mtapiga risasi wananchi na baadaye mtawagusa ndugu, wake, waume, wazazi na, watoto wa maaskari hao na Ikifika hapo itaanza kuwa vita ya askari kwa askari huku raia nao wakiungana dhidi ya askari.

Tusifike huko, nchi ni yetu sote, mambo yasiyo na afya yarekebishwe ili tuendelee kuijenga nchi.

Nimestuka sana vile watanzania wameshindwa kuungana katika sakata hili linaloendelea.

Mazingira haya, ingawa hatuombei, lakini ikitokea nchi ikatuvamia ninaamini tutaaibika, Jeshi la Wananchi ili liwe imara linahitaji sana hamasa kutoka kwa wananchi, na Wananchi wenyewe ndiyo hawa ambao akitokea adui kwao atakuwa ni 'Mkombozi', tunajitengenezea mazingira yale yaliyotuwezesha kumuondoa Iddi Amin. Kule Uganda.

Tusidanganyane, si jeshi wala Polisi wanaoweza kutuliza hali hii, so far kutumika kwao kumepelekea mwelekeo ubadilike na kuelekea Korongoni.

TUJIREKEBISHE!!
Sidhani kama kuna mtu anakuelewa, maneno yako ni magumu sana kueleweka maana watu washafika mbali sana. Na hawana mpango wa kugeuka nyuma. Pole sana nchi yangu tz
 
Anaeleweka vizuri sana, mkuu 'Zamazangu'.

Leo hii akitokea kiongozi, Mzalendo wa kweli wa nchi hii; utaona mambo yanavyo badilika haraka sana.
Tumwombe tu Mungu, atajaalie kuwapata viongozi hao mapema iwezekanavyo wakati huu.
 
Waelezeni hivyo waTanzania wajue waziwazi nia zenu ovu; badala ya kujificha nyuma ya kivuli cha AMANI, AMANI, AMANI!
ebu kula kijana unakaza fuvu sana, ccm utaondoka utaiacha
 
CCM siyo Samia Suluhu Hassan; unajua hivyo, au nalo unataka ufundishwe.
Umevaa shati la kijani hapo, bila ya kuwa na sifa yoyote ya kushika wadhifa huo, sasa unadai CCM ndiyo Samia?
 
Naomba nikiri kwamba, katika uhai wangu wa miongo ya kutosha kuitwa kikongwe, nimeshuhudia mambo mengi sana ya maana na ya hovyo ndani ya Tanzania.

Kwa miaka mingi Watanzania walikuwa ni watu ambao ndani kama zilivyo nchi nyingine waligawanyika na kutofautiana sana, kimitazamo, kimaslahi , kiimani na kiitikadi na kupitia tofaut hizo waliweza ku find their strengths wakaungana na kuwa wamoja na kishindo cha umoja na nguvu yao ilivuka mipaka ya nchi na kusikika kote barani Afrika.

Wao kwa wao ilikuwa ni kawaida kutofautiana, kugombana na hata kuchapana, lakini ilipotokea mtu wa nchi nyingine kujaribu kuingilia au ku take side, watanzania waliweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mtu huyu

Siku za karibuni, taratibu tulianza kushuhudia hali hiyo ikitoweka. Upendo wa Kinafiki ukachulua hatamu, hofu na chuki na ukatili navyo vikajichukulia nafasi.

Watawala wakaingiwa na hofu ya kupoteza madaraka, na hofu ilipozidi wakaanza kuwa makatili, wakatengeneza makundi ya watu kwa ajili ya kuumiza wengine. Wakatengeneza makundi ya vijana kwa ajili ya propaganda na matusi mitandaoni.

Nilishitushwa jinsi taarifa za hali ya matokeo ya mapigano kule Congo DRC ilivyokuwa zikipokewa nchini, ziwe zilikuwa za kweli au uongo nilishangazwa na hali ya kutojali kwa watanzania na kwa waliojali walionyesha kutamani iwe zaidi ya ilivyokuwa... nikadhani naota.

Sasa hivi limitokea hili la Wakenya kudukua mitandao ya taasisi nyeti nchini, na kutumia mitandao hiyo kusambaza taarifa za kusikitisha na zisizo rafiki ingawa zina ujumbe ndani yake.

Nchi imetikisika, lakini watanzania wanaoshangilia hili wanasikika zaidi kuliko wanaopinga. Watanzania wameshindwa kuungana, sasa hivi wanashangilia yeyote mwenye kuonekana kuwa na mbinu ya kuweza kuisumbua na kuiumiza serikali.

Vile vikundi vya propaganda na matusi vya mitandaoni vilivyotengenezwa na Chama na Serikali navyo hawasikiki katika wakati huu, wanepoteana.

Naililia Tanzania yangu, nchi imegawanyika sana, wananchi wake siyo wale tena ambao akitokea mvamizi walikuwa wakiweka ugomvi na tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya mvamizi, sasa hivi wanaombea kabisa mabaya yashuke mapema, wapo tayari kutoa msaada kwa wavamizi itakapohitajika.

Kuna kitu kinatakiwa kufanyika, ila kwa sababu za kihistoria au za kukosa maono, tutashupaza shingo.

Hekima na Busara viwaingie watawala ili kuiweka nchi pamoja. Mtapiga risasi wananchi na baadaye mtawagusa ndugu, wake, waume, wazazi na, watoto wa maaskari hao na Ikifika hapo itaanza kuwa vita ya askari kwa askari huku raia nao wakiungana dhidi ya askari.

Tusifike huko, nchi ni yetu sote, mambo yasiyo na afya yarekebishwe ili tuendelee kuijenga nchi.

Nimestuka sana vile watanzania wameshindwa kuungana katika sakata hili linaloendelea.

Mazingira haya, ingawa hatuombei, lakini ikitokea nchi ikatuvamia ninaamini tutaaibika, Jeshi la Wananchi ili liwe imara linahitaji sana hamasa kutoka kwa wananchi, na Wananchi wenyewe ndiyo hawa ambao akitokea adui kwao atakuwa ni 'Mkombozi', tunajitengenezea mazingira yale yaliyotuwezesha kumuondoa Iddi Amin. Kule Uganda.

Tusidanganyane, si jeshi wala Polisi wanaoweza kutuliza hali hii, so far kutumika kwao kumepelekea mwelekeo ubadilike na kuelekea Korongoni.

TUJIREKEBISHE!!
Naomba hata kesho Zanzibar na Tanganyika huu muungano uvunjike Kila mtu akae kwake,
 
Back
Top Bottom