godoro-la-comfy
Member
- Sep 9, 2013
- 52
- 28
Kama utakuwa umebeba Sembe wewe relax tu, ukiwa na papara utadakwa. Ila kama unasafiri tu kama abiria mwema tulia na utajifunza kutoka kwa muudumu au kuiga kwa abiria wenzako.
Mpaka sasa...sijapata jibu lolote. ..watu wa jf mnaudhi wakati mwingine..daah. Mnajibu mavimavi tu
Ok,jibu ni hili, ndege ni kama usafiri mwingine wowote,huwezi kukwama ukifika airport kwani utadesa kwa abiria wengine, ndani ya ndege ukijisikia kuchimba dawa unabonyeza kengele rubani anasimamisha kwenye kichaka unashuka na kushusha mzigo,pia usisahau kuomba siti ya dirishani ili uweze kununua vitu njiani na pia iwe rahisi ukitaka kutapika unatoa tu kichwa nje...safari njema.
Umeniharibia nadhiri yangu,nilitaka kununa siku nzima ona sasa nimecheka!Sorry...nilitaka niiweke huku..nikakosea nikaiweka kwenye kazi na tenda. Na sijui jinsi ya kufuta thread. Sijui mnafutaje..mi mgeni humu...natokea Mwanza..kwimba.
Wadau..mi kusema cha ukweli sijawahi kupanda ndege toka nimezaliwa. Nataman sana siku moja kuipanda. Umri wangu ni miaka 35. Naomba tuelimishane....siku ya kwanza inakuagaje?..Nikifika pale airpot JINIA...naelekea wapi na wapi mpaka naingia ndani ya ndege?..na humo kwenye ndege nasikia kuna mikanda unajifunga....je unaweza kutembea humo ndani wakati ndege ikiwa juu?..natamani kujua kiujumla...habari za ndege. Sagari za ndani na za yale madege makubwa ya nje.
Kuna uzi humu wa mwaka jana kama sikosei. Mwenzio aliuliza swali kama hili alikuwa anajiandaa kutoka Mwanza kwenda Dar .Majibu aliyapata, nikikumbuka nacheka sana. Utafute uzi huo.
Ok,jibu ni hili, ndege ni kama usafiri mwingine wowote,huwezi kukwama ukifika airport kwani utadesa kwa abiria wengine, ndani ya ndege ukijisikia kuchimba dawa unabonyeza kengele rubani anasimamisha kwenye kichaka unashuka na kushusha mzigo,pia usisahau kuomba siti ya dirishani ili uweze kununua vitu njiani na pia iwe rahisi ukitaka kutapika unatoa tu kichwa nje...safari njema.
Mnaudhi sana humu. Mavi kabisa....mmnfyuuuuuuussss
..Mkuu MbongoTZ, hapo kweny mstari umemdanganya mwenzetu anayetafuta Ushauri kwetu. Ndege haisimami kwenye Kichaka ila inasimama kwenye Wingu zito kwa ajili ya Abiria wanaotaka Kuchimba dawa!:becky: