Sijaona Jeshi Bora kwa sasa Afrika nzima kama letu la JWTZ, pongezi nyingi mno Kwao

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Nimebahatika Kukutana mahala na Wakufunzi Watatu wa Angola, Rwanda na Misri pamoja Wanajeshi wa Afrika Kusini na kwa Mshangao mkubwa wakaniambia MINOCYCLINE kuwa bado kwa sasa hawajaona Jeshi lolote la nchi za Bara la Afrika ( zikiwemo zao Wanazotoka ) lenye Ubavu wa Kupambana na Jeshi la uhakika la JWTZ.

Kiukweli wote walinipa sababu mbalimbali za Kimedani ( ambazo kwa Unyeti wake ) sitozianika hapa, ila itoshe tu kusema kama Wewe ni Mtanzania kama Mimi MINOCYCLINE basi Jivunie na tembea Kifua mbele kuwa Jeshi la Tanzania ( JWTZ ) halina Mpinzani Afrika.

Halafu anatokea Mlevi Mmoja wa Gongo anasema JWTZ halina Uweledi, linapiga hovyo Raia, sijui waombwe Radhi na kutishia Kuwaroga Wanajeshi wetu akisahau kuwa hii Amani Kubwa iliyoko nchi hii na inayomfanya awe Huru Kutwa na ID yake Kuonekana, Kutamba na Kujulikana ni Matunda ya Uimara wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania ( JWTZ )

I'm proud of TPDF and CDF Gen. Mkunda.
 
Ubora unatestiwa front line , jeshi letu linaenjoy na linapitia kipind cha Aman ni rahs kila kitu kukiona kipo Sawa
 
Huyu huyu genta aliesema wanajesh wa kawe wamemnanii leo huyohuyo anakuja kusema jesh boraa hahaha dah we genta mamame
 
Nimebahatika Kukutana mahala na Wakufunzi Watatu wa Angola, Rwanda na Misri pamoja Wanajeshi wa Afrika Kusini na kwa Mshangao mkubwa wakaniambia MINOCYCLINE kuwa bado kwa sasa hawajaona Jeshi lolote la nchi za Bara la Afrika ( zikiwemo zao Wanazotoka ) lenye Ubavu wa Kupambana na Jeshi la uhakika la JWTZ.

Kiukweli wote walinipa sababu mbalimbali za Kimedani ( ambazo kwa Unyeti wake ) sitozianika hapa, ila itoshe tu kusema kama Wewe ni Mtanzania kama Mimi MINOCYCLINE basi Jivunie na tembea Kifua mbele kuwa Jeshi la Tanzania ( JWTZ ) halina Mpinzani Afrika.

Halafu anatokea Mlevi Mmoja wa Gongo anasema JWTZ halina Uweledi, linapiga hovyo Raia, sijui waombwe Radhi na kutishia Kuwaroga Wanajeshi wetu akisahau kuwa hii Amani Kubwa iliyoko nchi hii na inayomfanya awe Huru Kutwa na ID yake Kuonekana, Kutamba na Kujulikana ni Matunda ya Uimara wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania ( JWTZ )

I'm proud of TPDF and CDF Gen. Mkunda.
Unapoleta hoja unatakiwa uwe na vyanzo viingi vya kujitetea ..umekutana na watu watatu tu unaona utafiti wako umekamilika jipange tenah
 
Amani hii ipo tu nafikir ni Mungu Mwenyewe kaamua iwe hivyo.sio Taasisi Wala chama flani.Kama Israel na Mossad na IDF na Taifa Teule kimenuka.Marekani na CIA na FBI Alipigwa sembuse Tanzania na vijana wa kuvunja Tofali pale Uwanja wa Uhuru
 
Nadhani umedandiwa na Wajeda unawaanza kuwasafisha

Uliwachafua Ukidhani watakuacha salama

Pole sana dogo
 
Nakumbuka hata Rais wetu wa awamu ya 5 aliwahi kudokeza hii.

Alisema "kwa sasa jeshi letu JWTZ ni jeshi imara kama yalivyo majeshi mengine unayoyajua duniani".

Kwa sasa lipo nafasi ya 6 kidunia.

Hata kama wewe ni kizazi Cha internet amini hiki nilichokiandika. Trust me.

MAGUFULI4LIFE.
 
Back
Top Bottom