Pongezi Jeshi la Polisi. Japo Nabii hakubaliki nyumbani, Jeshi sasa ni Sikivu, Most friendly na very hospitable

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Wanabodi,

Hili ni bandiko la pongezi kwa Jeshi letu la Polisi nchini, Japo Nabii Huwa Hakubaliki Nyumbani, Lakini Jeshi Letu La Polisi Sasa ni Jeshi sikivu lenye kutenda wema kama Malaika Usikute Polisi Wetu Ndio Most Friendly na Very Hospitable!, linastahili pongezi za that, kunapotokea jinai kama ya Lisu, linaomba kwanza kuwahoji mashahidi, likikataliwa, linasubiri hadi liruhusiwe!. Hili ni jambo jema na linastahili pongezi, kwenye mazuri jameni, tupongeze!.

Declaration of Interest
Paskali ni mtoto wa askari kwa wazazi wake wote wawili, hivyo ana damu ya kiaskari ambayo ni ya uzalendo wa kweli wa nchi yake, hata ukimkata, inatoka damu yenye rangi za Tanzania, na alipitia JKT, baadaye akajiunga na JWTZ, hivyo ni mjeshi kamili wa reserve, leo ikitangazwa vita, naingia mstari wa mbele, hivyo pongezi hizi kwa jeshi letu ni pongezi za kuonyesha uzalendo kwa jeshi letu la polisi na kwa nchi yangu Tanzania. Najua kufuatia watu kupigika sana na mkazo wa vyuma vya Magufuli, hivyo kuna watu wakisikia tuu mtu anapongeza jambo lolote zuri kwa serikali ya awamu ya tano, anakasirika na hunyooshewa vidole kuwa anatafuta uteuzi, mimi sina chama na sitafuti uteuzi wowote!.

Nabii Huwa Hakubaliki Nyumbani, Polisi Wetu Sasa ni Wema Kama Malaika!.
Kuna huu msemo kuwa "Nabii huwa hakubaliki nyumbani", siku zote wengi wetu huwa tunatupa lawama mbalimbali kwa jeshi letu la polisi kuhusu utendaji wake, na lawama hizo huwa tunazitoa pale tuu jeshi hilo linapotenda ndivyo sivyo, lakini jeshi letu la polisi, linapotenda mambo mema, au mambo mazuri, ni aghlabu sana kulipongeza, hivyo hili ni bandiko la pongezi kwa jeshi letu la polisi kwa kuwa jeshi sikivu lenye subra. Zamani kuitwa kuhojiwa polisi ilikuwa ni amri, sasa ni ombi, tena ukikataa, polisi wanasubiri mpaka siku utakapokubali!, huu ni wema ulioje?. Naendelea kusisitiza, wana jf, kwenye mazuri tupongeze, mabaya tukosoe na mapungufu turekebishe.

Kuna uwezekano mkubwa, Jeshi letu la Polisi Tanzania, Ndio Most Friendly na Most Hospitable Jeshi la Polisi Duniani!.
Kunapotokea jinai kubwa kama ya mtu kushambuliwa risasi Zaidi 40, jeshi hili halianzishi uchunguzi wa kuwahoji mashahidi immediately, bali huomba kuwahoji, na kumsubiri hadi muhojiwa akubali kuhojiwa, ndipo jeshi letu hutuma watu kufanya mahojiano hayo!. Huu ni wema mkubwa wa ajabu kwa jeshi letu, hii ni dalili, jeshi la polisi la Tanzania, linaweza kuwa ndio the most friendly, the most humanly na the most hospitable police force in the world, shahidi wa jinai, anahojiwa pale tuu anaporuhusu kuhojiwa!, na kusema ukweli utaratibu huu ukidumishwa, hata msongamano kwenye mahabusu zetu, utapungua.

Pongezi hizi nazitoa kufuatia taarifa hii ya IGP Simon Sirro kuhusu kutumwa kwa makachero wawili wa Jeshi letu la polisi kwenda jijini Nairobi kumhoji Lissu na dereva wake kuhusiana na shambulio la Lussu, lililotokea miezi 3 iliyopita.

Taarifa yenyewe ni hii
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amesema timu ya wapelelezi imetumwa kwenda Nairobi, Kenya kufanya mahojiano na Tundu Lissu.

Akizungumza jana na Nipashe katika mahojiano maalum, IGP Sirro alisema wametuma wapelelezi Nairobi baada ya kusikia Lissu amekubali kuhojiwa juu ya tukio hilo na matarajio yao pia ni kuwapata dereva na mlinzi wake.

“Tumetuma watu wetu kwenda kuchukua maelezo yake (Lissu)," alisema IGP Sirro. "Mwanzo tuliomba kwenda lakini chama (Chadema) walikataa. Juzi tumesikia wamesema wapo tayari".

"Tumetuma vijana wetu wawili kwenda Nairobi kuchukua maelezo yake.”

CHANZO: Nipashe
Jeshi la Polisi Sasa ni Jeshi Sikivu, Jeshi La Maombi na Sio Amri.
Natamani kuliona hilo ombi la polisi kufanya mahojiano, kwa kawaida utendaji wote wa serikali ni kwa maandishi, naamini hata hilo ombi la polisi kufanya mahojiano lilitolewa kwa maandishi, na Chadema walipokataa, naamini pia walikataa kwa maandishi, na Chadema walipokubali kuhojiwa, naamini wamewaandikia polisi kuwa sasa wako tayari kuhojiwa, maana Kamanda Sirro, amesema juzi wamesikia, kuwa Lissu yuko tayari kuhojiwa, sijui polisi watakuwa wamesikia wapi kuwa sasa Lissu tayari kuhojiwa, maana siku Lissu anatangaza mbele ya waandishi kuwa anafuatiliwa na hadi kutaja number ya gari inayomfuatilia, na kuwa maisha yake yako hatarini, jeshi la polisi, halikusikia, na msemaji wa polisi alisema kuwa jeshi la polisi halina masikio ya kusikia malalamiko yanayotolewa kwenye press conferences, lenyewe linasikia malalamiko yanayoripotiwa kituo cha polisi tuu, hivyo Lissu ilimpasa kuripoti polisi na sio kuripoti kwenye press conference, hivyo hawakufanya lolote, lakini sasa ni jeshi sikivu, hii ya jeshi kusikia Lissu yuko tayari kuhojiwa, bila Lissu kuripoti kituo chochote cha polisi, ni dalili njema kuwa sasa jeshi letu la polisi ni jeshi sikivu, linaweza hata kusikia tuu vitu kwenye media na ku act upon, japo haina maana watu sasa wasiripoti polisi, kuripoti polisi bado kuko pale pale, ila sasa jeshi letu la polisi pia ni sikivu, na lina masikio ya kusikia vitu kwenye media!.

Jeshi La Polisi Linastahili Pongezi, Kwa Kuwa Jeshi Rafiki Kuliko Polisi Wote Duniani!.
Likitaka Kufanya Mahojiano, Linaomba, Likikataliwa Linasubiri Hadi Liruhusiwe!.

Kumbe siku hizi, polisi wetu wakitaka kufanya uchunguzi wa kijinai, huwa wanaomba kwanza ruhusa ya kuhoji, na wanasubiri kwanza ruhusu ya wahusika, ndipo wafanye mahojiano ya kiuchunguzi!, shambulizi la Lissu limetokea miezi zaidi ya mitatu imepita bila taarifa zozote za uchunguzi wa tukio hilo, IGP Sirro anasema mwanzo waliwaomba Chadema, wakakataa!, kumbe uchunguzi wa kijinai siku hizi watu wanaombwa kuhojiwa!, ukitaa hauhojiwi, hadi ukubali!, lakini sasa Chadema wamesema wako tayari, hivyo ndio sasa jeshi letu la polisi, limetuma watu Nairobi kwenda kuwahoji!. Bahati nzuri sana Lissu na Dereva wake wana photographic memory za gigabites kubwa au telebites kabisa, kuweza kukumbuka kila kitu kilichotokea miezi mitatu iliyopita!, hawa ndio polisi wetu!.

Hongera Sana Jeshi Letu la Polisi.
Inawezekana polisi wetu ndio the most friendly police force dunia nzima!. Uhalifu ufanyike, tena jinai ya kutishia maisha ya mtu, shahidi muhimu kakimbilia nchi jirani ya Kenya, Tanzania na Kenya tuna mkataba wa ushirikiano kwenye uhalifu, polisi wetu walishindwa nini kumhoji dereva wa Lissu huko huko Nairobi siku zote hizi?!, kumbe walikuwa wanasubiri ruhusa ya Chadema!. Big up sana kwa polisi wetu.

Hitimisho.
Kama ambavyo huwa tunawalaumu polisi kwa mabaya, yakitokea mazuri kwa polisi wetu, jameni pia tuwapongeze, kama hili la kuomba kuhoji mashahidi na kusubiria hadi ruhusa itoke, sio jambo dogo!. Hongera sana polisi wetu.

Paskali
Rejea za maandiko yangu kuhusu Polisi
TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II!
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Ombi Muhimu Kwa Jeshi Letu La Polisi."Nyinyi ni Wenzetu, September Mosi, Please Msigeuke Makaburu!".
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,615
2,000
Nikupata sana mkuu Pascal ila uwe makini.... ila...

Sintakaa nisahau siku ambayo JESHI LA POLISI waliponipakazia kesi ya KUIBA KWA KUTUMIA SILAHA!! Niliwekwa ndani bila kosa...

Kwa kifupi nikimuona polisi naona usalama wangu uko mashakani....Ni bora nimuamini mbwa atanilindia nyumba yangu kuliko kumuamini polisi ambaye muda wowote anaweza kunibammbikizia kesi!!!
 

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,946
2,000
Hongera Sana Jeshi Letu la Polisi.
Inawezekana polisi wetu ndio the most friendly police force dunia nzima!. Uhalifu ufanyike, tena jinai ya kutishia maisha ya mtu, Tanzania na Kenye tuna mkataba wa ushirikiano kwenye uhalifu, polisi wetu walishindwa nini kumhoji dereva wa Lissu huko huko Nairobi siku zote hizi?!, kumbe walikuwa wanasubiri ruhusa ya Chadema!. Big up sana kwa polisi wetu.

Umeona Barua ya ruksa au ndiyo mambo yetu ya uandishi???????????????
 

mwayungi

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,773
2,000
Unazungumzia hawa polisi waliotuvamia mimi na kaka yangu SAA sita usiku pale ukonga Mombasa na kutupiga kutupora vitu vyetu au unazungumzia police hawa walionikamata nikiendesha gari na leseni ninayo wakikataa kuwa umri wangu sio wa kumiliki leseni???Wewe paskal bado hayakukuta mkuu police ni waonevu sana binafsi nikimkuta police amegongwa na gari namwagia petrol nampiga moto
 

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,786
2,000
Wanabodi,

Hili ni bandiko la pongezi kwa Pongezi kwa Jeshi letu la Polisi nchini, Japo Nabii Huwa Hakubaliki Nyumbani, Lakini Jeshi Letu La Polisi Sasa ni Jeshi Malaika kwa Wema, Ni Sikivu, Most Friendly na Very Hospitable!, linastahili pongezi, kwenye mazuri jameni, tupongeze!.

Declaration of Interest
Paskali ni mtoto wa askari kwa wazazi wake wote wawili, hivyo ana damu ya kiaskari ambayo ni ya uzalendo wa kweli wa nchi hii, na alipitia JKT, baadaye akajiunga na JWTZ, hivyo ni mjeshi kamili wa reserve, leo ikitangazwa vita, naingia mstari wa mbele, hivyo pongezi hizi kwa jeshi letu ni pongezi za kuonyesha uzalendo kwa jeshi letu la polisi na kwa nchi yangu Tanzania. Najua kuna watu wakisikia tuu mtu anapongeza jambo lolote zuri kwa serikali hii, hunyooshewa vidole kuwa anatafuta uteuzi, mimi sina chama na sitafuti uteuzi wowote!.

Nabii Huwa Hakubaliki Nyumbani, Polisi Wetu Sasa ni Wema Kama Malaika!.
Kuna huu msemo kuwa "Nabii huwa hakubaliki nyumbani", siku zote wengi wetu huwa tunatupa lawama mbalimbali kwa jeshi letu la polisi kuhusu utendaji wake, na lawama hizo huwa tunazitoa pale tuu jeshi hilo linapotenda ndivyo sivyo, lakini jeshi letu la polisi, linapotenda mambo mema, au mambo mazuri, ni aghlabu sana kulipongeza, hivyo hili ni bandiko la pongezi kwa jeshi letu la polisi. Naendelea kusisitiza, wana jf, kwenye mazuri tupongeze, mabaya tukosoe na mapungufu turekebishe.

Nimesema nabii huwa hakubaliki nyumbani, lakini amini usiamini, kuna uwezekano mkubwa,
Jeshi letu la Polisi Tanzania, Ndio Most Friendly na the most Hospitable Jeshi la Polisi Duniani!.

Kunapotokea jinai kubwa kama ya mtu kushambuliwa risasi Zaidi 40, jeshi hili halianzishi uchunguzi wa kuwahoji mashahidi immediately, bali huomba kuwahoji, na kumsubiri hadi muhojiwa akubali kuhojiwa, ndipo jeshi letu hutuma watu kufanya mahojiano hayo!. Huu ni wema mkubwa wa ajabu kwa jeshi letu, hii ni dalili, jeshi la polisi Tanzania, linaweza kuwa the most friendly, the most humanly na most hospitable police force in the world, shahidi wa jinai, anaohojiwa pale tuu anaporuhusu kuhojiwa!, na kusema ukweli utaratibu huu ukidumishwa, hata msongamano kwenye mahabusu zetu, utapungua.

Pongezi hizi nazitoa kufuatia taarifa hii ya IGP Simon Sirro kuhusu kutumwa kwa makachero wawili wa Jeshi letu la polisi kwenda jijini Nairobi kumhoji Lissu na dereva wake kuhusiana na shambulizi la Lissu.

Taarifa yenyewe ni hii

Jeshi la Polisi Sasa ni Jeshi Sikivu
Natamani kuliona hilo ombi la polisi kufanya mahojiano, kwa kawaida utendaji wote wa serikali ni kwa maandishi, naamini hata hilo ombi la polisi kufanya mahojiano lilitolewa kwa maandishi, na Chadema walipokataa, naamini pia walikataa kwa maandishi, na Chadema walipokubali kuhojiwa, naamini wamewaandikia polisi kuwa sasa wako tayari kuhojiwa, maana Kamanda Sirro, amesema juzi wamesikia, kuwa Lissu yuko tayari kuhojiwa, sijui polisi watakuwa wamesikia wapi kuwa sasa Lissu tayari kuhojiwa, maana siku Lissu anatangaza mbele ya waandishi kuwa anafuatiliwa na hadi kutaja number ya gari inayomfuatilia, na kuwa maisha yake yako hatarini, jeshi la polisi, halikusikia, na msemaji wa polisi alisema kuwa jeshi la polisi halina masikio ya kusikia malalamiko yanayotolewa kwenye press conferences, lenyewe linasikia malalamiko yanayoripotiwa kituo cha polisi tuu, hivyo Lissu ilimpasa kuripoti polisi na sio kuripoti kwenye press conference, hivyo hii ya jeshi kusikia Lissu yuko tayari kuhojiwa, bila Lissu kuripoti kituo cha polisi, ni dalili njema kuwa sasa jeshi letu la polisi ni jeshi sikivu, linaweza hata kusikia tuu vitu kwenye media na ku act upon, japo haina maana watu sasa wasiripoti polisi, kuripoti kuko pale pale, ila sasa pia lina masikio ya kusikia vitu kwenye media!.

Jeshi La Polisi Linastahili Pongezi, Kwa Kuwa Jeshi Rafiki Kuliko Polisi Wote Duniani!.
Likitaka Kufanya Mahojiano, Linaomba, Likikataliwa Linasubiri Hadi Liruhusiwe!.

Kumbe siku hizi, polisi wetu wakitaka kufanya uchunguzi wa kijinai, huwa wanaomba kwanza na wanasubiri kwanza ruhusu ya wahusika, ndipo wafanye uchunguzi, shambulizi la Lissu limetokea miezi zaidi ya mitatu imepita bila taarifa zozote za uchunguzi wa tukio hilo, IGP Sirro anasema mwanzo waliwaomba Chadema, wakakataa!, kumbe uchunguzi wa kijinai siku hizi watu wanaombwa kuhojiwa, ukitaa hauhojiwi, hadi ukubali!, lakini sasa Chadema wamesema wako tayari, hivyo ndio sasa watu wametumwa kwenda kuhoji!. Bahati nzuri sana Lissu na Dereva wake wana photographic memory za gigabitea au telebites kabisa, kukumbuka kila kitu miezi mitatu baadaye!, hawa ndio polisi wetu!.

Hongera Sana Jeshi Letu la Polisi.
Inawezekana polisi wetu ndio the most friendly police force dunia nzima!. Uhalifu ufanyike, tena jinai ya kutishia maisha ya mtu, Tanzania na Kenye tuna mkataba wa ushirikiano kwenye uhalifu, polisi wetu walishindwa nini kumhoji dereva wa Lissu huko huko Nairobi siku zote hizi?!, kumbe walikuwa wanasubiri ruhusa ya Chadema!. Big up sana kwa polisi wetu.

Hitimisho.
Kama ambavyo huwa tunawalaumu polisi kwa mabaya, yakitokea mazuri kwa polisi wetu, tuwapongeze.

Paskali
Rejea za maandiko yangu kuhusu Polisi
TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II!
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Mkuu paskali..endelea kukazana..kuna nafasi mbili za wakurugenzi zipo wazi..BUKOBA DC and BUKOBA MC
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom