Aug 12, 2021
64
117
Kimsingi kuna kitu hakifahamiki vizuri kwa wananchi, vyombo vya usalama nacho ni neno UGAIDI na kama wanakifahamu vizuri basi wanapotosha purposely.

Neno ugaidi lina maana ya Tishio, au kitendo kinacholenga kutisha watu kwa malengo ya kisiasa, kijamii, na kiusalama, hii ndio maana halisi inayofahamika katika vyombo vikubwa vya kiusalama hivyo ile definition ya kwenye somo la General studies haina mashiko ni brainwshing.

Hivyo basi tukio lolote lile ili lihesabiwe kuwa ni ugaidi lazima liguse angle kama tatu.

Moja:Siasa, ugaidi wa kisiaa hulenga kuinfluence malengo ya kundi fulani dhidi ya mamlaka inayotawala ili kubargain state authorities ili kupata sehemu au hadhi fulani katika serikali., Hivyo tukisema kuwa tukio.la salender ni UGAIDI tujiulize kuwa je jamaa huyo alikuwa na lengo la.kuitisha serikali ili apate naye mamlaka au ushawishi au apewe heshima na nafasi ya kisaisa katika serikali?

Bila shaka HAPANA, hivyo kisiasa tukio la jana siyo kigaidi.

Pili:Angle ya tatu ni Jamii, ili tukio liwe ni ugaidi ni lazima liwe na mlengo wa kuitisha hadhira/majorities ya watu ili kundi hilo au mtu huyo apate nguvu au aeneze nguvu zake kwa jamii hiyo ili kuitetelesha dola mfano kuua raia, kulipua masoko, minada, kujitolea muhanga katika vyombo vya usafiri., hivyo tukisema kuwa tukio la jana ni ugaidi tujiulize je aliilenga jamii ya watanzania?

Bila shaka No kwa sababu hakushambulia raia licha ya kuwa raia walikuwepo wengi na uwezo wa kufanya lolotebalikuwa nao., hivyo kwa kigezo hiki pia tukio la jana sio ugaidi.

Tatu, Ili tukio liwe la kigaidi ni lazima liguse angle ya Usalama(Security) kwa maana ya kudistabilize usalama wa nchi ili kuleta vurugu, uasi, na jaribio la mapinduzi , hali hii haijatokea salender , hivyo pia mimi sioni dalili ya ugaidi hapo.

Nne, Angle nyingine ni uchumi, ili tukio liwe la kigaidi halina budi kugusa eneo la uchumi wa nchi yoyote, washambuliaji/magaidi ni lazima wawe na lengo la kudistabilize uchumi wa eneo fulani ktk nchi, bara au dunia mfano kufanya piracying yaani uharamia wa majini mfano kuteka meli za mafuta ili kupewa fidia fulani, kuteka migodi mikubwa na maeneo nyeti ya kibiashara na uchumi, hivyo basi tukio la salender halina sifa ya ugaidi ktk mtizamo wa kiuchumi.

Je, nini kilichotokea salander?
Kilichofanyika ni uhalifu (Social crime) hivyo si kila crime ni ugaidi mfano wizi, ubakaji, mauaji ni uhalifu lakini hautaitwa ugaidi until angle nne hizo ziwe zimeguswa vuzuri, mfano nchini marekani tumekuwa tukishuhudia mauaji ya watu kuua kwa kutumia silaha lakini CIA,FBI na serikali hawajawahi kuiambia dunia kuwa ni ugaidi.

Kilichofanyika salender ni uhalifu ambao unabidi kujadiliwa kwa jicho la kiuhalifu siyo kigaidi ili kuepusha TAHARUKI, chuki na uhasama wa kijamii.

Matukio kama lile la jana salender mara nyingi husababishwa na migogoro binafsi waliyo nayo wahusika (personal conflicts), umasiki, psychological problems au pia relationship querrels yaani migigoro ya kimahusiano baina watu wake wa karibu, jamii inayomzunguka.

Katika tukio la jana kulikuwa na mengi ya kujifunza na kuyafahamu lakini Historia ilichelewa kuandika kwa sababu ya uharaka wa mauti kwa kwa mtekelezaji wa tukio kama angalikuwa hai tungepata mengi, lakini pia vifo vya askari navyo vimetunyima mengi ya kujua.

Hivyo tufanye nini?
Tuwatafute watu waliokuwepo/walioshuhudia kwa macho(vusual evidences) tuwahoji wao waliona nini kabla ya risasi hazijaanza kurushwa je mahusiano ya mtekelezaji na police waliokuwepo maeneo yale ni yapi?

Tukibaini hapo tutakuwa tumetegeua kitendawili.

Tanzania ipo salama msiwe na shaka.
 
Ile ilikuwa show kati ya Raia aliyekerwa na matendo ya Police vs Police wenyewe.

Ungekuwa ni ugaidi angeburuza raia kama 100 na ushee ili kushinikiza serikali kutoa majibu kwa takwa lake.

Na baada ya tukio tu kikundi kilichomtuma kingetoa msimamo.

Ila jamaa ana mafunzo mazuri ya kutumia silaha, aliyapata wapi, na kina nani, kwa ajili ya nini hasa majibu ya haya yote wasingemuua wangeshayajua.
 
Ile ilikuwa show kati ya Raia aliyekerwa na matendo ya Police vs Police wenyewe.

Ungekuwa ni ugaidi angeburuza raia kama 100 na ushee ili kushinikiza serikali kutoa majibu kwa takwa lake.

Na baada ya tukio tu kikundi kilichomtuma kingetoa msimamo.

Ila jamaa ana mafunzo mazuri ya kutumia silaha.

Hamza alikuwa anafikisha ujumbe wake kwa walioshupaza shingo na kujiaminisha kuwa kusikia wao ni kama kenge.

Message sent and delivered
 
Yule jamaa ni gaidi, hakuna namna nyingine ya kumuita.

Lile tukio ni la kigaidi hakuna namna ya kupindisha maneno.

Wanaosema eti alikua analipa kisasi kudhulumiwa na polisi, swali linakuja, baada ya kuwaua polisi na akapata ak 47 mbili, kama wabaya wake ni polisi kwa nini hakurudi hatua chache tu pale daraja la salenda kuna kituo cha polisi akapambane nao?

Kama kweli alikua na usongo na polisi, hatua chache kutoka kwake pale alipowaua askari kuna bank ya stanbic kuna polisi, mbona hakuwafuata, ukiachana na hilo, hatua chache pale alipofanya tukio la kwanza kuna ubalozi wa urusi, kuna polisi kwa nini hakuwafuata?

Yeye alikua anafuata nini ubalozi wa ufaransa na akaacha ubalozi wa urusi hatua chache kutoka alipofanyia tukio la kwanza?

Yule ni gaidi na alikua amelenga wafaransa ndio alitaka kwenda kuwamaliza na si vinginevyo.
 
Yule jamaa ni gaidi, hakuna namna nyingine ya kumuita.

Lile tukio ni la kigaidi hakuna namna ya kupindisha maneno.
Ni gaidi kwa hisia za kimtandoa na ile phobia waliyotengenezewa watu wakisikia mtu anatamka maneno ya kiarabu, but sisi wana taaluma wa maswala ya usalama tunaona kuwa siyo terrorism kwa sababu tukio hilo halijagusa maeneo makuu manne ambayo wataalamu wa mambo ya usalama na counter terrorism intelligence wamebainisha.
 
Ile ilikuwa show kati ya Raia aliyekerwa na matendo ya Police vs Police wenyewe.

Ungekuwa ni ugaidi angeburuza raia kama 100 na ushee ili kushinikiza serikali kutoa majibu kwa takwa lake.

Na baada ya tukio tu kikundi kilichomtuma kingetoa msimamo...

Ila jamaa ana mafunzo mazuri ya kutumia silaha...aliyapata wapi, na kina nani, kwa ajili ya nini hasa ...majibu ya haya yote wasingemuua wangeshayajua.
Jamaa inaonekana alikuwa na bifu na polisi na pengine siku nyingi. Huenda kama ilivyo kawaida walishamnyanyasa kwa jambo ambalo hakustahili. Kuna sehemu nimesoma wakasema alikuwa anamiliki pikipiki aliyoipata siku za karibuni. Je, walikuwa wanamsumbua nayo? Au kuna madili alipiga na polisi wakarushana, ukitilia maanani wasomali ni watu wa madili? Nadhani familia yake inaweza kuwa na hint kwani walikuwa wanaishi naye.
 
Kwa hiyo huyu alipanga 25/8 ndio akaoneshe chuki zake kwa polisi wa uniform, hao rai 6 waliojeruhiwa sio kitu cha kutiliwa maanani? Nani anaye jua Misri alikutana na watu wa aina gani?

Kwanini alikuwa mshabiki wa jihad, tunajua jihadist wanahusishwa na ugaidi sehemu mbalimbali duniani?

Nini kilimfanya aende jirani na eneo ambalo lilikumbwa na mashambulio ya kigaidi agust 1998? Ukisema ni kumbukizi ya tukio hilo inakuwa si sawa?

Nani alimfadhili kwenda kusoma Misri kuna ambaye ameshajua hilo. Familia za magaidi hulipwa na wafadhili wa ugaidi kupitia gaidi mwenyewe kwa hiki kipindi kifupi tayari uchunguzi wa yote haya umeshafanyika?

Afichaye ugonjwa/maradhi iko siku isiyojulikana kifo kitamuumbua. Mpaka sasa kimsingi kifo kimeshaumbua na kinachoendelea ni funika kombe tu. Penetration ya Hamza katika ranks za chama imetisha.
 
Jamaa inaonekana alikuwa na bifu na polisi na pengine siku nyingi. Huenda kama ilivyo kawaida walishamnyanyasa kwa jambo ambalo hakustahili. Kuna sehemu nimesoma wakasema alikuwa anamiliki pikipiki aliyoipata siku za karibuni. Je, walikuwa wanamsumbua nayo? Au kuna madili alipiga na polisi wakarushana, ukitilia maanani wasomali ni watu wa madili? Nadhani familia yake inaweza kuwa na hint kwani walikuwa wanaishi naye.
Polisi ni wadhulumati. Unakumbuka enzi za Jiwe walivyomnyang'anya kwa nguvu mgiriki madini mgiriki Jiwe akawasifu
 
Sikufurahishwa ya yule police aliyemuua risasi ya kichwa..ilitakiwa leo awe hai tujue in out...hamza nini ulitaka??

Information ni muhimu saana saana, Police wetu waende mafunzo tena.
wATAzungumza nae hivyo hivyo...na atasema tu...!
 
GAIDI anatetewa kwa nguvu zote sababu yeye ni kada wa Chama
Anayetetewa ni Mbowe ndio ambaye watu wanasema Mbowe hawezi kufanya ugaidi au hawezi kuwa gaidi ila Hamza hatetewi bali watu wanajadili alichokifanya kuwa ni ugaidi ama sio ugaidi. Mleta mada katoa mfano hapo kuwa uhalifu kama wa Hamza hutokea sana tu huko Marekani ila hawajawahi kuita ni ugaidi.

Ila mimi nachokiona hapa tatizo ni imani tu ya Hamza ndio tatizo lenye kufanya aonekane ni gaidi ila kama asingekuwa na hiyo imani basi isingekuwepo hii issue ya kuitwa gaidi.
 
Jamaa inaonekana alikuwa na bifu na polisi na pengine siku nyingi. Huenda kama ilivyo kawaida walishamnyanyasa kwa jambo ambalo hakustahili. Kuna sehemu nimesoma wakasema alikuwa anamiliki pikipiki aliyoipata siku za karibuni. Je, walikuwa wanamsumbua nayo? Au kuna madili alipiga na polisi wakarushana, ukitilia maanani wasomali ni watu wa madili? Nadhani familia yake inaweza kuwa na hint kwani walikuwa wanaishi naye.
Je, Unadhani kuna chochote tutakachoambiwa ambacho kitakua na mtazamo hasi kwa vyombo vya dola?

Hapa chochote kitakachogundulika huko ambacho kitakua against na sifa za nchi kitazikwa. Zaidi vitaletwa vyeti vya mirembe na vipimo kwamba alikua UDI (under drugs influence) na itakua ndo ivyo.
 
Yule jamaa ni gaidi, hakuna namna nyingine ya kumuita.

Lile tukio ni la kigaidi hakuna namna ya kupindisha maneno.

Wanaosema eti alikua analipa kisasi kudhulumiwa na polisi, swali linakuja, baada ya kuwaua polisi na akapata ak 47 mbili, kama wabaya wake ni polisi kwa nini hakurudi hatua chache tu pale daraja la salenda kuna kituo cha polisi akapambane nao?

Kama kweli alikua na usongo na polisi, hatua chache kutoka kwake pale alipowaua askari kuna bank ya stanbic kuna polisi, mbona hakuwafuata, ukiachana na hilo, hatua chache pale alipofanya tukio la kwanza kuna ubalozi wa urusi, kuna polisi kwa nini hakuwafuata?

Yeye alikua anafuata nini ubalozi wa ufaransa na akaacha ubalozi wa urusi hatua chache kutoka alipofanyia tukio la kwanza?

Yule ni gaidi na alikua amelenga wafaransa ndio alitaka kwenda kuwamaliza na si vinginevyo.
Usipendelee kuandika sana ukiwa umelewa. Afadhali kulala kisha ukiamka uandike ukiwa na akili zako nzuri.
 
Back
Top Bottom