Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,569
- 93,236
Nimemsikiliza CAG Ikulu Dodoma wakati wa kuwasilisha report yake Kwa Rais nimeshtuka sana.
Moja ya sababu alizozitaja za NHIF kupata hasara ni wastaafu kutibiwa bila kuchangia.
Sasa swali langu Kwa CAG anaelewa kweli maana ya mstaafu? Hii nchi yetu ina laana gani? Ni Kwa nini watu wakiwa kwenye maofisi hawafikirii maisha ya wastaafu?
Tanzania kamwe Mungu hawezi kuibariki kama itaendelea kutowathamini wazee.
Hawa watu ni wa kukemewa vikali, madhara ya kuwakalia kimya watakuja na Sera ya wazee kuchangia matibabu Kwa kisingizio wanaitia hasara NHIF wakati ujana wao wote wametumika serikalini na sasa wamejichokea nyumbani CAG anataka wanyang'anywe hata haki ya matibabu, hii ni roho mbaya na ubinafsi uliopitiliza.
Tuseme Kwa Sauti Kwa hili hapana mnatafuta laana.
Wajifunze nchi za ulaya na Marekani serikali zao zinatowa ajira kabisa Kwa watu wa kulea wazee Sisi Tanzania tunataka kuwauwa kabla ya siku zako, tulikatae wazo ovu la CAG.