Sahar
Senior Member
- Jul 15, 2012
- 184
- 83
Kuna binti nilimtamkia dhamira yangu ya kuwa nae kimapenzi.......... Lakini majibu yake yakawa hawezi kuwa na mimi kwa sababu ana mtu mwingine tayari..... Sikutaka kumsumbua sana, hivyo yakabaki mawasiliano ya kawaida tu. Hata hivyo kinachonishangaza ni pale ninapokuwa nimepata safari na akajua kwamba nimesafir bila kumpa taarifa, basi atalalamika huyo, anajinunisha mpaka nimuombe msamaha ndio yana isha!!! Baada ya kuona hivyo juzi nikamkumbusha tena dhamira yangu, jibu alilonipa ni kwamba hayuko tayari kuingia mapenzini!!! Sasa swali ni kwanini anapenda kujihusisha sana na mambo yanayonihusu as if mie ni hubby ake!???