Sijajiuzulu uongozi CHADEMA-Prof.Baregu

Sijajiuzulu uongozi CHADEMA-Prof.Baregu

Mods mtela mwampamba apigwe ban,kwa kutoa taarifa za uongo.

Hili toto hata wakati ule Arusha lilileta uzushi mbaya sana nakumbuka likapewa kifungo sasa karudia tena. Kijana mdogo kuwa mwongo na mzushi ni aibu sana halafu unajiita mwanasiasa? Eti huyu ndio wajamaa wanajivunia kuwa wamepata kijana hodari? Hawajiulizi nini kilimfukuzisha Chadema? Mods fungia hii mbulula iliyosababisha watu wanapoteza muda kujadili uongo wake,pia kamvunjia heshima Pro Baregu maana kuna watu wamemtusi bure.
 
Mtasema sana nyie magambazi but chadema ni kama maji usipoyaoga utayanywa tu.kama unabisha jaribu uone kwetu cdm hatumwogopi mtu hata kama anaumbo kama tembo atang'oka tu.
 
safi sana kamanda baregu kwani arfi kishajionyesha yeye ndiye m2 natamani aachie na ubunge hapo ndo ndamwona kwel imemuuma chadema moto mdundo up two 2015
 
Juzi juzi SLAA alisema ZITTO hana shida bali ni watu wanawachonganisha, leo wamemnyang'anya madara, siasa bwana.

Halafu unaambiwa mwenye ndimi mbili ni huyo aliyefukuzwa!!!!!!!

Wapenzi wa vyama kazi wanayo asee
 
Mods ikithibitika aliyeleta uzi apewe LIFE BAN pamoja na kwamba ana ID nyingine atakayoendelea kuitumia

Kweli kabisa Mkui.
The same guy aliletaga thread ya Mgombea udiwani CHADEMA kurudi CCM few daus before hawajarusha bomu na 4 bila..akapewa bun ya mwezi mmoja.
Cc Invisible
 
Last edited by a moderator:
ile thread ya prof kujitoa wana cdm walimponda hana mchango.....sasa imekuja hii wanahaha,mmh siasa fuata upepo haitakiwi,katiba ipitishe ugombea binafsi bila chama ss.
 
Prof Baregu naye ajiuzulu nyazifa zake ndani ya chama baadaya kamati kuu kuwavua nyazifa zao akina Zitto na wenzake.
 
TUNATARAJIA ADHABU KALI SANA KUTOKA JF kumwangukia yule mtengeza UZUSHI ULE AMBAYE ANAONEKANA BADO ANAENDELEA KUCHANGIA .
 
hata mimi nilikuwa nashaanga sana, Ila la makanu Mwenyekiti, nadhani akina mwampamba walikuwa wanatembea na hiyo balue kwenye flash zao

Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Prof. Mwesiga Baregu amekanusha vikali taarifa za kujiuzulu nafasi za uongozi ndani ya CHADEMA zilizozagaa kwenye mitandao, asema hana mpango wa kufanya hivyo.

Professa Baregu amesema uvumi huo unaenezwa na CCM na vibaraka wake na kuendelea kusisitiza kwamba Chadema itaendelea kuwa moja na Imara zaidi.

Source:Mwananchi Breaking News
 
Waswahili hawana shida ya kumalizia msemo huo.

Ni furaha kubwa sana kwa wale ambao siku zote humu JF tumeshambuliwa kwa kuitwa wadini eti kwa kuwa tu tunaanika ukweli na hatukusita kukemea udini na ukanda wa dhahiri unaooneshwa na viongozi, wanachama, mashabiki, wanazi na bila kuwasahau misukule wa magwanda.

Furaha ilioje kubainika ukweli kuwa chadema ni chama kinachoongozwa kibaguzi. Ubaguzi wa ukabila na udini umejionesha wazi wazi kwa yanayojiri sasa hivi.

Dhambi hiyo ndiyo inawakaanga leo chadema.

Si mimi, waliotangaza kuachia ngazi bila kufukuzwa wamesema hayo.

Poleni sana wale walioipenda chadema kwa dhati na kufikiri kuwa ingewaletea mabadiliko. Leo naona simanzi na huzuni imewashika, hamtaki kuamini ukweli, lakini huo ndio ukweli.

Jee, M2 siyo Mohamedi Mtoi?

...Furaha ya mvuvi.
 
Mkuu Molemo, asante kwa taarifa. Prof. Beregu, kwa maoni yangu, ndio the only wise ndani ya CC ya Chadema akifuatiwa na JJ.Mnyika!. Ni mtu mwenye msimamo usioyumba na asiyekubali kupelekwa pelekwa kwa kutanguliza maslahi ya taidfa mbele ndipo nyuma chama kifuate, pale alipolazimishwa kujitoa kwenye Tume ya Katiba!, akawagomea kata kata hao "vichwa panzi" ambao kiukweli, mwanzo walikuwa na "uwezo" na "tuliwatumainia sana", ila sijui ni nini kimewapata!, uwezo wao unashuka kuelekea sifuri, zero, ila bado "watu" wanawatumainia", na ndio "wanawategemea" kwa 2015!.

Lets wait and see!.
Pasco.
 
CCM is completely frustrated......... wanatafuta gogo la kufa nalo.....!
 
Hasira za Mkizi...

Back
Top Bottom