Sifahamu mimi ni nani

Sifahamu mimi ni nani

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Tell them, green piggies are here to stay, they ain't going nowhere!

- KANA -
Not for long though the angry birds have finally seen them piggues' true color revenge is on the way.

Sent from my E5306 using JamiiForums mobile app
 
Usisumbuke kutaka kuivuruga familia, Karibu kwenye mabanda yetu sabasaba ujipatie dawa ya kumvuta alie mbali. Karibu sana na majaribio yatafanyika. Nikuhakikishie huyo mzee msepa familia atakuja mwenyewe kama kuku aliemwagiwa mchele.
 
Nilipokusoma mwanzo na baada ya kusoma comments nyingi humu, kidogo na mimi nikwambie achana na mawazo ya huyo baba, ila baada ya kukusoma in deep na kusoma comments za baadhi ya watu naona kuna umuhimu wa wewe kumjua huyo baba hata kama hayuko hai basi hata ndugu zake au ukoo wake, mana hata ukisema uachanane na hilo la kumjua baba yako, utabakia na maswali mengi na ninge nisinge nyiiingi kiasi kwamba naona u will never have a peace of mind or even find real happiness, my advice find him, na ikibidi jaribu hata kumwambia huyo mzee aliekulea kwamba u need to find you biological father ili atleast uweze kupata amani na labda majibu ya maswali unayojiuliza concerning hali ya maisha na tabia na mambo mengine ambayo unahisi labda kumjua baba yako kutaleta ufumbuzi kwako na kwa kaka yako, na hata kama hutapata majibu or wherever basi angalau utapata amani
Asante, I'm working on it, hope I'll find what I'm looking for

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wengi wana elimi ila hawajaelimika. They have education but they are not educated
I thought knowing oneself is part of what you're talking about (education) but i don't blame anyone concerning what they have to offer as an advice/comment by the way education is a wide concept, so i don't know how you define education from your perspective but when it comes to me incase if I'm to be asked i would say Education is what triggered the need to find out the truth.. Trust me kama sio shule nisingekua na sababu ya kuutafuta ukweli ulio jificha

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu pole sana ndo ukubwa huo. Mama kameza pini. Ila time will tell kuwa na subra kama ulivyojua haya utajua na mengine zaidi

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Kama hakuna kasoro iliyojitokeza kwa watoto sidhani kama kuna haja ya kushughulika na mambo yaliyopita. Shida nyingine ni namna jamaa anavyotaka kushughulikia hili suala
That's is why I'm after your advice not criticism, if i knew how to sort things out by myself i would not bring my nose is this forum, so i would appreciate your advice on this one. Period

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Hujafatilia mtililiko wa comments huyo babu/bibi hana details zozote za huyo mtu zaid ya alichomwambia

Kuhusu wapi hata pata details nilishasema huko juu awatafute hata marafiki wa mamake wale best friends huenda kuna kitu wanachojua

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app
Asante rafiki atleast i know where and how to start

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Dogo acha ujinga wewe kama ukoo ungekukataa ungesha kufa sasa unatafuta laana na Si kingine tulia andaa maisha yasonge wapo walotumia ukoo wa mama yeye na vikukuu ulisikia wamekufa ?

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Kiongozi nimekuelewa. Nawatakia kila la kheri katika harakati za ufukuzi wa makaburi.

My take: sishauri katika hili. Atahangaika atakuja kushtuka muda na nguvu zimeshapotea
Samahani brother kufukua makaburi maana yako ni ipi hasa? I mean how is it related with digging graves

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Huyu jamaa anataka kuleta issue zake za kidizaini, nikuhakikishie hiyo fadhila/heshima aliyoipata huyo dada kwenye familia yenu huyu jamaa asitegemee kwa mjeda coz alishatimiza wajibu wa kumfikisha jamaa alipofika. Hivyo kama analeta jeuri ataishia kunyea kambi, Tangu lini baba aliesepa akamkubali mwanae?
Nanyeaje kambi bhana?? Despite of being Independent( self sufficient) i still respect the oldman and it is going to be that way forever, i don't mean to blow the whistle what I'm doing is just searching for the truth as a person without involving any of my relatives sasa hiyo ishu ya kunyea kambi imekaaje?

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nasisitiza kwa uchumi wetu wa viwanda hatuna muda wa kuhangaika na haya mambo, kwanza hajatuambia alisoma nini chuo tumpangie majukumu kuendana na Mpango wetu wa Maendeleo. Hakuna blabla hapa. Kazi tuu....
Unipangie Majukumu !!! Okay i pursued Banking & Finance and i work with TPDF
what's the plan??

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Usisumbuke kutaka kuivuruga familia, Karibu kwenye mabanda yetu sabasaba ujipatie dawa ya kumvuta alie mbali. Karibu sana na majaribio yatafanyika. Nikuhakikishie huyo mzee msepa familia atakuja mwenyewe kama kuku aliemwagiwa mchele.
I hope you're serious!

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu pole sana ndo ukubwa huo. Mama kameza pini. Ila time will tell kuwa na subra kama ulivyojua haya utajua na mengine zaidi

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
Asante THT

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Dogo acha ujinga wewe kama ukoo ungekukataa ungesha kufa sasa unatafuta laana na Si kingine tulia andaa maisha yasonge wapo walotumia ukoo wa mama yeye na vikukuu ulisikia wamekufa ?

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
Sijafahamu hao waliotumia majina ya koo za mama yao, hivyo siwezi jua kama walikufa, sounds Odd

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Habari za leo wana forum,

Mimi ni kijana at late 20's toka nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 90 nilikuwa nafahamu kuwa baba na mama yangu ndio hawa waliokua wakinilea lakini mwaka 2015 wakati nimemaliza chuo na kurudi nyumbani niliipata taarifa ambayo ilibadili mtazamo wangu kuhusu hawa wazazi wangu na siri kubwa waliyo nayo.

Iko hivi kwa mama yetu mzazi tuko watoto wa nne, mimi ni wa pili kuzaliwa kuna wa kwanza wa kiume na wadogo zetu wawili wa kike na kiume ambao sina shaka juu ya uhalisia wao kwa kua wamezaliwa nikiwa na akili timamu.

Baba yetu tunae mfahamu ni askari wa jeshi la wananchi na mama yetu kipindi hicho alikua ni mwalimu wa shule ya msingi. Kusema ukweli mzee huyu ametulea ki- dictator mpaka inafikia stage unamuogopa and you cannot make story with him or express yourself to him as your father lakini tukazoea na kuona labda tunalelewa kijeshi and by then we lived in a military Barack.

But the good thing about the oldman ni kwamba amekuwa na moyo wa kujitolea kuhusu maisha yetu like taking us all to the most expensive school in town and supplying all our basic needs abundantly, inshort he is Generous nadhani hii ndio sababu iliyotuaminisha kua he is our biological father kwa kua mpaka ada ya kulipia chuo kikuu amenilipia bila kua na mkopo kutoka HESLB.

Sasa wakati nimemaliza chuo nilirudi kijijini kumsalimia bibi (mama wa mama) huko nilikutana na mzee mmoja ambae alinitambua kwa jina la asili ambalo sikuwahi kulijua kabla nilishangazwa na lile jina nikaamua kumuuliza yule babu vipi mbona tunaitana majina ya ajabu.

Mzee akaniuliza kwani wewe unaitwa nani nikamtajia jina langu kwa kudhani kua amenifananisha, akasema "nakufahamu tokea ukiwa mtoto wa umri wa siku moja" yaani kabla mama yetu hajaolewa na huyu mzee tunaemuita baba, honestly he ruined my day and i almost slapped him on his face but thank God i managed to conceal my true feelings.

Nikamwambia mzee kabla sijaondoka nitakuja nikuone tuongee vizuri. Hata sikutamani tena kukaa kwa yule bibi yetu muda wote nilikua nafikiria maneno ya yule mzee baada ya siku 3 niliamua nimuage bibi and i went straight to the oldman's house.

Yule mzee alinieleza kwa masharti kua nimekua mtu mzima nahitaji kujitambua mimi ni nani, na asingeweza kuniambia hizo taarifa wakati wa kipindi cha nyuma labda nisingeweza kumuheshimu huyu mzee wetu ukizingatia anatusaidia kwa mambo makubwa ambayo mama yetu as a single parent asingeweza ku afford like taking us all to international schools.

Nikamuuliza mzee vipi kuhusu hili jina ninalotumia? Akanieleza kua baba yetu (sisi watoto wawili wa kwanza) alikuwa ni dereva wa magari makubwa alikua akija pale nyumbani kwa msimu na hakua akituhudumia.

Sasa huyu askari alipohamishiwa kwenye mji ule kikazi ndipo akakutana na mama yetu akiwa na watoto wawili (mimi na kaka yangu) akafanya kutu adopt na kutubadilishia majina yetu na kuanza kutumia majina ya ukoo wake, kuna muda baba yetu alikuja pale nyumbani alipata kichapo akaenda mahakamani akashindwa kesi kua hana mchango kwa familia kwa hiyo akatoweka mpaka Leo, mimi mpaka sasa hivi sijijui kua ni nani.

Nikimaanisha kabila wala ukoo, ndugu zangu wote hawajagundua hili and we all live like brothers, namuheshimu sana huyu mzee na amefanya kila kitu kuhakikisha tunasoma ili tujitegemee kiasi kwamba nilivyomaliza tu chuo akanitafutia nafasi jeshini moja kwa moja and to be honest I was just glad.

Naomba mnishauri hapa kwa kua niliamua kumkabili mama anieleze ukweli kwa njia ya kumdadisi kwa kua sifanani na mama wala na baba huyu tofauti na wadogo zetu. Lakini mama amekua mkali kua namkosea heshima maswali hayo ni ya kumvua nguo na nimekosa nini kwa baba huyu mpaka kuulizia mtu nisiye mfahamu wala asiyenisaidia lolote.

Yuko sahihi lakini mimi natumia majina ya kichaga ambayo kiuhalisia nimepewa tu hayana mahusiano na mizizi yangu mie and what disturbs me the most ni wanangu, hawa wanangu watakua kabila gani? Si nitakua nimewapa kabila ambalo sio lao? Na wajukuu zangu pia?

Naombeni ushauri this is killing me inside whenever it comes to my mind because I'M A STRANGER TO MYSELF

Regards

Pharaoh_2
Achana na habari ya kutafuta baba hewa na makabila yasiyowajibika kwa familia. Baba wa kichagga aliku.adopt completely, that means hata wanao ni wachagga. Kama unaona huyo Mzee wa Kichagga aliwakosea, basi ww na kaka yako mkapimwe akili muungane na baba yenu mzazi aliyekula kichapo kwa kutojali familia.
 
Jina halina uhusiano na wewe hata kama ungeitwa kisu hamna ambae angepinga na undugu ni kusaidia na sio kufanana nilichokibaini kutoka kwako ni kadiri ulivyokisoma ndivyo ulivyokipingua akiri umefundishwa miaka yote kwa maneno na matendo kwamba huyu babayako na huyu mama yako wakakughalamia kwa juhudi na maalifa kisha anakuja mjonga mmoja tu kuvunjwa elimu uliyofundishwa na wepenzi wako wanaokutakia mema tena kwa dakika 5 nawe kwa ujinga wako unafuta yooote na kuanza kuomba ushauri kwa jambo la kipumbavu. Umenichukiza sana lau kama mimi ndie ningekua mama yako na adabu hiyo unayonivunjia kwa kuwa tu eti umepata kazi sasa na unajifanya unajitambua ningekuazibu azabu ambayo dunia ingejifunza kitu kutokana na ujinga wako.

Sent from my SM-G930V using JamiiForums mobile app
 
Unachokitafuta kiko sahihi kabisa ni vizuri ujifahami hata kama huyo mzee hakukulea wewe ulikuwa mtoto huwezi kuelewa Mambo ya nyuma kwani kujua ukweli kuna ubaya gani je kama huyo mazazi wako alikuwa fukara utajuaje tuache kupotosha ukweli huyo mazazi anachokificha ni nini Hizo chuki zake na huyo mazazi wako asikujumlishie na wewe busara ni vizuri Zaidi ikatumika kuliko kukukatili usijue ukweli

Sent from my TECNO R7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom