Habari za leo wana forum,
Mimi ni kijana at late 20's toka nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 90 nilikuwa nafahamu kuwa baba na mama yangu ndio hawa waliokua wakinilea lakini mwaka 2015 wakati nimemaliza chuo na kurudi nyumbani niliipata taarifa ambayo ilibadili mtazamo wangu kuhusu hawa wazazi wangu na siri kubwa waliyo nayo.
Iko hivi kwa mama yetu mzazi tuko watoto wa nne, mimi ni wa pili kuzaliwa kuna wa kwanza wa kiume na wadogo zetu wawili wa kike na kiume ambao sina shaka juu ya uhalisia wao kwa kua wamezaliwa nikiwa na akili timamu.
Baba yetu tunae mfahamu ni askari wa jeshi la wananchi na mama yetu kipindi hicho alikua ni mwalimu wa shule ya msingi. Kusema ukweli mzee huyu ametulea ki- dictator mpaka inafikia stage unamuogopa and you cannot make story with him or express yourself to him as your father lakini tukazoea na kuona labda tunalelewa kijeshi and by then we lived in a military Barack.
But the good thing about the oldman ni kwamba amekuwa na moyo wa kujitolea kuhusu maisha yetu like taking us all to the most expensive school in town and supplying all our basic needs abundantly, inshort he is Generous nadhani hii ndio sababu iliyotuaminisha kua he is our biological father kwa kua mpaka ada ya kulipia chuo kikuu amenilipia bila kua na mkopo kutoka HESLB.
Sasa wakati nimemaliza chuo nilirudi kijijini kumsalimia bibi (mama wa mama) huko nilikutana na mzee mmoja ambae alinitambua kwa jina la asili ambalo sikuwahi kulijua kabla nilishangazwa na lile jina nikaamua kumuuliza yule babu vipi mbona tunaitana majina ya ajabu.
Mzee akaniuliza kwani wewe unaitwa nani nikamtajia jina langu kwa kudhani kua amenifananisha, akasema "nakufahamu tokea ukiwa mtoto wa umri wa siku moja" yaani kabla mama yetu hajaolewa na huyu mzee tunaemuita baba, honestly he ruined my day and i almost slapped him on his face but thank God i managed to conceal my true feelings.
Nikamwambia mzee kabla sijaondoka nitakuja nikuone tuongee vizuri. Hata sikutamani tena kukaa kwa yule bibi yetu muda wote nilikua nafikiria maneno ya yule mzee baada ya siku 3 niliamua nimuage bibi and i went straight to the oldman's house.
Yule mzee alinieleza kwa masharti kua nimekua mtu mzima nahitaji kujitambua mimi ni nani, na asingeweza kuniambia hizo taarifa wakati wa kipindi cha nyuma labda nisingeweza kumuheshimu huyu mzee wetu ukizingatia anatusaidia kwa mambo makubwa ambayo mama yetu as a single parent asingeweza ku afford like taking us all to international schools.
Nikamuuliza mzee vipi kuhusu hili jina ninalotumia? Akanieleza kua baba yetu (sisi watoto wawili wa kwanza) alikuwa ni dereva wa magari makubwa alikua akija pale nyumbani kwa msimu na hakua akituhudumia.
Sasa huyu askari alipohamishiwa kwenye mji ule kikazi ndipo akakutana na mama yetu akiwa na watoto wawili (mimi na kaka yangu) akafanya kutu adopt na kutubadilishia majina yetu na kuanza kutumia majina ya ukoo wake, kuna muda baba yetu alikuja pale nyumbani alipata kichapo akaenda mahakamani akashindwa kesi kua hana mchango kwa familia kwa hiyo akatoweka mpaka Leo, mimi mpaka sasa hivi sijijui kua ni nani.
Nikimaanisha kabila wala ukoo, ndugu zangu wote hawajagundua hili and we all live like brothers, namuheshimu sana huyu mzee na amefanya kila kitu kuhakikisha tunasoma ili tujitegemee kiasi kwamba nilivyomaliza tu chuo akanitafutia nafasi jeshini moja kwa moja and to be honest I was just glad.
Naomba mnishauri hapa kwa kua niliamua kumkabili mama anieleze ukweli kwa njia ya kumdadisi kwa kua sifanani na mama wala na baba huyu tofauti na wadogo zetu. Lakini mama amekua mkali kua namkosea heshima maswali hayo ni ya kumvua nguo na nimekosa nini kwa baba huyu mpaka kuulizia mtu nisiye mfahamu wala asiyenisaidia lolote.
Yuko sahihi lakini mimi natumia majina ya kichaga ambayo kiuhalisia nimepewa tu hayana mahusiano na mizizi yangu mie and what disturbs me the most ni wanangu, hawa wanangu watakua kabila gani? Si nitakua nimewapa kabila ambalo sio lao? Na wajukuu zangu pia?
Naombeni ushauri this is killing me inside whenever it comes to my mind because I'M A STRANGER TO MYSELF
Umejichanganya vibaya ungeenda au kuwatafuta Wale mashosti wa maza wa zaman pale pale kijijin tena ungesaidiwa na huyo mzee. Ila tahadhar nakupa hata ukimkuta huyo baba halis ucfanye jambo lolote litalomuumiza baba mlez ni laana kubwa utachukua. Kulelea mtoto mpaka atoke huko mtu c kaz rahc mpe heshima yake. Na unawaza kumletea Mother matatizo kwa mumewe.
Regards
Pharaoh_2