Mkuu Pharaoh_2 usirudi nyuma katika kumtafuta baba yako halisi ,ukweli utakuweka huru.
Nimesoma kwa makini karibia kila ushauri uliotolewa kwako. Wengi wanaosema usimtafute wanatoa sababu kuwa hakukutunza. Hii siioni kama ni sababu ya msingi kwa kuwa katika Uzi wako umetuambia baba yako (mzazi/halali) alijaribu kuwatafuta lakini akaishia kupigwa na kesi juu. Pengine hata kesi hii alishindwa kutokana na social status au rushwa alafu leo hii watu wanakushauri usimtafute babaako mzazi ambaye alipigana kukupata akishindwa nguvu!!!
Watu wengi wa dunia ya sasa wamekuwa very materialistic kiasi kwamba wanajali pesa na mali kuliko utu.
Bwana Pharaoh_2 usiache kumtafuta baba yako. Kwenye ulimwengu wa kiroho kuna mambo mengi yanaweza kukutatiza wewe mwenyewe au kizazi chako kama hutamjua baba yako. Madhara ya kiroho yanayoweza kutokea ni pamoja na watoto wa familia moja kuoana na matokeo yake mara nyingi huwa hasi.
Ni mtazamo tu.