1. Naomba ku-subscribe kwenye hii thread. Usiache kuja kutupa mrejesho mkuu
2. Mara nyingi tunapoomba msaada tunakuwa tayari tuna upande wa majibu ambao tunautamani kuusikia. Inapotokea mtu akakujibu tofauti na matarajio yako ni rahisi kukasirika na kuanza kujibu vibaya (hata kama yeye ndiyo kaanza kukutukana).
3. Mwisho wa yote, maamuzi ya mwisho utayafanya wewe na yatakayojiri utayabeba mwenyewe. Hivyo chukua shauri zote kisha ziweke kwenye mizani. Yaani kwa sasa, chukulia kama pande zote mbili ziko sahihi. ondoa jibu ulilonalo kichwani. Tafakari kwa kupima.
4. Baada ya kusoma mabishano ya comments kadhaa ninachelea kutoa maoni yangu ila nikusihi uwe na msimamo wa peke yako. Sikiliza ushauri (hata matusi na maudhi) kisha fanya maamuzi yako binafsi. Muombe sana Mungu (kuna nyakati nimeshindwa kujua kama unaamini mizimu au la) lakini nikusihi kuomba sana juu ya hili. Maadamu ni box lililokwisha kufunguliwa ni ngumu sana kulifunga bila kutaka kujua kilichopo ndani. Kuna nyakati ni baraka na kuna nyakati ni heri kutochungulia..again, unahitaji tafakuri sana.
5. Usipunguze heshima yako kwa baba yako. Umeshajua ukweli, huwezi kuufukia na kujifanya huujui. Usiache kumheshimu na kuendelea kumuita 'baba' hata kama utaamua baadaye kumtafuta na hata ukimpata huyo mwingine.
6. WADADA: Mimi ninalia na dada zangu..mnaona yanayotokea kwa huyu? Basi iwe funzo kwenu. Tutapiga kelele kuwasema vijana wasiojali watoto wao lakini ni vyema mtambue, mwisho wa yote mzigo mkubwa unatua kwenu. Kwenye suala la mimba aisee, jukumu kubwa ni lenu. BE VERY WISE.
Salaam.