SIASA ZA VITA: Imeanza kuzungumzwa kwa dhati kama hapo kabla Marekani haijatumia bomu la nyuklia, kuwa inaepusha mauaji zaidi kwa kutumia nyuklia!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Baada ya mamilioni ya watu zaidi ya 30,000,000 kufa katika nchi mbalimbali kutokana na vita kuu ya pili ya dunia, washauri wa mambo ya vita wa marekani walimshauri raisFranklin Delano Roosevelt wa wakati huo kuwa, ili kumaliza vita hivyo, inabidi aidhinishe matumizi ya bomu la nyuklia (wakati huo liloijulikana kama bomu la atomiki/atomic bomb. Wakati huo Marekani ilikuwa imeshindwa kuilazimisha Japan isalimu amri kwa kutumia nguvu za kivita. Hivyo ikaonekana mamilioni ya raia na askari wa pande zote zinazopigana wataendelea kufa. Lakini kama Marekani itaamua kutumia bomu la atomiki, pamoja na kwamba watakufa watu wengi, lakini bila shaka Japan itasalimu amri na kupelekea vita kukoma na hivyo kuzuia mauaji zaidi kuendelea. Ushauri huo ulikubalika na Marekani ikaipiga Japan na kwa kutumia mabomu ya nyuklia mara mbili. Walipopigwa mara ya kwanza Japan haikusalimu amri. Lakini ilipopigwa mara ya pili Japan ilinyoosha mikono na huo ukawa ndio mwisho wa vita kuu ya pili na mauaji yakakoma.

Kabla ya mabomu hayo ya nyuklia zaidi ya watu milioni 30 walikuwa waqmekufa. Mabomu hayo mawili ya nyuklia yaliua watu 355,000 hapo hapo mbali na wale waliokufa baadaye. Mpaka leo watu wanaamini kuwa kama si Marekani kutumia bomu la nyuklia, vita vingeendelea kwa miaka mingi zaidi na mamilioni wengi zaidi wangekufa! Kwa hiyo bomu hilo linasifika kwa kuepusha mauaji zaidi.

Hoja hiyo hiyo imeanza kuzungumzwa kwa dhati na washauri wa mambo ya vita wa Urusi kuwa, ili kuepusha mauaji zaidi ni lazima kuilazimisha Ukraine kusalimu amri kwa kutumia mabomu ya nyuklia!!!! Kwa sasa hakuna dalili za ukraine kusalimu amri kwa sababu inategemea misaada ya kivita kwa maana ya zana za kivita na pesa toka nchi za magharibi hususan Marekani na Uingereza. Kuna dalili zote kuwa usjhauri huo umeshakubalika kwa vioingozi wengi wa Urusi kasoro tu rais Putin bado anasita, japo kuna dalili kubwa kuwa ameshaanza kushawishika, ndio maana amekubali kupeleka silaha hizo pia nchi jirani rafiki. Kwa hali ya mambo jinsi ilivyo tusishangae kuamka na kukuta mji mzima wa Kiev umeteketea na maelfu ya watu kufa hapo hapo!!

Swali lililopo ni kuwa je Urusi ikamua kumaliza vita kwa mtindo huo, ni nani alaumuwe? Je ni urusi ilaumiwe? au je ni Marekani na NATO walaumiwe kwa kumtumia Ukraine kupigana na Urusi huku wakiizuia ukraine kufanya mazungumzo na urusi? au je ilaumiwe Ukraine kwa kukubali kutumiwa na Marekani ili ipigane na Urusi!! Watu wanasema, unapoamua kupigana na Taifa lenye silaha za nyuklia unategemea nini? Hata Marekani haiwezi kuthubutu kushambulia Taifa lenye silaha za nyuklia kama Korea ya kaskazini! Ilikuwaje Ukraine kukubali8 kutumiwa na NATO kupigana na Urusi? Je ikipigwa bomu la nyuklia itashangaa?

Sergey Karaganov: By using its nuclear weapons, Russia could save humanity from a global catastrophe​

A tough but necessary decision would likely force the West to back off, enabling an earlier end to the Ukraine crisis and preventing it from expanding to other states
 
URUSI WA BUZA UNAKUSUMBUA DUNIA YA SASA SIO ILE YA 1945, MWAMBIE HUYO MWEHU WENU APIGE HILO BOMU AFU AONE MOTO WAKE
 
Wanasema mkaidi hafaidi hadi siku ya idi.

Hata mtoto mtukutu, kama anapewa adhabu hataki kuacha utukutu basi kuna siku anapewa kibano kikali na cha haja, akitoka hapo anasema mwenyewe 'NIMEKOMA'
 
Back
Top Bottom