The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,464
- 17,303
Baada ya mgogoro wa kivita wa Ukraine kuanza, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Bwana Sergey Lavrov alitahadharisha kuhusu matumizi ya Nyuklia na kusema Urusi haitasita kutumia silaha za nyuklia pale itakapobidi.
Sasa naanza kuelewa kwamba ile ilikua ni defense mechanism ili kuficha udhaifu wa Urusi kwenye silaha.
Nimesema hayo kwa sababu zifuatazo.
Moja, Mwaka 2018 wakati Urusi wakifanya sherehe ya kuushinda unazi na sherehe hizo huambatana na maonyesho ya silaha mpya, Putin alitangaza silaha mpya za kisupasonic (supersonic missiles) zinazoitwa Kinzhal missiles na kusema hakuna mfumo wowote wa ulinzi Duniani wa kuzizuia, na kusema kwamba Urusi hua hatua 10 mbele kwenye uzinduzi wa technolojia mpya ya silaha kabla ya wapinzani wao, akimaanisha Marekani.
Mwaka jana mwezi wa 8, waziri wa ulinzi na Urusi Bwana Surgey Shoigu pamoja na watengenezaji wa silaha za kinzhal walisema hizo silaha hazina mfumo wa ulinzi Duniani, hakuna.
Cha kushangaza na kusikitisha juzi Ukraine kwa kutumia mfumo wa kizamani wa Marekani wa Patriotic missiles defense system waliweza kutungua silaha za Kinzhal bila kizuizi chochote.
Sasa kama silaha ambazo Urusi inasema ni za kisasa na za teknolojia ya mbele zaidi ya wenzake zinaweza kutunguliwa na mfumo wa kizamani wa Patriotic missiles defense system, Urusi amebakia na nini?
Pili, juzi hapa ndege isiyo na rubani ama drone ilitunguliwa ikiwa juu ya ya paa ya nyumba anayoishi Putin.
Urusi ikawatuhumu Ukraine na Marekani kwamba wanataka kumuua Putin.
Swali la kujiuliza, Urusi haina mfumo wa ulinzi wa anga hadi drone isafiri kutoka Ukraine hadi Moscow bila mfumo wa anga wa Urusi kuitambua? Hii ina maana kwamba Marekani ama Ukraine wakitaka kumuua Putin ni dakika sifuri tu kwa sababu hana mfumo wa ulinzi wa anga wa kumlinda.
Binafsi nilikua namkubali sana Putin lakini kwa haya madhaifu makubwa yaliyotokea hapa karibuni naanza kua na mashaka na uwezo wa kijeshi wa Urusi.
Urusi alichobakisha ni silaha za nyuklia tu otherwise ni maneno tu.