Siasa za Tanzania na Nguvu ya Mwenyezi Mungu 2015-2020, 2020-2025

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,805
1,873
Mengi yamezungumzwa kufuatia vifo vya Aliyekuwa Raisi wa Tanzania John Magufuli (aliyefariki 17/3/2021) na Bernard Kamilius Membe (aliyefariki 12/5/2023). Wawili hawa ndio waliingia katika hatua za mwisho kuchaguliwa kuwa wagombea Uraisi kwa tiketi ya CCM, 2015. Yeyote kati ya hawa angeweza kuwa Raisi. Bahati ikamuangukia Magufuli.

Nguvu ya Mwenyezi Mungu imeonyesha kwamba kwa yeyote kati yao ambaye angekuwa Raisi wa Tanzania, kikomo chake kingekuwa katika kipindi chake cha awamu ya pili (2021-2025) ya Uraisi wake. Tofauti yao ingekuwa ni miaka 2 na miezi 2 katika kipindi hicho hicho cha Uraisi. Hili ni funzo kubwa sana ndugu zangu watanzania, linalothibitisha mapenzi ya Mwenyeezi Mungu, yaliyompendeza M Mungu katika siasa za Tanzania.

Ninaimani kuwa hata kama Bernard Kamilius Membe angemshinda John Magufuli katika uchaguzi ndani ya CCM 2015 bado makamu wake wa Raisi angekuwa Samia Suluhu Hassan. Hii inamaanisha kuwa Samia Suluhu Hassan ndiye angekuwa Raisi wa Tanzania bila kujali nani kati ya wawili hao angekuwa Raisi mwaka 2015-2020 na 2020-2025. Haya ni Mapenzi ya M Mungu. Samia ni Chaguo la M Mungu.

Kifo kinaweza kuja kwa namna tofauti, ugonjwa, ajali, umelala tu ndio moja kwa moja n.k. Utaumwa, utanyweshwa sumu lakimu M Mungu asipopenda utapona na kuendelea kuishi. Hayo yaliyotokea ndio aliyoyapenda M Mungu, Tuwaombee tu marehemu. Na tusiache kumuombea Rais wetu Samia Suluhu H, chaguo la M Mungu.
 
Back
Top Bottom