mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,098
- 9,994
Alikuwepo diwani maarufu kwa jina la Kanyanyila aliyeingia madarakani mwaka 2015 kuongoza kata yake ya Lusungo. Ilikuwa ni jambo la kushangaza kwa mwanamke kushikilia madaraka makubwa ya kisiasa namna hiyo hapo Lusungo na ukanda wa Ndamba kwa ujumla.
Utawala wake ulikuwa wenye kuudhi watu. Alikuwa mbabe sana na hakuwa msikivu. Hakuweza kuwapa huduma wananchi wake. Alijijengea utiisho sana kwa madaraka aliyopewa na mwishoni mwa madaraka yake alikumbwa na tuhuma za mauaji ya mtu asiye na hatia.
Muda wote wa utawala wake alizungukwa na chawa ambao muda wote walimwambia kuwa wako pamoja nae maana anaupiga mwingi. Chawa hawa walimwambia mama kanyanyila kuwa atapita miaka mitano mingine kwani anakubalika sana kwa yote anayo yafanya pale lusungo.
Ulifika muda wa kura za maoni ndani ya chama 2020, wajumbe ndani ya chama kwa umoja wao walipiga kura za hasira dhidi ya mama kanyanyila... aliangushwa akashika nafasi ya tatu.
Kamati ya siasa ya chama ngazi za juu ilitumia turufu yake kumpitisha mama huyu kuwa mgombea udiwani kupitia chama Tawala chenye mizizi yake kwa miaka mingi pale lusungo.
Wananchi walighafilishwa sana na jambo hilo.. ghadhabu hii ilikuwa kubwa kuliko kura za maoni.
Siku ya uchaguzi mkuu wote walipiga kura za udiwani kwa upande wa CDM huku wakimpa kura Raisi magufuli kwa upande wa uraisi. Kama Kanyanyila aliokota kura basi ni za familia yake tu.
Wilaya nzima ya Kyela kata moja tuu ya Lusungo ilipotelea upinzani.
Je, Watanzania wanaweza kufanya maamuzi magumu juu ya utawala huu mwaka 2025?