Mto Songwe unatajwa katika kuweza kuinua kipato cha wakaazi wa Jimbo la Songwe iwapo mto huo utatumika katika kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo mto huo ambao unamwaga maji yake katika Ziwa Rukwa una umuhimu kwa nchi mbili, Tanzania na Malawi. Kwani unamwaga maji yake ndani ya Ziwa Malawi/Nyasa vilevile.
Kabla ya kuendelea kujadili hili kuna memba yoyote mwenye ufahamu wa mto huu, unaanzia wapi?
Iwapo una manufaa kwa nchi mbili, je kuna mpango wowote wa kuwa na kamisheni ya pamoja kati ya Tz na Malawi ili kuona kuwa mto huo unatumika kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili pasipo kuwepo na ugomvi?
Kibunango,
... naomba wenye ujuzi na hayo maeneo tuelemisheni. Je mto Songwe unaanzia wapi na kuishia wapi?
.... ukimuuliza mwakipesile kwa nini unawachukuia hawa wezako hana jibu ukiwauliza wasomi hawa watakuambia kwanini ameteuliwa u RC na kuwekwa mbeya ....
nilipokuwa primary nilikuwa naishi kilomita 1 kutoka mto songwe ulipo. mpaka leo sijui unaanzia wapi lakin najua unamwaga maji yake ziwa nyasa. kijij nilichokuwa naishi mto huo ulikuwa unaact kama mpaka kat ya tz na malaw
mto huo ambao hauna kingo kama za mto kiwira unaletaga shida sana unapofurika miez ya 4 au 5 maana maji yake yanasambaa kwenye vijij vya jiran
Ila ndugu yangu mbona Mbeya hakuna akina Mwakatojofu? Sisi Mbeya wote ni majitu kwahiyo tunajiita Mwaitojofu au Mwalitojofu.
Kuhusu hawa waheshimiwa kupatanishwa mbona imefanywa mara nyingi? Hata kamati ya Kinana iliwapatanisha na wakaombana na msamaha, lakini kabla hata wino kwenye hayo makubaliano yao haujaisha, wakaanza kulimana vijembe.
kama hawa jamaa hawaelewani kweli hiv hakuna wa kuwapatanisha?
anaweza kuwa mbunge yeyote wa maeneo yale au mkuu wa mkoa wa mkoa jirani au kiongoz wa kitaifa.
siku akiwapatanisha inaweza kuwa habari kwenye vyombo vya habari na aliyewapatanisha anaweza pata credits ktk siasa. wanasiasa wetu hawaoni hii opportunity? cv inaweza kua
Lakini mimi nina shida kubwa hapa, nilikuwa nikiishi Mbeya wakati Mkuu wa Mkoa akiwa Maj Gen Makame. Gen Makame aliweza kufanya lolote awezalo juu ya Mbeya na still wanambeya walimshangilia. Ni kipindi hichohicho Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya alikuwa akitoka Ushirika(kitongoji kati ya Kiwira na Kyela).Na kilikuwa ni kipindi kofia mbili, katibu wa mkoa(CCM) akitokea Tanga(sahamani katibu huyo kwa sasa ni marehemu na jina limenitoka). Mbona hatukuweza kusikia longolongo zozote?
Ikumbukwe kuwa ni wakati au enzi hizo ambapo Mbeya Hotel ilivamiwa na hotel za watu binafsi, na ni kipindi hichohicho jumba la sinema opposite na Posta kuu ya Mbeya ilipogeuzwa kuwa jumba la kutangaza Injili. Na ni kipindi hicho hicho boogie disco ilipopigwa marufuku Mbeya. Sioni lolote katika mada hii kuhusu Gen Makame jinsi alivyoweza kuwafunga mdomo wanyakyusa! Ama kwa uwa kuwa alikuwa ni Mjeshi na amehusu Mtwara?
Tafadhalini sana nina omba tujiepushe na ukabila na udini, kwani hivyo sio sehemu ya maendeleo ya TZ kwa Ujumla. Iwapo Mkuu wa Mkoa wa sasa anapinga maendeleo ni vema kuweka bayana kuwa mkuu huyo ameweka mguu katika suala hili ama ile ambalo lina lengo la kuendeleza Mkoa huo!
Mimi binafsi hapa nilipo nje ya TZ, napokutana na watu wapendao kwenda TZ huwa nawaambia wasite kwenda Mbeya kuona comet, kule Mbozi, the highest road peak in Tz barabara ya kwenda Chunya, Daraja la Mungu Kiwira(Mshike adabu zenu na Mkapa, kwani yeye ana tengeneza umeme tu). Matofali ya Mungu(Lutengano karibu na shule ya Viziwi), Mlima Rungwe(wa tatu kwa urefu Tz) Milima ya Livingstone, lake Nyasa(sasa ni malawi...wanyakyusa wa Kyela mmelalal mno) Mfumo wa Kichifu, kilimo cha iriki,chai na kahawa.. na mambo tele..
Kwa wale waliokuwa Lutengano 1985-7,tuwasiliane
Indeed, lakini katika social life ya Jiji la Mbeya, Afande wako alichemka vibayaNilipokuwa National Service Makame alikuwa Kamanda kikosi, Mafanikio yake yanatokana na Charisma aliyo nayo, hata jeshini alikuwa anaelewana vizuri Karibu na askari wa ngazi zote. Anaproject aina fulani ya relaxation, nadhani vijana mnaita being cool, hivyo ukifanya nae kazi unachapa kazi bila kinyongo. ( I may be biased remember I was a kuruta then)
nakumbuka mengi alisha waasa wapiganaji kuwa mafisadi hawa wananguvu kubwa ya fedha na ushawishi na kwamba wanaweza kukuangamiza hata ukiwa nje ya nchi kwani wana mtandao.Matukio haya kwa mwakyembe ni kielelezo tosha,we unadhani Iringa ilipotokea ajari au Kyela ni mbali kiasi hicho kwa mafisadi?Thubutuuuuuu............usimjeruhi mbogo atakuua inabidi kuua kabisa(Hawa majeruhi Lowasa,Rostam,Karamagi watatumaliza tukiwaacha waendelee na ushawishi wao serikalini na kutumia umasikini wa wanakyela kuangamiza wapambanaji akiwemo dr.mwakyembe)
Kazi ipo!
Sikonge naomba wimbo wa Mayasa- Marijani Rajabu, kama unao kwenye archieves zako.
Waachieni polisi wafanye kazi yao! visu na mapanga ya nini kwenye mikutano! hahahahaha
Masa,
Hapo tupo pamoja. tusubiri POLISI wafanye kazi yao na si Mwandishi uchwara kuanza kuwahukumu vijana kwa hisia zake potofu.
Wimbo wa Mayasa, ohh my God. Nipe muda baada ya Weekend ntaanza kukutafutia. Tatizo hii miziki imekuwa too much na hadi nasahau kuwa ninayo. Ntaomba univumilie kidogo kwani sina uhakika kama ninayo au laah. Vinginevyo nitautafuta ni site gani upo na nikuelekeze ukadownload.
Sikonge,
Hii habari mimi niliituma moderators wa JF wakasema ni majungu.
Ni kwamba huyo kijana alikamatwa akiwa ana record mkutano wa mbunge kwa kutumia simu. Baada ya hapo wakamfungia kwenye gari, kisha wakampeleka nyumbani kwa mbunge Ikolo na kuanza kumpekua, wakamnyang'anya simu, wakasoma sms zote.
Walimkamata saa nane mchana lakini wakamfikisha polisi saa mbili usiku wakati huo tayari jeshi la polisi limeshaanza kumtafuta.
Walipoona balaa wakazua case ya kwamba alikuwa na mwenzake ambaye alikuwa na kisu na walitaka kumdhuru mbunge. Polisi hata wamejua kisu kilinunuliwa wapi mjini. Ni yale yale ya ajali ya Iringa na kusingizia kugongwa na lori kwa nyuma.
Kwa taarifa za chini chini, RCO na kundi lake wameshathibitisha kwamba ni uwongo mtupu na sasa wanaandaa taarifa ambayo kila mtu anaisubiri kwa hamu maana kuna mtu atafungwa safari hii.
Huwezi kumteka kijana na ukampeleka nyumbani kwako na kumtesa masaa sita wakati hiyo kazi ni ya polisi, tena polisi wenyewe wako sio mbali na hapo mkutano ulipokuwa unafanyika. Hayo yote yanafanywa mbunge anashiriki, mtu ambaye inatakiwa aongoze kwa kulinda sheria.
Nipashe hawataji muda kwasababu haiingii akilini umkamate mtu aliyetaka kumuua mbunge saa nane na umfikishe polisi saa tatu usiku.
Wengine hapa tumetulia na uwongo huu utaumbuliwa mno. Someni na nipashe ya leo muone waliyoyaandika. Ni magazeti ya Mengi yanatumiwa vibaya na watu ambao wanataka wabaki madarakani kwa njia zote. Kila mtu anasubiri RPC wa Mbeya anonge.
Asubuhi nimesikia kwenye uchambuzi Danny Mwakalinga sijui inakuwaje hapo Masa na Sikonge?