Si Vipapai, bali ni barabara

Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
195
Sheria za barabarani kama zikisimamiwa vizuri nafikiri hatuna tatizo kubwa, kwa mfano utoaji wa leseni kama uta-demand mtu lazima kupita chuo na driving test ikawa na maana sio njaa za trafiki nafikiri tutakuwa na madereva wazuri sana.

KIngine tujifunze kwenye nchi zenye sheria kali ambazo mtu anaogopa kuivunja kwani kosa lake malipo yake sio mchezo kwa mfano kama Japani ukizidisha mwendo tu na camera ikakuona faini yake ni kubwa mno pamoja na kufungiwa kwa muda usiopungua mwezi bila kuendesha gari.

Ngoja watunga sheria wanaoshindwa kuzisimamia wafe labda inaweza kusaidia. Mbona watu wanachinjwa kila siku lakini serikali iko usingizini, leo baada ya viongozi kupata ajali ndo wanaanza kuogopa. After all viongozi wengine ni ma-bogus hawana mchango +ve kwa jamii sana sana mafisadi tu.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,208
2,000
Madereva wajitetea juu ya za ajali za viongozi
Frederick Katulanda, Mwanza (mwananchi)

WAKATI taifa likiomboleza kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia aliyefarika katika ajali juzi mkoani Iringa, baadhi ya madreva wameeleza kuwa ajali nyingi zimekuwa zikiwakumba viongozi wa serikali zinatokana na baadhi yao kutoawajali madreva wao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana mjini hpa, baadhi ya madreva hao walisema ajali nyingi zimekuwa zikiwakumba viongozi kutokana na baadhi yao kuwafanyaisha kazi madreva wao wakiwa na njaa, usingizi, mawazo na hata matatizo ya kifamilia.

Akielezea ajali hizo dreva wa CCM mkoa Adamu Sudi, alisema kuwa viongozi wamekuwa wakiwatumia madreva bila ya kuwajali jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao kwa vile dreva kuendesha akiwa na njaa inaweza kusababishia ajali na hata kupoteza maisha.

"Mfano tatizo linaloweza kusabaisha ajali kwa viongozi ukiondoa uzembe wa madreva, ni viongozi kutowajali madreva wao, huwezi kuendeshwa na dreva mwenye njaa, ama unamfanyika kazi hadi usiku wa manane na kisha untaka alfajili akuendeshe, anahitaji kupumzika," alisema.

Dreva James Lisalaka alisema huku akitoa mfano kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwaangali madreva wao kama watu wasio na maana wakati wamekuwa wakilinda maisha yao katika safari na hivyo kusema kuwa wanapaswa kuwaangali na kujali afya zao.

"Madreva wanapokwenda safari baadhi ya viongozi wamekuwa wakishindwa kuwalipa hata posho, hatua ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi yao kuishi katika mazingira magumu, wengine kulala katika magari, kushinda njaa," alisema.

Wamesema kuwa baadhi ya viongozi pia wamekuwa wakichukua madreva wasio na uzoefu mkubwa kutokana na kuwalipa gharama kubwa na matokeo yake kusababisha ajali.
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0

Mhh,

hapa kuna kazi kweli!
 
Mwanamalundi

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,124
2,000
acha nikuulize kitu kidogo, serikali inapoamua kitu vyama vya siasa huusishwa ikiwa pamoja na ccm ?

Kada, mbona unazidi kunitia majaribuni. Are you real serious??? Kuna tofauti gani kati ya raisi na mwenyekiti wa CCM??? Una maana gani unaposema kuwa serikali inapoamua kitu CCM haihusishwi??? Au unataka uone wamevaa mashati ya kijani na kofia za njano ndio ujue kuna mkono wa CCM katika haya maamuzi???Karibu mawaziri wote wamo NEC if not central committee. How do you disentangle CCM from the current government???

nafahamu unachosema, angalau viongozi wa ccm huwa na ilani ambayo ni kama dira yao ya kuaccomplish hizo ahadi, kumaanisha tokea wapange kwenye chama, chama hakitohusika tena katika maamuzi ya serikali.

Yaani hapa kada ndio umeboronga kwelikweli. Kumbe CCM haina ubavu wa kuwauliza viongozi wa serikali juu ya utekelezaji wa ilani yao. Tunashukuru kwa kuliweka wazi hili hapa JF. Nadhani kila mtu amesikia.

pia kuna tofauti kubwa, si unaona mfano marehemu mama Mbatia alipokuwa anaenda nadhani kwenye shughuli za chama, lakini alitumia gari binafsi na kuiacha ya serikali serikalini!

Kada, kwanza huna uhakika na unachoongea. Umetumia neno nadhani. Hata hivyo kutumia gari binafsi sio hoja. Yaani unauliza swali na kujijibu mwenyewe.

Tatizo linalokukabili ni la kushindwa kutofautisha the roles of technocrats and policy makers. Technocrats si lazima awe mwanachama wa CCM, au chama chochote cha siasa. Kati ya makundi haya mawili, kundi lenye nguvu ni lile linalohusisha policy makers. Kazi ya technocrats ni kudadavua sera za policy makers. Kwa mfano, ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 inatamka bayana kuwa mpaka kufikia 2010, mikoa yote ya tanzania inatakiwa kuwa imeunganishwa kwa barabara zenye kiwango cha lami. Ilani haisemi aina ya kokoto, aina ya lami, upana wa barabara, madaraja, etc. Hii ni kazi ya technocrats.
 
Aug 2, 2007
61
0
wanaforums hapa si barabara wala madereva,,swala hawa waheshimiwa inabidi wamrudie mungu huu ndio wakati wenyewe hata kama wakiweka 6lanes,,nani asiejua ajali ngapi zinapatikan kwenye mororgoro road kutoka ubungo mpaka mbezi,,na hivi sasa wanataka kuongeza barabara kupunguza ajali,,swala wamjue mungu,,kama huamini wawape nafasi baadhi ya wachungaji waingie bungeni wakeme mapepo ya uchawi na mengineyo muone vituko vitkavyotokea,,,hata wanaforums hivi sasa tunaitaji kumrudia mungu pia kuna baadhi ya topic unmwachia mungu aseme nao,,come back to jesus
 
WembeMkali

JF-Expert Member
Jun 16, 2007
282
0
Sijui tutalirudia hili mpaka lini.Tatizo hapa si uchawi,vipapai,kulogana,ndumbwe,au kuoneana gere ! Tatizo hapa ni mlolongo wa mambo kadhaa ambayo Serikali na viongozi hawayatilii maanani au wanayazembea tu au hawaoni kuwa ni priority kwao.Nilishawahi kueleza huko nyuma kwenye thread nyingine kuwa ubovu wa barabara,kutozingatia sheria za barabarani,mfumo mbovu wa utoaji wa leseni za uendeshaji magari,kutokuwa na mfumo mzuri wa kukagua magari yote kila baada ya muda fulani kupita na mambo mengine kadha wa kadha kama walivyochangia wenzangu hapo juu kuwa ndiyo hasa kiini cha ajali hizi ambazo zimechinja watanzania wengi na zinaendelea kuua kila kukicha.
Tulipolalamika kuwa ni kwanini wabunge wanakopeshwa mashangingi tukaambiwa kuwa ni kwa ajili ya kuwawezesha kufika vijijini eti kwa sababu barabara ni mbovu!.Yaani viongozi wetu waliona kuwa huo ndio ufumbuzi wa matatizo ya usafiri vijijini.
Wengine tukapigwa na butwaa zaidi pale suala la msongamano wa magari lilipoanza kuwa kero kwa wananchi tukaelezwa kuwa serikali inampango wa kununua helikopta kwa viongozi ili kuwawezesha kufika haraka! Kwao hilo ndiyo suluhisho la msongamano wa magari barabarani na kana kwamba siye wengine hatustahili kuwahi huko tunakoenda.Hii ndiyo serikali inayojiita ya watu na kujifanya kuwa iko kwa ajili ya watu.Nadhani sasa wameanza kuona kuwa mashangingi siyo suluhisho la matatizo ya usafiri kwani nayo yameshawaua sana ukiachilia mbali kuwakata mikono na viungo vingine vya mwili.Na muda si mrefu pia mungu epushia mbali tutanaweza kabisa kuambiwa kuwa helikopta nazo zimeanguka na kuua wote waliomo!
Sasa basi ili serikali iweze kupunguza matatizo ya usafiri na ajali mbaya za barabarani ni lazima izingatie mambo kama hayo tuliyayataja hapo juu na labda ni yafupishe tu kwa kifupi.

1)Kuweka sheria KALI KABISA kwa madereva ambao wanavuna sheria za barabarani.Na ikiwezekana kuwanyang'a kabisa leseni zao pindi wanapofanya makosa yanayoweza kusababisha ajali.
2) Kuwe na ukaguzi wa magari kwa kila baada ya muda fulani kupita.Kwa mfano kila baada ya miaka miwili gari lifanyiwe uchunguzi kabla ya kuruhusiwa kuwa barabarani tena.Hii itasaidia kuondoa magari mabovu barabarani na kuepusha ajali zisizo za lazima.
3)Kunyonga matrafiki wote ambao hupokea rushwa na kuruhusu magari mabovu kuendelea na safari zake au kuruhusu madereva wanaovunja sheria za barabarani kuendelea na safari zao.Kwa sababu wao nao wanahalalisha mauti kwa raia wasio na hatia.
4)Kujenga na kukarabati barabara zote mpaka vijijini na siyo kununua mashangingi au helikopta.
5)Kutoa mafunzo bora kwa madereva wetu kuhusu uendeshaji na usalama watu barabarani kabla ya kutoa leseni kwa madereva.
6)Kuweka kando siasa na kutimiza wajibu.

Wembemkali.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,208
2,000
Kujaribu kuondoa siasa katika maendeleo ya nchi ni kujaribu kuweka samaki kwenye mchanga. Siasa ndiyo kiini cha utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo. Ni siasa ambayo inatengeneza dira ya Kitaifa na inaunda sera ya kufikia dira hiyo. Hivyo serikali yoyote duniani haiwezi kufanya kazi zake pasipo kufungumana moja kwa moja na siasa za chama chake tawala au mwelekeo wake wa kisera kama Taifa.

Serikali iliyoko madarakani katika Tanzania inatokana na wanasiasa, na sera zake zimetungwa na/ na zinatekelezwa katika ngazi za juu kabisa na wanasiasa. Ni maamuizi ya kisiasa yanayoamua nani anapata nini, na wapi kinafanyika nini. Hivyo basi siasa kama ilivyosemwa ni kiini cha msingi na ndio maana katika vile vitu vinne tunavyohitaji ili tuendelee utaona kuwa kuna "siasa bora".

Tatizo la Tanzania siyo watu au viongozi wazuri n.k, tatizo lake kimsingi ni siasa isiyo na mwelekeo, malengo yasiyo na dira, na maono yasiyoeleweka. Kiini cha matatizo yetu leo hii kama Taifa kimeanzia na kinaishia kwenye siasa.

Ninapozungumzia mapambano ya kiitikadi na kifikra kiini chake ni mgongano wa mwelekeo wa kisiasa uliopo nchini.

Hivyo mtu yeyote hata akiwa na malengo mazuri kiasi anayejaribu kutalikisha uhusiano huo wa asili uliopo kati ya siasa na maendeleo ya nchi haitendei haki nchi yetu, na mwelekeo wa mawazo yake ni "myopic".

Kama kweli tunataka kujenga Taifa la kisasa, hatuna budi kuangalia kwanza siasa zetu ziko vipi na mwelekeo wake ukoje, na nini kifanyike ili tuwe na mazingira bora zaidi ya kisiasa. Somo hili siyo gumu kulielewa, na sitasita kujaribu kulifafanua kwa yule ambaye linakuwa gumu kidogo. Msaada wa wachambuzi wengine bila shaka unahitajika.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,074
2,000
ama Wabunge na viongozi wametishika, basi wapeleke mswaada wa kujenga barabara pana na zenye lami kuunganisha mikoa na si kujenga viwanja vya ndege au kununua tundege tudogo eti kuepuka ajali.

Naunga mkono suala la upanuzi wa barabara, hasa hizi za mkoa wa Iringa, ni nyembaba mno.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,074
2,000
Kazi ya technocrats ni kudadavua sera za policy makers. Kwa mfano, ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 inatamka bayana kuwa mpaka kufikia 2010, mikoa yote ya tanzania inatakiwa kuwa imeunganishwa kwa barabara zenye kiwango cha lami. Ilani haisemi aina ya kokoto, aina ya lami, upana wa barabara, madaraja, etc. Hii ni kazi ya technocrats.

Ni kweli kabisa, tutenganishe siasa na utaalamu!
 
NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
560
0
acha nikuulize kitu kidogo, serikali inapoamua kitu vyama vya siasa huusishwa ikiwa pamoja na ccm ? nafahamu unachosema, angalau viongozi wa ccm huwa na ilani ambayo ni kama dira yao ya kuaccomplish hizo ahadi, kumaanisha tokea wapange kwenye chama, chama hakitohusika tena katika maamuzi ya serikali.

pia kuna tofauti kubwa, si unaona mfano marehemu mama Mbatia ( Mungu amrehemu) alipokuwa anaenda nadhani kwenye shughuli za chama, lakini alitumia gari binafsi na kuiacha ya serikali serikalini !

Nikukumbushe tena kidogo, zipo taarifa hapa JF na wewe unazifahamu, kuwa alikuwa atumie gari la serikali kwa kazi hiyo hiyo, lakini kwa vile dereva alichelewa (sijui shauri ya foleni ama vipi) akaamua kutumia gari lake binafsi. Kwa hiyo, kihoja, hapo haujashika kabisa, tafuta nyingine, hiyo nyepesi mno.....
 
djwalwa

Member
Sep 27, 2007
39

Huu ni udaku kwa hiyo upelekwe kwa Shigongo akauze magazeti yake. Kuna mambo mengi ya msingi ya kutafakari juu ya kuinusuru nchi yetu na UFISADI. Haya mambo ya kutumia sijui gari binafsi sijui la serikali haitusaidii chochote. It is already history, let us discuss future
 
Shemzigwa

JF-Expert Member
Jan 8, 2007
336

Babu naona umeidandia tren kwa mbele ungesoma toka mwanzo kimbembe chenyewe ungeelewa!
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,814
2,000
Madereva wajitetea juu ya za ajali za viongozi
Frederick Katulanda, Mwanza (mwananchi)

WAKATI taifa likiomboleza kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia aliyefarika katika ajali juzi mkoani Iringa, baadhi ya madreva wameeleza kuwa ajali nyingi zimekuwa zikiwakumba viongozi wa serikali zinatokana na baadhi yao kutoawajali madreva wao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana mjini hpa, baadhi ya madreva hao walisema ajali nyingi zimekuwa zikiwakumba viongozi kutokana na baadhi yao kuwafanyaisha kazi madreva wao wakiwa na njaa, usingizi, mawazo na hata matatizo ya kifamilia.

Akielezea ajali hizo dreva wa CCM mkoa Adamu Sudi, alisema kuwa viongozi wamekuwa wakiwatumia madreva bila ya kuwajali jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao kwa vile dreva kuendesha akiwa na njaa inaweza kusababishia ajali na hata kupoteza maisha.

"Mfano tatizo linaloweza kusabaisha ajali kwa viongozi ukiondoa uzembe wa madreva, ni viongozi kutowajali madreva wao, huwezi kuendeshwa na dreva mwenye njaa, ama unamfanyika kazi hadi usiku wa manane na kisha untaka alfajili akuendeshe, anahitaji kupumzika," alisema.

Dreva James Lisalaka alisema huku akitoa mfano kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwaangali madreva wao kama watu wasio na maana wakati wamekuwa wakilinda maisha yao katika safari na hivyo kusema kuwa wanapaswa kuwaangali na kujali afya zao.

"Madreva wanapokwenda safari baadhi ya viongozi wamekuwa wakishindwa kuwalipa hata posho, hatua ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi yao kuishi katika mazingira magumu, wengine kulala katika magari, kushinda njaa," alisema.

Wamesema kuwa baadhi ya viongozi pia wamekuwa wakichukua madreva wasio na uzoefu mkubwa kutokana na kuwalipa gharama kubwa na matokeo yake kusababisha ajali.

Hii ni point nzuri sana. Nimeona mara nyingi TZ, wakubwa wanajichana, dereva kalala na njaa kwenye gari, kisha safari inaanza.

Pia kuna suala la mkuu wa safari kuwa ndiye controller wa safari yenyewe wakati si ajabu hajui hata kuendesha gari. Wenzetu huku
ni sheria ukiendesha masaa mawili inatakiwa upumzike, Tanzania madereva wengine wanaendesha hata masaa manane bila kupumzika.
Huenda madereva wa malori na mabus ni sawa lakini kwa dereva ambaye anaenda safari ndefu mara chache sana, ni hatai kuendesha gari kwa masaa nane bila kupumzika.

Ukimwuliza dereva umechoka, tupumzike, anakuambia hapana anaweza kuendesha siku nzima. Ukweli ni kwamba anaona akisema amechoka ataonekana weak, matokeo yake wanasababisha ajali.
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,814
2,000
wanaforums hapa si barabara wala madereva,,swala hawa waheshimiwa inabidi wamrudie mungu huu ndio wakati wenyewe hata kama wakiweka 6lanes,,nani asiejua ajali ngapi zinapatikan kwenye mororgoro road kutoka ubungo mpaka mbezi,,na hivi sasa wanataka kuongeza barabara kupunguza ajali,,swala wamjue mungu,,kama huamini wawape nafasi baadhi ya wachungaji waingie bungeni wakeme mapepo ya uchawi na mengineyo muone vituko vitkavyotokea,,,hata wanaforums hivi sasa tunaitaji kumrudia mungu pia kuna baadhi ya topic unmwachia mungu aseme nao,,come back to jesus

This is total rubish, Watanzania wote wanaokufa kwa ajali kwa mwaka ni wanasiasa? Anapokufa mwanasiasa mmoja, kuna raia wema wengine 100 wamekufa.

Huyo mungu anatuandama sisi tu Tanzania? Mbona hawa wengine ambao hata hawamjui mungu, wana ajali kidogo sana kulinganisha na sisi?

Kwani wachungaji kuhubiri mpaka waende bungeni?
 
Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Rev. Kishoka,

Nakubaliana na mengine yote uliyoyandika isipokuwa hilo la kupanua barabara, je utapanua kama ile barabara ya Morogoro mpaka Mbeya ili iwe na lane ngapi? Je ni economically feasible kufanya hivyo? Tuna pesa za kufanya hivyo wakati robo tatu ya nchi yetu haina barabara za maana? Je hata tukipanua tutapunguza ajali? Ukiangalia barabara nzuri TZ ndio zinaongoza kwa ajali, yaani ile ya Dar mpaka Arusha na ya Dar mpaka Mbeya. Uk

Nafikiri muhimu kwa TZ ni alama barabarani, sheria za kubana madereva wanaokimbiza magari, ubora wa magari, ubora wa barabara kwamba zisiwe na mashimo ambayo yanaweza kusababisha ajali na elimu ya kutosha kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara.

Mtanzania,

Umeuliza economical benefits za kupanua barabara nitakujibu.

Je unajua kisa cha nchi zote zilizoendelea kuwa na barabara kubwa na pana? Nitakupa mfano mmoja tu wa Marekani. Wakati wa vita kuu ya dunia, Rais wa Marekani alitoa fungu maalum la pesa (kuongeza kosi0 ili kuhakikisha kuwa barabara zilikuwa ni kubwa, bora na zenye kutoka ng'ambo moja mpaka kwingine ili kurahisisha usafirishaji wa wanajeshi na vyombo vyao kuzuia Taifa lao lisivamiwe.
Matokeo yake ni mfumo mkubwa wa kiuchumi wa mawasiliano na uchukuzi (usafirishaji) ambao umelisaidia sana Taifa la Marekani katika maendeleo yake.

Sisi tutapata faid kubwa sana kama tungejenga barabara kuu kuunganisha mikoa ambazo ni pana(just two lanes each direction) kama Morogoro road kuanzia pale UWT road mpaka Kimara mjini.

Hili lingeimarisha sana;

1. Ufanisi katika uchukuzi (usafirishaji) wa bidhaa hasa mazao ya wakulima na mahitaji ya lazima. Hili halitaishia mikoani tuu, bali hata kwa nchi majirani ambao hawana midomo ya bahari kupeleka mali zao ghafi ughaibuni. chukulia mfano hata wa Kenya kupeleka bidhaa Malawi mpaka Namibia!
2. Kurahisisha na kufupisha muda na gharma za kusafiri. Barabara kubwa na nzuri hupunguza misongamano na ni rahisi kudhibiti mwendo kasi wa madereva.
3. Kupeleka maendeleo katika mikoa inayoachwa nyuma kila siku kutokana na ukosefu wa vitendea kazi vya kucochea maendeleo.

Naomba tusiendelee kuwa masikini wa mawazo na woga wa kutumia pesa ambazo matunda yake ni makubwa kwa vijukuu wetu.

Tusiwe na yale mawazo ya kusema kuwa Kompyuta ni anasa na ni kitu cha kitajiri na fahari hivyo ni mwiko na haina mnufaa kiuchumi!

Wenzetu wako sasa kwenye Nanotech, sisi bado tunapanda punda!
 
Sam

JF-Expert Member
Jun 6, 2006
416
0
Rev.
I think you are too general. Ili tuendelee lazima tuelewe kwanza mazingira yanayotuzunguka. Kwa kuwa huu mjadara umetokea baada ya kifo cha mama Mbatia naomba tuchukulia barabara ya Njombe-Songea as our case example. Kwa sisi tunayoijua labda ninaweza kusema ni moja ya barabara bora kabisa katika nchi yetu. Ndiyo ni nyembamba ina lane mbili. Kwa wakati wa mchana labda gari zinapiga baada ya dakika 10 mpaka 15. Wakati wa usiku ni baada ya saa hadi masaa mawili. Naomba nifafanulie umuhimu wa kuipanua hiyo barabara kwa manufaa ya kiuchumi kama ulivyoelezea.
Kwa watu mnaoishi US najua mnajua most of the highways speed limit ni 65m/hr ambayo ni sawa na 105km/hr. Lakini watu wengi wanaenda zaidi ya 100m/hr ambayo ni kama 160km/hr. Kuna wakati inatokea kuna bonge ya traffic kwenye highway na gari zote ziko zaidi ya 100m/hr na hakuna ajari inayotokea. Hayo ni mazingira ya wenzetu ambayo nao wanalalamika sana kuwa barabara nyingi zinatakiwa kupanuliwa. Kwenye mazingira yetu ambapo interval ya magari ni 10-15 minutes ajari kila kukicha. Nini nini tatizo.
Nimeangalia ile picha na kuchunguza lile gari sijaona kitu kinaitwa air bags. Kwa wale mnaojua physics mtakubaliana na mimi kuwa kama gari lina-move at 90km/hr basi na abiria waliomo ndani wana move at the same speed. Kwa muda alioondoka Iringa na muda aliopata ajari lazima walimkuwa wako over speed limit let say 90.1 km/hr, hivi mtu uki crush at that speend without air bags utapona?
Jambo jingine ambalo nimegundua hapa ni kwamba watanzania wengi hawafahamu muundo wa serikali yao kabisa na jinsi inavyofanya kazi. Wengi wenu hamuwezi kutofautisha kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na mipaka ya kazi zake. Wengi wenu hamjua ni barabara gani ziko chini ya ya serikali kuu au serikali za mitaa. Mnachojua ninyi ni kuwa barabara zote ziko chini ya CCM. Mmmh. Hivi halmashari ya Karatu inafuata Ilani za CCM katika kutekeleza majukumu yake? KadaMpinzani alikuwa anataka kuwaeleza mambo yalivyo na nyie mmeanza kumpinga kabla hamjaelewa. I think the most important thing to understand before you move to the next step of development is to understand your surroundings. Baada ya hapo ndiyo unaweza kuamua kama hivyo ndiyo unataka iwe au unahitaji mabadiliko.
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,814
2,000
Rev. Kishoka,

Kweli kwa barabara ambayo gari zinapita kwa rate ya kama gari 10 kwa saa utapanua hiyo barabara ili ilete faida zipi?

Tunachotakiwa ni kujenga barabara kama ya Mbeya mpaka Morogoro kwenye mikoa mingine yote ili kurahisha usafiri na hivyo kupeleka maendeleo huko mikoani na wilayani.

Kama alivyosema Sam, kupanua barabara kama ya Makambako mpaka Njombe ni kupoteza bure pesa za wananchi. Afadhali hizo fedha zitumike kwenye miradi mingine ya maendeleo.

Sababu zinazosababisha ajali zinajulikana, upana wa barabara labda unachukua nafasi ya chini kabisa.
 
Mwanamalundi

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,124
2,000
Rev.
Nini nini tatizo.Nimeangalia ile picha na kuchunguza lile gari sijaona kitu kinaitwa air bags

Kwa hiyo unataka kutuambia chanzo cha ajali ni kukosekana kwa air bags kwenye gari ya marehemu??? Yaani kwa kuangalia picha, tayari umeshapata majibu??? Umelichunguza gari kivipi??? Uchunguzi unafanyika kwenye picha???Be serious sam.

Rev.
..Jambo jingine ambalo nimegundua hapa ni kwamba watanzania wengi hawafahamu muundo wa serikali yao kabisa na jinsi inavyofanya kazi. Wengi wenu hamuwezi kutofautisha kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na mipaka ya kazi zake. .

Ni watanzania gani wanaoshiriki kujadili mada hapa, unadhani hawajui muundo wa serikali. I think this is too simplistic and overgeneralization.

Rev.
Wengi wenu hamuwezi kutofautisha kati ya serikali kuu na serikali za mitaa na mipaka ya kazi zake. .

Huu ni udhalilishaji. Ungelijua usingelithubutu kuandika hicho ulichoandika hapo

Rev.
Mnachojua ninyi ni kuwa barabara zote ziko chini ya CCM. Mmmh. Hivi halmashari ya Karatu inafuata Ilani za CCM katika kutekeleza majukumu yake? .

Again, hii ni kushusha heshima ya wachangiaji hapa. Nilitoa mfano hapo awali; kuunganisha barabara za mikoa yote kwa kiwango cha lami. Nani ametaja barabara za karatu hapa???

Rev.
KadaMpinzani alikuwa anataka kuwaeleza mambo yalivyo na nyie mmeanza kumpinga kabla hamjaelewa. .

kada hakuwa na hoja ndio maana ameingia mitini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom