Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,531
Tukaambiwa wale 27 wa ajali ya Mbeya ni kafara ya saidia Taifa Stars iwafunge Machinga, Huko Singida wamefariki watatu sijui ilikuwa ndio kafara ya kumtafuta aliyemlawiti mtoto mdogo?
Waswahili tunapenda kukimbilia imani chafu panapotokea balaa. Mudhihir, Kapuya, Mwakanjuki na sasa Mama Mbatia. Si kufuru za Chadema au CUF, bali ni ubovu wa barabara zetu ulioandamana na sheria mbovu, ulafi wa wenye magari na kukosekana kwa nidhamu kwa madereva ambayo ungeambatana na mafunzo bora.
Kwa nini mpaka leo Taifa halijaanza mpango rasmi wa kupanua barabara kuu? Kwa nini kila kuna kuna matuta makubwa katika barabara kama tuta la viazi?
Ni kwa kuwa tumeachilia siasa ishikilie uhandisi na mipango bora.
Kama Serikali itakuwa makini, waache kutafuta mchawi na kufuja pesa hovyo na kuwanza kampeni rasmi ya kupanua barabara zetu, ambazo zitakua na alama bora na udhibiti wa mwendo kasi unaofanya na madereva.
Jee ile wiki ya Usalama barabarani ishakufa au ndio mtaji wa trafiki?
Kama Wabunge na viongozi wametishika, basi wapeleke mswaada wa kujenga barabara pana na zenye lami kuunganisha mikoa na si kujenga viwanja vya ndege au kununua tundege tudogo eti kuepuka ajali.
Si kipapai, kafara au malipo kwa kufuru ya ufisadi, bali ni barabara nyembamba na mbovu!
Mungu aziweke mahali pema roho za wote waliopoteza masha kwa ajali hizi na awape nguvu na afya walio majeruhi.