Baba mtakatifu91
JF-Expert Member
- Apr 25, 2026
- 3,971
- 8,319
Na hapo kwa mumeo ni sawa kabisa ila kama ni maswala ya uzazi mwambie mama yakoKwa Mungu sawa kabisa
Na hapo kwa mumeo ni sawa kabisa ila kama ni maswala ya uzazi mwambie mama yakoKwa Mungu sawa kabisa
Hii mwenyewe ni shahidi so mpka nakuja na hili bandiko nimejifunza1. Kutangaziwa hapo ndo penyewe 😝unaweza kujuta kuelezea tatizo lako
Anaweza mtu kukusikiliza ukadhani utasaidika kumbe umemuuzia udhaifu ambao atautumia dhidi yako2. Kila mtu ana matatizo yake. Hapa nimejifunza kitu.unaweza kuomba ushauri kwa mtu ambaye hayuko huko kabisa na hata hakusikilizi.😜
Sahihi kabisa japo pia umakini unahitajikaMimi Niko radhi kuomba ushauri kwa asiyenijua na nisiyemjua kabisa
Hii inavutia sana ❤️Ohoooo! Nakuambia kabisa
Ni wapi nije kukuungishaUkiishiwa gesi usipate shida mkuu. Fika kwenye gas station yangu utapatiwa huduma ya uhakika! 😂😂😂
In fact,Katika dunia tunayoishi leo, si rahisi kupata msaada wa kweli wa kihisia kutoka kwa watu
Mara nyingi mtu anapokuwa na changamoto hutamani kuonewa huruma kuambiwa maneno ya faraja, kushikwa mkono, kusaidiwa kifedha au hata kusaidiwa kwa vitendo
Kwa kawaida, msaada huo unaweza kuupata kutoka kwa mtaalamu wa saikolojia, rafiki wa karibu, mpenzi au ndugu
Lakini ukweli ni kwamba hata hao tunaowategemea wana maisha yao na mizigo yao ya kihisia
Wanaweza kuwa wanapitia matatizo makubwa kuliko hata yako
Hali hiyo inaweza kufanya ushindwe kupata kile ulichokitarajia kutoka kwao, na wakati mwingine ukajikuta unawalaumu, ilhali wao pia walikuwa wanahitaji mtu wa kuwasaidia
Pia, si kila mtu ana uwezo wa kushauri au kubeba hisia za watu wengine
Unaweza kujikuta umemweleza mtu ambaye hana busara, hana uzoefu au hana uwezo wa kushughulikia tatizo lako
Mwisho wa siku, badala ya kupata nafuu unarudi ukiwa na maumivu makubwa zaidi
Wakati mwingine unapomfuata mtu ukimweleza jinsi unavyojisikia, kuna uwezekano wa mambo mawili kutokea
ama akushauri kwa hekima au akaenda kutangaza siri zako kwa wengine
Hapo ndipo unapojikuta umefedheheka, umevunjika moyo na kujutia kwa nini ulimwamini mtu ambaye hakutunza uaminifu wako Badala ya mzigo kupungua, unaongezewa jeraha jingine
Sasa jiulize, ni mara ngapi umewahi kuomba ushauri halafu baadaye ukajuta?
Ni mara ngapi ulijiona kama umejidhalilisha kwa sababu ulimfungulia mtu moyo, lakini hakukuelewa au hakutunza siri yako?
Au pengine uliomba ushauri kutoka kwa mtu ambaye naye alikuwa anahitaji msaada kama wewe
Hapo ndipo swali linazaliwa: ikiwa anayekuongoza naye anahitaji kuongozwa, nani atamwongoza mwenzake?
Kwa mtazamo wangu, kila mtu anatakiwa ajifunze kujifanyia ushauri binafsi kwa kiwango fulani
Sisemi kwamba watu wasitafute msaada, lakini ukweli ni kwamba hakuna anayejua maumivu yako, historia yako na uwezo wako wa kuyavumilia kuliko wewe mwenyewe
Ukijifunza kujitafakari, kujielewa na kutuliza hisia zako, utagundua kuwa wakati mwingine majibu mengi yapo ndani yako 📌
Sasa mtu anawezaje kujishauri mwenyewe?
Kwanza, kubali hisia zako Usijilazimishe kuonekana uko sawa wakati ndani unaumia
Kukubali kwamba una huzuni, hasira, hofu au maumivu ndiyo mwanzo wa kupata suluhisho
Pili, usifanye maamuzi ukiwa umejaa hasira, huzuni au maumivu
Jipe muda wa kutulia kwanza, kwa sababu hisia za muda zinaweza kukufanya ufanye maamuzi ambayo baadaye utayajutia
Tatu, jifunze kujiuliza maswali ya kweli🤔
Jiulize tatizo ni nini hasa, chanzo chake ni nini na ni hatua gani unaweza kuanza nayo leo badala ya kuendelea kulaumu kila kitu
Nne, andika mawazo yako
Mara nyingi mawazo yanapokuwa kichwani yanaonekana makubwa kuliko uhalisia wake
Ukiyaandika, unapata nafasi ya kuyachambua kwa utulivu
Tano, acha kujilaumu kwa kila jambo
Kubali makosa pale ulipokosea, lakini usijibebeshe mzigo wa mambo ambayo hayakuwa ndani ya uwezo wako
Pia, jifunze kuwaondoa au kuwaweka mbali na maisha yako watu ambao unaona wazi kabisa hawachangii uponyaji wako
📌 📌
Kuna watu kila unapowafuata ukiwa na tatizo, badala ya kukupa amani wanakuongezea hofu, lawama, msongo wa mawazo na maumivu
Si kila mtu anayepaswa kujua kila kinachoendelea kwenye maisha yako 📌
Linda amani yako ya akili
Kama unaona uwepo wa mtu fulani kila mara unakufanya ujisikie vibaya, unapoteza kujiamini au unaondoka ukiwa umeumia zaidi kuliko ulivyokuwa mwanzo, usione vibaya kupunguza ukaribu naye 📌
Wakati mwingine njia ya kupona si kuongeza watu wengi kwenye maisha yako, bali ni kupunguza wale wanaokuongezea maumivu
Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba kujishauri mwenyewe kuna mipaka yake
Kuna wakati maumivu yanakuwa makubwa kiasi kwamba huwezi tena kujiongoza peke yako
Katika hali kama hiyo, usione aibu kutafuta msaada kutoka kwa mtu unayemwamini au kwa mtaalamu
Kuomba msaada si udhaifu, bali ni busara unapogundua kuwa mzigo umekuwa mkubwa kuliko uwezo wako
Mwisho, kumbuka kwamba si kila anayekusikiliza ana uwezo wa kukuponya, lakini pia si kila tatizo linahitaji kuwafikia watu wengi
Jifunze kuisikiliza nafsi yako, kuituliza kwa hekima, kuchukua hatua sahihi na kumtegemea Mungu katika kila jambo(kama una imani)
Wakati mwingine, tiba kubwa si maneno ya watu, bali ni utulivu wa moyo unaoupata baada ya kujielewa na kuamua kusonga mbele
JE UNA TABIA YA KUJISHAURI MWENYEWE?
UNATUMIA NJIA GANI?
KARIBU
ShesRise_1 🤚
CC Marcostilone
Mimi mumeo siwezi kutangaza habari zako kufanya hivyo nitakuwa naivunja ndoa yangu kwa mikono yangu mwenyeweKuna wanaume wambeya uongoo realMamy 🤣
Unahitajika umakini mkubwa sana hapa pia.Hii mwenyewe ni shahidi so mpka nakuja na hili bandiko nimejifunza
Na this time najifunza ku solve matatizo yangu madogo madogo bila kuomba ushauri
Anaweza mtu kukusikiliza ukadhani utasaidika kumbe umemuuzia udhaifu ambao atautumia dhidi yako
Sahihi kabisa japo pia umakini unahitajika
Tupo Singida mjini. Karibu sana. Ukijaza mtungi saizi yo yote unatumia kwa miaka miwili mpaka minne.Ni wapi nije kukuungisha
Gentleman nimesema sio mara zote unatakiwa kuomba ushauriIn fact,
suala la kutegemeana kwa binadamu kwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushauriana haliepukiki, na hakunaga bingwa wa maisha katika ulimwengu huu. Tunahitajiana sana kama binadamu.
Hapa nagongelea na nyundo mara zote watu wanao kumaliza ni wale uliowaamini na kuwauzia kila kitu kukuhusu mpka udhaifu wakoNi muhimu sana kujizuia kutoa siri za ufalme wako kwa watesi wako ambao saa zingine unaweza kudhani ni rafiki zako sana, kwasababu kwa kufanya hivyo unawapa urahisi wa kukuangamiza kwa namna ambayo hutatarajia.
Narudia kwamba sisemi watu wasiombe ushauriLakini pia,
ni vizuri kuepuka kujiuliza na kujijibu mwenyewe, hasa kwenye mazingira ambayo unahitaji jawabu mbadala la changamoto yako nje ya mawazo yao, athowise unaweza kujikuta jibu au suluhisho la ulichojiuliza ikawa ni kujinyonga, na kwamba hiyo ndio the best solution kwa ulichojiuliza.
Exactly 🐒Tugeuze changamoto tunazokumbana nazo kua fursa muhimu sana za kutufanya tuwe makini zaidi, tujipange upya, tujirekebishe, tujisahihishe na kufanya vizuri zaidi mbeleni 🐒
Exactly sweetheartUnahitajika umakini mkubwa sana hapa pia.
Tukome Sasa kujieleza 😝
Kuna watu nilikuwa nawaamini sana na kila nikitaka kufanya jambo nilikuwa nawashirikisha sasa walijikuta wanajua kila kitu pasipo wao eti siwezi toboa. Saivi nimekuwa mtu wa kujiamlia mambo acha waninunie mara ooh we jamaa umekuwa mjanja wakati ndo tumekupokea mjini. Namshukuru Mungu mambo yangu yanaenda fresh tu tangu niache kuwashirikisha mambo yangu. Leo kuna jambo nilitaka nisikie ushauri wao kuhusu wazo la kufuga samaki acha wakosoe mara huwezi kufuga samaki wa ziwani ukiwa Dodoma haaaaaah.Hii mwenyewe ni shahidi so mpka nakuja na hili bandiko nimejifunza
Na this time najifunza ku solve matatizo yangu madogo madogo bila kuomba ushauri
Anaweza mtu kukusikiliza ukadhani utasaidika kumbe umemuuzia udhaifu ambao atautumia dhidi yako
Sahihi kabisa japo pia umakini unahitajika
Shukran kaka mimi sipo singinda nipo kwenye jiji la chalamilaTupo Singida mjini. Karibu sana. Ukijaza mtungi saizi yo yote unatumia kwa miaka miwili mpaka minne.
Wewe umeshaelewa na unaajua cha kufanya hapo sina la kuongezaKuna watu nilikuwa nawaamini sana na kila nikitaka kufanya jambo nilikuwa nawashirikisha sasa walijikuta wanajua kila kitu pasipo wao eti siwezi toboa. Saivi nimekuwa mtu wa kujiamlia mambo acha waninunie mara ooh we jamaa umekuwa mjanja wakati ndo tumekupokea mjini. Namshukuru Mungu mambo yangu yanaenda fresh tu tangu niache kuwashirikisha mambo yangu. Leo kuna jambo niliwaambia eti nataka nianze kufuga samaki acha wakosoe mara huwezi kufuga samaki wa ziwani ukiwa Dodoma haaaaaah.
Asante dada kwa kiniappreciateWewe umeshaelewa na unaajua cha kufanya hapo sina la kuongeza
KaribuAsante dada kwa kiniappreciate
Mi nalalaKaribu
Lala salama🙏Mi nalala
Obheja bujiku mwakaLala salama🙏