Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Watu wengi tumedanganywa na maneno kama, “Ulikuwa unaishi kabla hujamjua,” au “Umejuana naye ukubwani.” Maneno haya wakati mwingine yanatufanya tuwachukulie poa watu ambao tumekutana nao katika maisha yetu, kwa sababu tunaamini kwamba wakiondoka, tutakuja kupata wengine.
Lakini usidanganyike. Si kila mtu pengo lake linaweza kuzibika. Kuna watu ukimpoteza, unaweza kukutana na watu wengi baada yake, lakini bado ukakosa yule aliyekuwa na nafasi yake ya kipekee katika maisha yako.
Kauli hii huwezi kuielewa vizuri kama hujawahi kumpoteza mtu mzuri, ukajaribu kutafuta mtu kama yeye na ukamkosa. Ni kawaida ya binadamu kutambua thamani ya mtu baada ya kumpoteza, lakini wakati mwingine majuto huja wakati ambao hakuna tena nafasi ya kurekebisha mambo.
Kama umebahatika kumpata mtu ambaye ukiwa naye una amani, furaha na utulivu, mtunze. Weka pembeni kiburi. Ukimkosea, muombe msamaha. Usijidanganye kwamba kwa sababu anakupenda, basi atarudi tu kila wakati.
Wala usijidanganye kwamba kwa sababu uliwahi kumpata mtu mzuri, basi utampata mwingine kama yeye. Watu wanaomuomba Mungu awape mtu mwenye tabia kama yake ni wengi sana. Pengine Mungu alikupendelea miongoni mwa hao wengi na akakupa nafasi ya kuwa naye.
Na kama akiondoka kwako, huenda akaenda kwa mtu mwingine ambaye atamthamini, kumheshimu na kumpa nafasi ambayo wewe ulimnyima.
Kabla hujafika katika hatua ya kujuta sana, mlinde, mtunze, mpe kipaumbele na mthamini. Usisubiri kumpoteza ndipo uanze kuelewa thamani yake.
Kwa kufanya hivyo, utakuwa umempa sababu ya kubaki na wewe, na hata kama siku moja ataondoka, hutajuta kwamba matendo yako ndiyo yaliyosababisha aondoke.
Mthamini mtu wako akiwa bado yupo. Maana wakati mwingine, pengo la mtu fulani halizibwi kwa kumpata mwingine, bali hubaki kuwa kumbukumbu ya mtu ambaye ulipaswa kumthamini zaidi.