Si kila tatizo linahitaji kumweleza Mtu!

Si kila tatizo linahitaji kumweleza Mtu!

Kwa mimi mkimya huwa najishauri mim mwenyew tu.

Kuna mtu unaweza kumwelezea shida yako badala akushauri anaanza kukuzodoa, hadi unajiraum kwanin umemshirikisha.

Kwakwel napenda uturivu, nikikaa peke angu ahsubuh au jua linapozama mahari iwe pemben ya mto, juu ya ghorofa ama mliman juu.

Ntaenda huko ntajitafakari mwenyew nakujishauri huku nikitazama uzuri wa nchi.

Natoka huko nimepata majibu na moyo/hakil imepata uturivu
 
Katika dunia tunayoishi leo, si rahisi kupata msaada wa kweli wa kihisia kutoka kwa watu

Mara nyingi mtu anapokuwa na changamoto hutamani kuonewa huruma kuambiwa maneno ya faraja, kushikwa mkono, kusaidiwa kifedha au hata kusaidiwa kwa vitendo

Kwa kawaida, msaada huo unaweza kuupata kutoka kwa mtaalamu wa saikolojia, rafiki wa karibu, mpenzi au ndugu

Lakini ukweli ni kwamba hata hao tunaowategemea wana maisha yao na mizigo yao ya kihisia

Wanaweza kuwa wanapitia matatizo makubwa kuliko hata yako

Hali hiyo inaweza kufanya ushindwe kupata kile ulichokitarajia kutoka kwao, na wakati mwingine ukajikuta unawalaumu, ilhali wao pia walikuwa wanahitaji mtu wa kuwasaidia

Pia, si kila mtu ana uwezo wa kushauri au kubeba hisia za watu wengine

Unaweza kujikuta umemweleza mtu ambaye hana busara, hana uzoefu au hana uwezo wa kushughulikia tatizo lako

Mwisho wa siku, badala ya kupata nafuu unarudi ukiwa na maumivu makubwa zaidi

Wakati mwingine unapomfuata mtu ukimweleza jinsi unavyojisikia, kuna uwezekano wa mambo mawili kutokea
ama akushauri kwa hekima au akaenda kutangaza siri zako kwa wengine

Hapo ndipo unapojikuta umefedheheka, umevunjika moyo na kujutia kwa nini ulimwamini mtu ambaye hakutunza uaminifu wako Badala ya mzigo kupungua, unaongezewa jeraha jingine

Sasa jiulize, ni mara ngapi umewahi kuomba ushauri halafu baadaye ukajuta?

Ni mara ngapi ulijiona kama umejidhalilisha kwa sababu ulimfungulia mtu moyo, lakini hakukuelewa au hakutunza siri yako?

Au pengine uliomba ushauri kutoka kwa mtu ambaye naye alikuwa anahitaji msaada kama wewe

Hapo ndipo swali linazaliwa: ikiwa anayekuongoza naye anahitaji kuongozwa, nani atamwongoza mwenzake?

Kwa mtazamo wangu, kila mtu anatakiwa ajifunze kujifanyia ushauri binafsi kwa kiwango fulani

Sisemi kwamba watu wasitafute msaada, lakini ukweli ni kwamba hakuna anayejua maumivu yako, historia yako na uwezo wako wa kuyavumilia kuliko wewe mwenyewe

Ukijifunza kujitafakari, kujielewa na kutuliza hisia zako, utagundua kuwa wakati mwingine majibu mengi yapo ndani yako 📌

Sasa mtu anawezaje kujishauri mwenyewe?

Kwanza, kubali hisia zako Usijilazimishe kuonekana uko sawa wakati ndani unaumia

Kukubali kwamba una huzuni, hasira, hofu au maumivu ndiyo mwanzo wa kupata suluhisho

Pili, usifanye maamuzi ukiwa umejaa hasira, huzuni au maumivu

Jipe muda wa kutulia kwanza, kwa sababu hisia za muda zinaweza kukufanya ufanye maamuzi ambayo baadaye utayajutia

Tatu, jifunze kujiuliza maswali ya kweli🤔

Jiulize tatizo ni nini hasa, chanzo chake ni nini na ni hatua gani unaweza kuanza nayo leo badala ya kuendelea kulaumu kila kitu

Nne, andika mawazo yako
Mara nyingi mawazo yanapokuwa kichwani yanaonekana makubwa kuliko uhalisia wake

Ukiyaandika, unapata nafasi ya kuyachambua kwa utulivu

Tano, acha kujilaumu kwa kila jambo

Kubali makosa pale ulipokosea, lakini usijibebeshe mzigo wa mambo ambayo hayakuwa ndani ya uwezo wako

Pia, jifunze kuwaondoa au kuwaweka mbali na maisha yako watu ambao unaona wazi kabisa hawachangii uponyaji wako
📌 📌

Kuna watu kila unapowafuata ukiwa na tatizo, badala ya kukupa amani wanakuongezea hofu, lawama, msongo wa mawazo na maumivu

Si kila mtu anayepaswa kujua kila kinachoendelea kwenye maisha yako 📌

Linda amani yako ya akili

Kama unaona uwepo wa mtu fulani kila mara unakufanya ujisikie vibaya, unapoteza kujiamini au unaondoka ukiwa umeumia zaidi kuliko ulivyokuwa mwanzo, usione vibaya kupunguza ukaribu naye 📌

Wakati mwingine njia ya kupona si kuongeza watu wengi kwenye maisha yako, bali ni kupunguza wale wanaokuongezea maumivu

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba kujishauri mwenyewe kuna mipaka yake

Kuna wakati maumivu yanakuwa makubwa kiasi kwamba huwezi tena kujiongoza peke yako

Katika hali kama hiyo, usione aibu kutafuta msaada kutoka kwa mtu unayemwamini au kwa mtaalamu

Kuomba msaada si udhaifu, bali ni busara unapogundua kuwa mzigo umekuwa mkubwa kuliko uwezo wako

Mwisho, kumbuka kwamba si kila anayekusikiliza ana uwezo wa kukuponya, lakini pia si kila tatizo linahitaji kuwafikia watu wengi

Jifunze kuisikiliza nafsi yako, kuituliza kwa hekima, kuchukua hatua sahihi na kumtegemea Mungu katika kila jambo(kama una imani)

Wakati mwingine, tiba kubwa si maneno ya watu, bali ni utulivu wa moyo unaoupata baada ya kujielewa na kuamua kusonga mbele

JE UNA TABIA YA KUJISHAURI MWENYEWE?

UNATUMIA NJIA GANI?

KARIBU


ShesRise_1 🤚

CC Marcostilone

Una akili sana we mama, hivi ushaolewa?

Nje ya topic though😛😛😎
 
Bado kuna mchumba huko🤣🤣🤣
Nimechoka kulala kama panga

Kuna fine kwa kutoka njee ya topic 😜

Vijana wa kibongo hawataki mwanamke mwenye akili mingi ujue! 😛 😛 haya maanalysis yako yanawaweka mbali sana yani wanaona bora wakapige monde zao na kata k zao!

Anyway nakusoma...
 
Vijana wa kibongo hawataki mwanamke mwenye akili mingi ujue! 😛 😛 haya maanalysis yako yanawaweka mbali sana yani wanaona bora wakapige monde zao na kata k zao!
Upo sahihi hata kama umeongea kwa njia ya utani ni ukweli tupu

Uzuri mimi sivutiwi kabisa na vijana
Na sijui kwa nini ikiwa mi mwenyewe sio mtu mzima

Anyway nakusoma...
Karibu ulipotea jukwaani lakini
 
Upo sahihi hata kama umeongea kwa njia ya utani ni ukweli tupu

Uzuri mimi sivutiwi kabisa na vijana
Na sijui kwa nini ikiwa mi mwenyewe sio mtu mzima


Karibu ulipotea jukwaani lakini

Maisha magumu, kuna mida unajilipua kuifukuzia shilingi hadi unasahau ndugu na jamaa jeifuni, anyway shukrani sana nipo tena jamvini, by the way unamaanisha wazee wakumbukwe?
 
Kwa mimi mkimya huwa najishauri mim mwenyew tu.
Hongera
Kuna mtu unaweza kumwelezea shida yako badala akushauri anaanza kukuzodoa, hadi unajiraum kwanin umemshirikisha.
Tatizo linaanzia hapa
Kwakwel napenda uturivu, nikikaa peke angu ahsubuh au jua linapozama mahari iwe pemben ya mto, juu ya ghorofa ama mliman juu.

Ntaenda huko ntajitafakari mwenyew nakujishauri huku nikitazama uzuri wa nchi.

Natoka huko nimepata majibu na moyo/hakil imepata uturivu
Hongera sana una maisha yako fulani ya kuvutia
 
Vijana wa kisasa hawapendi mambo magumu yani, hamna kuumiza kichwa siku hizi, mambo ya kufakarisha haya nani anataka? Chuo tu tunadesa sembuse kitaani?
Hao vijana wasiopenda haya mambo basi wasubiri zile nyuzi zangu za kulombana nitawapa hitaji la moyo wao😅😅
 
Yaan mtu Hakikisha matatizo yako unakomaa nayo Mwenyewe
Kulikuwa na mchungaji ni rafiki yangu sana
Kila watu wakienda kuomba ushauri ye kwenye kahawa tukiwa tunapata jion ananisimulia kwamba usione mzee fulan mkewe hivi na vile ,

Usione watoto wa mama fulan bangi Tupu

Yaan ikikubidi usimwambie mtu matatizo yako
shukurani nimepata somo
 
Nina Jinsi ya kutatua changamoto zangu
Ikiwa nahitaji ushauri wa kutoka nje huwa napenda kuweka tatizo langu Kwa njia ya maswali ambapo huwa nauliza watu zaidi ya mmoja, pia Kuna muda nahitaji tu mtu wa kunisikiliza bila ya yeye kushauri chochote na Kuna muda nataka kuwa muda nataka either nilewe au nitombane tu.
 
Back
Top Bottom