Si kila tatizo linahitaji kumweleza Mtu!

Si kila tatizo linahitaji kumweleza Mtu!

Upo sahihi ngoja tuende na wachache wanaolewa

Uzuri ni kua nina aina nyingi za mada
Mara nyingine nakua kwenye siasa
Kwenye habari kama hizi za leo
Bila kusahau mada za wakubwa 😅

So kila mmoja anaependa kusoma mada zangu ata enjoy tu
Endelea na mtindo huu huu Madam, anayeelewa ataelewa.
 
Binti:

Huwa napendelea sana mada zako maana, kwa kiasi fulani, zinaonyesha ukomavu katika baadhi ya mambo. Hata hivyo kuna wakati huwa nahisi kama wakati mwingine thread zako zinakuwa ndefu unnecessarily. Kama unavyojua attention span ya watu wengi siku hizi ni shida. Hivyo pengine kuna watu wengi tu ambao wanakosa busara zako kwa uzi kuwa mrefu bila sababu za msingi. Kama ukiweza, na kama ulimwelewa vizuri mwalimu wako wa Ufupisho darasa la 4 somo la Kiswahili, hebu jaribu kuwa unazifupisha hizi thread bana bila kuzipotezea utamu na mguso wake. Huu ni ushauri na observation yangu tu na so lazima uuzingatie 🙏🏿.

Back to the topic: Privacy is power hasa kwetu introverts. Mpaka nikaseme kitu kwa mtu aisee labda sijui iweje. Labda nikiambiwa nina terminal cancer na nina mwezi mmoja tu wa kuishi. Naamini kwamba mbali na mama yangu, hakuna mtu mwingine anayenitakia mema kwa asilimia 100 hapa duniani. Hata marafiki zangu naamini hawapendi wakisikia I am doing better than them. Ndo maana hata ikitokea nikawashirikisha kitu (kizuri au kibaya), sisemi ukweli wote. Nasema ambacho nadhani kitaendana na uhalisia wao. Ndivyo ninavyoishi. Nikibanana sana afadhali nikaongee na therapist huko asiyenijua au bro wangu asiye na makuu Evelyn Salt 😂😂😂

Zaidi ya hapo ni mimi na Mungu wangu tunasaidiana kutatua changamoto zinazotukabili 🙏🏿
Hayaee bwana Tonny Kapora naona unapata vya kuhubiria kanisani
 
Katika dunia tunayoishi leo, si rahisi kupata msaada wa kweli wa kihisia kutoka kwa watu

Mara nyingi mtu anapokuwa na changamoto hutamani kuonewa huruma kuambiwa maneno ya faraja, kushikwa mkono, kusaidiwa kifedha au hata kusaidiwa kwa vitendo

Kwa kawaida, msaada huo unaweza kuupata kutoka kwa mtaalamu wa saikolojia, rafiki wa karibu, mpenzi au ndugu

Lakini ukweli ni kwamba hata hao tunaowategemea wana maisha yao na mizigo yao ya kihisia

Wanaweza kuwa wanapitia matatizo makubwa kuliko hata yako

Hali hiyo inaweza kufanya ushindwe kupata kile ulichokitarajia kutoka kwao, na wakati mwingine ukajikuta unawalaumu, ilhali wao pia walikuwa wanahitaji mtu wa kuwasaidia

Pia, si kila mtu ana uwezo wa kushauri au kubeba hisia za watu wengine

Unaweza kujikuta umemweleza mtu ambaye hana busara, hana uzoefu au hana uwezo wa kushughulikia tatizo lako

Mwisho wa siku, badala ya kupata nafuu unarudi ukiwa na maumivu makubwa zaidi

Wakati mwingine unapomfuata mtu ukimweleza jinsi unavyojisikia, kuna uwezekano wa mambo mawili kutokea
ama akushauri kwa hekima au akaenda kutangaza siri zako kwa wengine

Hapo ndipo unapojikuta umefedheheka, umevunjika moyo na kujutia kwa nini ulimwamini mtu ambaye hakutunza uaminifu wako Badala ya mzigo kupungua, unaongezewa jeraha jingine

Sasa jiulize, ni mara ngapi umewahi kuomba ushauri halafu baadaye ukajuta?

Ni mara ngapi ulijiona kama umejidhalilisha kwa sababu ulimfungulia mtu moyo, lakini hakukuelewa au hakutunza siri yako?

Au pengine uliomba ushauri kutoka kwa mtu ambaye naye alikuwa anahitaji msaada kama wewe

Hapo ndipo swali linazaliwa: ikiwa anayekuongoza naye anahitaji kuongozwa, nani atamwongoza mwenzake?

Kwa mtazamo wangu, kila mtu anatakiwa ajifunze kujifanyia ushauri binafsi kwa kiwango fulani

Sisemi kwamba watu wasitafute msaada, lakini ukweli ni kwamba hakuna anayejua maumivu yako, historia yako na uwezo wako wa kuyavumilia kuliko wewe mwenyewe

Ukijifunza kujitafakari, kujielewa na kutuliza hisia zako, utagundua kuwa wakati mwingine majibu mengi yapo ndani yako 📌

Sasa mtu anawezaje kujishauri mwenyewe?

Kwanza, kubali hisia zako Usijilazimishe kuonekana uko sawa wakati ndani unaumia

Kukubali kwamba una huzuni, hasira, hofu au maumivu ndiyo mwanzo wa kupata suluhisho

Pili, usifanye maamuzi ukiwa umejaa hasira, huzuni au maumivu

Jipe muda wa kutulia kwanza, kwa sababu hisia za muda zinaweza kukufanya ufanye maamuzi ambayo baadaye utayajutia

Tatu, jifunze kujiuliza maswali ya kweli🤔

Jiulize tatizo ni nini hasa, chanzo chake ni nini na ni hatua gani unaweza kuanza nayo leo badala ya kuendelea kulaumu kila kitu

Nne, andika mawazo yako
Mara nyingi mawazo yanapokuwa kichwani yanaonekana makubwa kuliko uhalisia wake

Ukiyaandika, unapata nafasi ya kuyachambua kwa utulivu

Tano, acha kujilaumu kwa kila jambo

Kubali makosa pale ulipokosea, lakini usijibebeshe mzigo wa mambo ambayo hayakuwa ndani ya uwezo wako

Pia, jifunze kuwaondoa au kuwaweka mbali na maisha yako watu ambao unaona wazi kabisa hawachangii uponyaji wako
📌 📌

Kuna watu kila unapowafuata ukiwa na tatizo, badala ya kukupa amani wanakuongezea hofu, lawama, msongo wa mawazo na maumivu

Si kila mtu anayepaswa kujua kila kinachoendelea kwenye maisha yako 📌

Linda amani yako ya akili

Kama unaona uwepo wa mtu fulani kila mara unakufanya ujisikie vibaya, unapoteza kujiamini au unaondoka ukiwa umeumia zaidi kuliko ulivyokuwa mwanzo, usione vibaya kupunguza ukaribu naye 📌

Wakati mwingine njia ya kupona si kuongeza watu wengi kwenye maisha yako, bali ni kupunguza wale wanaokuongezea maumivu

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba kujishauri mwenyewe kuna mipaka yake

Kuna wakati maumivu yanakuwa makubwa kiasi kwamba huwezi tena kujiongoza peke yako

Katika hali kama hiyo, usione aibu kutafuta msaada kutoka kwa mtu unayemwamini au kwa mtaalamu

Kuomba msaada si udhaifu, bali ni busara unapogundua kuwa mzigo umekuwa mkubwa kuliko uwezo wako

Mwisho, kumbuka kwamba si kila anayekusikiliza ana uwezo wa kukuponya, lakini pia si kila tatizo linahitaji kuwafikia watu wengi

Jifunze kuisikiliza nafsi yako, kuituliza kwa hekima, kuchukua hatua sahihi na kumtegemea Mungu katika kila jambo(kama una imani)

Wakati mwingine, tiba kubwa si maneno ya watu, bali ni utulivu wa moyo unaoupata baada ya kujielewa na kuamua kusonga mbele

JE UNA TABIA YA KUJISHAURI MWENYEWE?

UNATUMIA NJIA GANI?

KARIBU


ShesRise_1 🤚

CC Marcostilone
1. Kutangaziwa hapo ndo penyewe 😝unaweza kujuta kuelezea tatizo lako

2. Kila mtu ana matatizo yake. Hapa nimejifunza kitu.unaweza kuomba ushauri kwa mtu ambaye hayuko huko kabisa na hata hakusikilizi.😜

Mimi Niko radhi kuomba ushauri kwa asiyenijua na nisiyemjua kabisa
 
1. Kutangaziwa hapo ndo penyewe 😝unaweza kujuta kuelezea tatizo lako

2. Kila mtu ana matatizo yake. Hapa nimejifunza kitu.unaweza kuomba ushauri kwa mtu ambaye hayuko huko kabisa na hata hakusikilizi.😜

Mimi Niko radhi kuomba ushauri kwa asiyenijua na nisiyemjua kabisa
Hakuna mtu sahihi wa kimweleza shida zako isipokuwa Mungu na mumeo
 
Back
Top Bottom