Shule ya Turkish Maarif School Arusha ni tatizo

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
8,721
13,959
Shule zote nchini zimefunguliwa jana, hii shule iko Ngaramtoni Arusha, inamilikiwa na Waturuki.

Viongozi wa shule wanawarudisha watoto kisa ni ada. Kuna watoto wametoka Manyara wamerudishiwa getini.

Wizara ya Elimu angalieni hii shule. Angalieni dhima ya mnaowapa vibali vya kuendesha shughuli za elimu hapa Tanzania.

Baadhi ya wazazi wameshalipa zaidi ya nusu ya ada ya mwaka lakini watoto wanarudishiwa getini. Siamini kwamba huu ni utaratibu mzuri.

Mtoto ana kosa gani?

Utawala unatakiwa kuangalia utaratibu mzuri na wazazi na sio kuwatesa watoto.
 
Uwe umekamilisha Kila kitu alafu wakurudishe Mlangoni. Trust me LIPA ADA KAMA HAWAJAKURUHUSU KUINGIA.

SERIKALI hauwezi kuhangaika na hao Turkish people kuwarudisha wanafunzi getini Ilihali inashule zake Kila kata
 
Shule za serikali za bure zipo huko ulifuata nini? Lipa ada acha mbambamba!
Wanawake ndio wanaowaingiza mkenge wanaume kuingiza Watoto shule za Kingereza bila kujari uwezo halisi wa familia.

Wanaume wengi wamegeuzwa mateka na wake zao mbele ya familia, mama anatafuta shule ghari Baba utowe pesa ya ada.

Kwakweli inatia huruma 80% ya wanaosomesha Watoto shule za Kingereza hawana uwezo huo, ni kujiumiza tu.
 
Naona kila kitu unawasukumizia wanawake

Hata kweli kwenye sababu ya kuvunjika ndoa umeng'aka kimanga, ha ha ha ha.

Hivi huna pesa kweli umkubalie tu mke, utakuwa zwazwa hasaa.
 
Shule zote nchini zimefunguliwa jana, hii shule iko Ngaramtoni Arusha, inamilikiwa na Waturuki.

Viongozi wa shule wanawarudisha watoto kisa ni ada. Kuna watoto wametoka Manyara wamerudishiwa getini.

Wizara ya Elimu angalieni hii shule. Angalieni dhima ya mnaowapa vibali vya kuendesha shughuli za elimu hapa Tanzania.

Baadhi ya wazazi wameshalipa zaidi ya nusu ya ada ya mwaka lakini watoto wanarudishiwa getini. Siamini kwamba huu ni utaratibu mzuri.

Mtoto ana kosa gani?

Utawala unatakiwa kuangalia utaratibu mzuri na wazazi na sio kuwatesa watoto.
Kuna shure za bure ,sasa kwa nn ujipe mzigo ambako unaona kabisa hauwez kutoboa
 
Mh. Waziri,

Shule zimefunguliwa juzi, hii shule imekataa kupokea wanafunzi kwa madai hawajalipa ada. Wanafunzi waliotoka mikoani wanarudishiwa getini.

Nijuavyo mimi, wanafunzi hawajaingia mkataba na shule, bali tatizo ni mzazi na utawala wa shule. Nashauri kabla shule haijapatiwa kibali iwe inachunguzwa malengo yake. Hii shule ya Waturuki wana hujumu juhudi kubwa za serikali kukuza elimu.

Naomba Mh. Waziri fuatilia hii shule kwa karibu. Pia wananchi wanataka kujua waliwezaje kuchukua hili eneo na kilikuwa kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum. Eneo lilitolewa na serikali kwa minajili hiyo na sio biashara ya shule.
 
Back
Top Bottom