Shule ya Turkish Maarif School Arusha ni tatizo

Shule ya Turkish Maarif School Arusha ni tatizo

Watanzania wanapenda sana huruma hata pasipo stahili huruma.... nilijua kuna waliomaliza ada wakafukuzwa! Kumbe wanadaiwa kweli, walipe ada.
 
Wabongo wengi ni mabogas sana,ina maana mnaomponda mtoa hoja mnataka kusema hana logic???
Hana logic.. hata chakula kinatoka kwenye Ada hiyo hiyo. Kama huna Ada wasiliana Kwanza na uongozi wa shule kabla mtoto hujamsafirisha kwenda shule.
 
Shule zote nchini zimefunguliwa jana, hii shule iko Ngaramtoni Arusha, inamilikiwa na Waturuki.

Viongozi wa shule wanawarudisha watoto kisa ni ada. Kuna watoto wametoka Manyara wamerudishiwa getini.

Wizara ya Elimu angalieni hii shule. Angalieni dhima ya mnaowapa vibali vya kuendesha shughuli za elimu hapa Tanzania.

Baadhi ya wazazi wameshalipa zaidi ya nusu ya ada ya mwaka lakini watoto wanarudishiwa getini. Siamini kwamba huu ni utaratibu mzuri.

Mtoto ana kosa gani?

Utawala unatakiwa kuangalia utaratibu mzuri na wazazi na sio kuwatesa watoto.
Mkuu mbona Shule ni nyingi?
Mpeleke Shule unayoweza kuimudu.
 
Wabongo wengi ni mabogas sana,ina maana mnaomponda mtoa hoja mnataka kusema hana logic???
Ndiyo, hana logic. Ametia sahihi mkataba kuwa atalipa karo kwa awamu, inafika awamu hataki kulipa. Mtoto wake atapewaje huduma ya bure. Mbona benki tukikopa tukishindwa kulipa nyumba au shamba au vote huchukuliwa na huwezi kulalamika. Au unategemea wazazi wa watoto wengine wagharimie elimu ya mtoto wako japo kwa muda.
 
Waturuki taratibu wanateka vizazi vya Watanzania kupitia shule zao. Hata Wakristo wanagombania kupeleka watoto wao shule za Kituruki. Mturuki anachukuliwa kama Mzungu Tanzania, lakini ukienda Ulaya anadharauliwa. Ulaya na Marekani ni Waislamu tu ndiyo wanapeleka watoto wao shule za Waturuki.
Kudharauliwa Ulaya siyo sababu kamili ya kutetea kutolipa karo. Waturuki elimu ya yao ni nzuri na wana vyuo vyenye sifa kubwa duniani. Wameendelea kama nchi zingine au zaidi ya nchi zingine Ulaya. Huoni wanavyochapa kazi kwenye SGR. Unafikiri mainjinia wao wamepata wapi elimu. Naona wewe unawachukia kwa vile ni Waislamu. Wacha chuki na ubaguzi wa kidini weye mlokole.
 
Hujaelewa nini? Jibu hoja kwa hoja! Hata Waislamu wanapeleka Watoto wao shule za mission kupata elimu, but it all comes at a cost. Mitaala ya elimu ya Tanzania ni duni based on rote memorization (kukariri random facts), plus rampant corruption in the govt ndiyo maana Waturuki wanafanya biashara nzuri za mashule nchi masikini kama Tanzania.. Waturuki hawapenyi nchi zilizoendela na mtandao wao wa shule za msingi/sekondari kama Feza. Wakiruhusiwa kuanzisha shule nchi za dunia ya kwanza, ni kwa gia ya shule za Kiislamu, na hawatoi mainstream education. Mzungu maskini hawezi mpeleka mwanae shule ya kituruki sababu hazikidhi viwango vya elimu nchi husika, , lakini Tanzania hata JPM alimpeleka mwanae Feza. Sitoshangaa hizi Feza Schools zipo chini ya viwango vya elimu vya Uturuki yenyewe.
Feza ziko cchini ya viwngo vya shule za Waturki kwa kutumia vipimo gani? Tumia takwimu kuthibitisha au achana na uongo kwa vitu usivyo na uhakika navyo. We call that a sweeping statement.
 
Feza ziko cchini ya viwngo vya shule za Waturki kwa kutumia vipimo gani? Tumia takwimu kuthibitisha au achana na uongo kwa vitu usivyo na uhakika navyo. We call that a sweeping statement.
Chini ya viwango kwa kufuata mitaala ya NECTA. Wanafunzi watakuwa wanafanya vizuri kwa viwango vya Tanzania lakini siyo kwa viwango vya Uturuki. Shule kama Feza wana academic programs mbili: International na local. Ile ya local ndiyo NECTA na ada zao ni za chini. Ile ya International ina ada kubwa na viwango vya juu zaidi vya Cambridge. Hapo tayari Feza Schools wameamua mitaala ya NECTA ni duni.
 
Wanawake ndio wanaowaingiza mkenge wanaume kuingiza Watoto shule za Kingereza bila kujari uwezo halisi wa familia.

Wanaume wengi wamegeuzwa mateka na wake zao mbele ya familia, mama anatafuta shule ghari Baba utowe pesa ya ada.

Kwakweli inatia huruma 80% ya wanaosomesha Watoto shule za Kingereza hawana uwezo huo, ni kujiumiza tu.
100% correct, agiza mguu mzima wa mbuzi nakuja kulipa.
 
Wanawake ndio wanaowaingiza mkenge wanaume kuingiza Watoto shule za Kingereza bila kujari uwezo halisi wa familia.

Wanaume wengi wamegeuzwa mateka na wake zao mbele ya familia, mama anatafuta shule ghari Baba utowe pesa ya ada.

Kwakweli inatia huruma 80% ya wanaosomesha Watoto shule za Kingereza hawana uwezo huo, ni kujiumiza tu.
This is FACT.

Mkuu kwahili nakubaliana nawewe kabisa, na sio shule tu, wanawake huwa wanalazimisha mambo yaliyo nje ya uwezo wa familia ilimradi tu

Wanapenda kuiga iga.
 
Feza ziko chini ya viwngo vya shule za Waturki kwa kutumia vipimo gani? Tumia takwimu kuthibitisha au achana na uongo kwa vitu usivyo na uhakika navyo. We call that a sweeping statement.
 
Members Wamemsagia Kunguni Mleta Thread Mwanzo ~Mwisho





Lete Maneno.....Mzazi
 
Mh. Waziri,

Shule zimefunguliwa juzi, hii shule imekataa kupokea wanafunzi kwa madai hawajalipa ada. Wanafunzi waliotoka mikoani wanarudishiwa getini.

Nijuavyo mimi, wanafunzi hawajaingia mkataba na shule, bali tatizo ni mzazi na utawala wa shule. Nashauri kabla shule haijapatiwa kibali iwe inachunguzwa malengo yake. Hii shule ya Waturuki wana hujumu juhudi kubwa za serikali kukuza elimu.

Naomba Mh. Waziri fuatilia hii shule kwa karibu. Pia wananchi wanataka kujua waliwezaje kuchukua hili eneo na kilikuwa kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum. Eneo lilitolewa na serikali kwa minajili hiyo na sio biashara ya shule.
Mkuu habari

Naomba kujua fee structure ya hii shule ina range ngapi
 
Back
Top Bottom