KERO Shule ya Msingi Kamara iliyopo Mungonya, Halmashauri ya Kigoma, walimu wamewageuza wanafunzi vibarua wao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Walimu wamekuwa na tabia ya kuwapeleka wanafunzi muda wa vipindi kufanya kazi za shamba, ikiwamo kulima, kupalilia, kuvuna na kupukuchua mahindi pamoja na kuwachotea na kuwapelekea maji walimu majumbani kwao wale wanaoishi kwenye nyumba za kota za shule.

Nyakati nyingine wanafunzi wanarudishwa muda wa jioni kwa ajili ya kufanya kazi hizo.
 
Habari ya leo?

Wananchi wa kijiji cha kamara kilichopo ndani ya kata yamungonya wilaya ya kigoma mkoani kigoma. Tumekuwa na kero sugu iliyopo katika shule ya msingi kamara iliyopo ndani ya kijiji chetu. Walimu wamekuwa na mtindo wa kuwapa kazi zao binafsi zisizo za kitaaluma wanafunzi wazifanye tena katika muda ambao ni wavipindi.

Wamekuwa na mfululizo wa kuwatoa wanafunzi darasani na kuwapa wanafunzi kazi binafsi za shamba ikiwamo kulima, kupalilia, kuvuna na kupukuchua mahindi ya walimu hali inayopekea wanafunzi kusoma nusu siku na nusu nyingine kufanya kazi binafsi za walimu. Mbaya zaidi hata madarasa ya mtihani wanakatishwa vipindi wanapewa kazi hizo.

Muda mwingine wanafunzi hurudishwa jioni kwa ajili ya kwenda kuchota na kuwapelekea maji walimu wanaoishi kwenye nyumba za shule ya kutumia kwa shughuli zao binafsi hali inayowaweka wanafunzi kwenye hatari ya kufanyiwa ukatiri na kudumaza muda wao wa kujihimarisha kitaaluma.

Tunaomba mtusaidie kupaza sauti mamlaka husika zichukue hatua kwa ajili ya kuokoa kuzorota kwa hali za kitaaluma za wanafunzi wa shule ya msingi kamara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…