gasper jj
Member
- Nov 13, 2012
- 54
- 40
tukiita shule ya uongozi huoni tutakuwa tuna muenzi H. Polepole maana alishaanzisha shule ya uongozi on line. au amekuomba umwakilishie wazo.Sikatai kumuenzi Mwalimu nyerere,
Lakini hii kasumba ya kumuenzi Mwalimu kwa kuita Majengo jina lake Naona sasa Imepitwa na wakati!
Ifahamike Mwalimu hakuwa malaika! Hivyo tunaweza kufanya bora zaidi kutoka pale alipoishia yeye!
Kuita Shule ya Mwalimu nyerere, ni kuweka speed gavana kwenye saikolojia ya mafunzo yatayofanyika mahala pale!
Nashauri itoshe pale kuitwa SHULE YA UONGOZI TANZANIA (SUT) ili kuweka Uhuru wa mafunzo!
Mafunzo yatakayotolewa pale yatawanukuu viongozi mbalimbali akiwemo Mwalimu nyerere na wengine duniani kama role model!
Hivyo kuita kila kitu MWALIMU NYERERE hii wala siyo uzarendo Bali ni unafiki!
Mwalimu nyerere anatakiwa kuenziwa moyoni na si kwenye majengo!
Nashauri hivi ili kuvutia hata wanasiasa kutoka mataifa ya mbali kuja kujifunza pale pasipo kufungamana na jina LA Mwalimu nyerere!
Taasisi zilizowahi kupewa jina hilo zinatosha!
Sasa naomba majengo yabebe MAONO halisi ya LENGO!
Itakuwa na maana kubwa sana kama Pataitwa SHULE YA UONGOZI TANZANIA (SUT)
Tuondoe hii speed gavana ya Mwalimu
Naomba tuliokaribu na Rais Samia hususani Usalama kitengo cha siasa na propaganda Tumuombe Rais apendekeze hilo jina litumike siku ya uzinduzi 23 Feb pale KIBAHA
View attachment 2124648
nyerere ni icon ya Afrika na hata duniani alitambulika kama kiongozi bora kwa wakati wake na hata sasa hakuna alie wewza kuvaa viatu vyake tz kwa mantiki hiyo acha apewe sifa zake.
cha kusisitiza hapa ni elimu na mafunzo na wakufunzi na wana zuoni wawe na element za nyerere hasa kwenye uadilifu.
tukiwa tuna waita watu kama Pro Lumumba from kenya aje kukata kipindi siku moja next time anaenda Jeneral Ulimwengu tunakuja na profesa Issa Shivya n.k italeta maana kidogo ya hilo jina.