abulaaliyah77
JF-Expert Member
- Oct 13, 2021
- 1,750
- 1,154
Samia akithubutu kufanya hlo hapo wale wala kiti barid lazma wamparure
Sikatai kumuenzi Mwalimu nyerere,
Lakini hii kasumba ya kumuenzi Mwalimu kwa kuita Majengo jina lake Naona sasa Imepitwa na wakati!
Ifahamike Mwalimu hakuwa malaika! Hivyo tunaweza kufanya bora zaidi kutoka pale alipoishia yeye!
Kuita Shule ya Mwalimu nyerere, ni kuweka speed gavana kwenye saikolojia ya mafunzo yatayofanyika mahala pale!
Nashauri itoshe pale kuitwa SHULE YA UONGOZI TANZANIA (SUT) ili kuweka Uhuru wa mafunzo!
Mafunzo yatakayotolewa pale yatawanukuu viongozi mbalimbali akiwemo Mwalimu nyerere na wengine duniani kama role model!
Hivyo kuita kila kitu MWALIMU NYERERE hii wala siyo uzarendo Bali ni unafiki!
Mwalimu nyerere anatakiwa kuenziwa moyoni na si kwenye majengo!
Nashauri hivi ili kuvutia hata wanasiasa kutoka mataifa ya mbali kuja kujifunza pale pasipo kufungamana na jina LA Mwalimu nyerere!
Taasisi zilizowahi kupewa jina hilo zinatosha mfano; chuo cha Mwalimu nyerere, secondary na primary za nyerere, uwanja wa nyerere, chuo cha Mwalimu nyerere Zanzibar, kigoda cha Mwalimu nyerere, Mwalimu nyerere memory academy, ukumbi wa Mwalimu nyerere, nyerere square, Daraja la nyerere n.k! (ZINATOSHA)
Sasa naomba majengo yabebe MAONO halisi ya LENGO!
Itakuwa na maana kubwa sana kama Pataitwa SHULE YA UONGOZI TANZANIA (SUT)
Tuondoe hii speed gavana ya Mwalimu
Naomba tuliokaribu na Rais Samia hususani Usalama kitengo cha siasa na propaganda Tumuombe Rais apendekeze hilo jina litumike siku ya uzinduzi 23 Feb pale KIBAHA
View attachment 2124648