Shule mbeya mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule mbeya mjini

Discussion in 'Matangazo madogo' started by IPILIMO, Oct 22, 2012.

 1. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Wadau wa elimu, napigia debe shule moja ya sekondari iliyopo Mbeya jijini. ITENDE SEC. SCHOOL

  • Ni shule ya wasichana na wavulana
  • Ni ya kutwa na hosteli ndani ya shule
  • Imeanzishwa tangu 1992
  • Ina O & A levels
  • O level-masomo ya ARTS & SAYANSI
  • A level-michepuo HGL, HKL, HGK & HGE
  • A level ilianza 2009 na inafanya vema ( 2012 ya 5 kimkoa, 40 kitaifa)
  • ADA kutwa ni sh 400,000 (inalipwa kwa awamu mbili 250,000/150,000)
  • ADA ya kutwa pamoja na HOSTELI ni sh 900,000 ( inalipwa 500,000/400,000)
  • NAFASI za kuhamia januari 2013 zipo; kidato cha 1, 2, 3, 4, 5 & 6
  • KUANZIA JANUARI 15, HADI APRIL 30 2013 KUTAKUWA NA MASOMO YA PRE-FORM 5 KWA ADA YA SH. 80,000 KWA KIPINDI CHOTE na WATAKAO TAKA HOSTELI WATALIPA 180,000 KWA KIPINDI CHOTE.
  • WATAKAO SOMA PRE-FORM 5 na ikatokea wakaendelea na FORM 5 HAPA SHULE WATAPEWA PUNGUZO LA ADA ( 350,000 SH badala ya 400,000 sh).
  • shule ipo mazingira tulivu ya kujisomea, pia nje kidogo ya pilikapilika za jijini.

  Mawasiliano; kihegam@gmail.com utende2011@yahoo.com; 0652-656565, 0756-629094
   
 2. Kig

  Kig JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 1,060
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mbona mambo ya msingi hasa uwepo wa walimu wenye viwango na wanaojituma, uwepo wa vitu kama maabara zenye vifaa na wataalamu, nk hujagusia kabisa katika kutangaza shule yako. Umeegemea sana kwenye hela.
  Nimeangalia matokeo ya form six 2012 kwenye mtandao hayajanivutia sana hasa ukizingatia wanafunzi walikuwa 16 tu, na wote ni wa masomo ya art ambayo vijana wengi wanafaulu vizuri sana, lakini sijaona division one hata moja. Lakini hongeren maana hakuna division zero. Jipangeni vizuri kijana wangu nategemea nitamleta hapo siku chache zijazo.
   
 3. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  ASANTE KWA USHAURI MKUU, WALIMU WA A LEVEL WANA NI QUALITY GRADUATES; KILA SOMO WALIMU WAWILI P1&P2, TUANAO FULL TIME NA PART TIME (ambao hutusaidia kuleta radha ya kutoka shule zingine wanakotaoka kama MBEYA DAY, LOREZA, META, SANGU NA MUST). KWAKUWA NDO TUNAMOVE HATUISHI MBINU ZA KUFANIKISHA DIV.1 mkakati ni kuondoa div. 3 na 4. Pia asilimia kubwa ya wanafunzi wetu hawa kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa ni wale wa kuunga unga masomo yao wakati wa O level, na wengine kutafuta credit wakiwa f.5, so we are doing the best we can to make them perfect!! MAABARA kwa ajili ya sayansi O level ipo nzuri, pia makitaba na mafunzo ya kompyuta yapo, kwamchango wa elfu 30 tu kwa kozi ya program 4; introduction to computer, MS WORD, EXCEL & INTERNET AND EMAIL. (akifaulu hupatiwa cheti).
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  hii shule iko Kalobe, ni shule ya umoja wa wazazi wa CCM.
  Kiwango chake cha ufaulu ni duni sana, haina maabara wala maktaba.
  Hii shule ni sawa na chuma chakavu
   
 5. B

  BLB JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamaa kasema mbeya mjini, mkuu umemmaliza, Duu
   
 6. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  nakuunga mkono mkuu kwa hilo hawa jamaa ni pangu pakavu tia mchuzi twende,between 2000/2004 lilikuwa ndio zoa zoa la waliochujwa mashule mengine kama mbalizi sangu na nyinginezo. Sio shule ni sanaa tu!
   
 7. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Si kweli kaka, njoo utembelee uone hicho chuma chakavu, usiwachanganye watu, sio vizuri. Shule ipo Itende si Kalobe, na tena zingatia kuwa si kila mtoto na mzazi ataweza peleka mtoto shule unazo fikiri wewe!! HII ni shule nzuri sana; mandhari na miundombinu; library na laboratory zipo!! matokeo kwamba ni duni yawezekana hasa kama watoto wanaokuja na kupokelewa hapa wengiwao ni total failures std 7, Lakini wakija hapa wanatoka na kitu atleast. Na wanaokuja vizuri ndo hao wanapeta, hata walio kwenda serikalini wengine wanakuja hapa!
   
 8. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Narudia shule ipo mbeya mjini, kama unamskiliza huyo jamaa utapotea, Kwani KALOBE IKO WAPI HAPA MBEYA? Mkuu kalobe ipo mbeya mjini (tena jijini mbeya!!!) hiyo ni kata ndani ya jiji la mbeya. Sema shule iko pembeni ya jiji.
   
 9. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Shule inamilikiwa na nani?
  Location sahihi, ni wapi ukiwa barabara kuu ya Tunduma, distance?
  Nia ni kuzidi kuifahamu tu
   
 10. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Aisee jamaa kawahadaa sana, Acheni kuwaharibia watu, kama hamuamini why not take your time to visit the school! vipi kuhusu wanafunzi wanaofaulu kupitia hapo, NA je nyinyi mnaelewa private school management and administration? If it is a community/parent school mnajua vision yake? Je mnataka walio chujwa au wasio chaguliwa shule zingine WAACHWE mtaani? basi kila shule ingekuwa ni mbalizi/meta/sangu/mbeya day ambako PIA KUNA div. 0,4,3,2,1. Uelewa na kiwango cha akili kinatofautiana baina ya mtoto na mtoto. OK mpeleke mwanao/mdogo wako/ndugu yako aende shule hizo KISHA achujwe kisha mlete hapa itende, sisi tutampokea coz tuna amini ataweza, na yeye akikubali kweli ataweza!!
   
 11. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Inamilikiwa na Jumuiya ya Wazazi Tz, kama ilivyo META, SANGU, MBALIZI, IVUMWE, TEGETA nk. Ukifika Nzovwe kama unaelekea Iyunga/mbalizi/Tunduma kuna barabarani ya vumbi mkono wa kulia, panaitwa NJIA PANDA YA ITENDE; kuna BODDABODA hapo uliza wakulete ni kama KM 2 AU 2.5 mwendo wa dk 15/20 kwa mguu, pikipiki dk 5/10.
   
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Hii ndo shule ya mulogo??


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 13. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  SIYO, ya kwake ni ya mtu binafsi (yeye) Southern Highland!!
   
 14. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Usitetee, shule tunawapeleka watoto wakajifunze na kufaulu vizuri, hatuleti watoto shule ili wakue na mwisho wa siku eti "at least watoke na kitu".
  Kwanini mnachukua mazuzu magic, je hamjioni kwamba mnakula hela za watu bure?
   
 15. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Shule yenu ni bomu kweli, yaani wanafunzi wanafeli hata kozi za awali kabisa za kompyuta, loooo, aibuuu
   
 16. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  muache kuwauzia wanafunzi ulanzi ndo tutakuja
   
 17. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  nani kahadaa?? mie nilikuwa natoa past experince with that school kwanini hamkuwa mnachukua freshers kama wengine na pia hata ilikuwa ukiangalia performance zao wanafunzi by then was more than below compared to the mentioned schools. Anyways may be with time things have changed. But it seems kama umehamaki vile mkuu.
  10% bwana LOL !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11
   
 18. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  With time, normally things change, take your own life experience and consider the aspect, then you will understand why you get me wrong! Try to imagine, if people will try to criticize and blame you because of the past!!

  What Itende high school is trying, is to strive for the best; Ni kwambie strategies zinatofautiana kati ya shule na shule; as as for the private schools, wengine huanza shule zao kwa mchujo na wakapata wanafunzi na wengine huanza kwa kuchukua kila mtoto by time factor wanaamua kuanza kuchuja, so usishangae siku moja ITENDE watakuwa ktk position ya kuchuja, ikiwa watabadili vision yao.

  But our strength is that; japo kuna wanafunzi wanakuja wakiwa so dull minded, juhudi zetu zinasaidia kuwaadilisha atleast to better status!! wengine wanafaulu kabisa (refer nini lengo la kupata elimu).

  Na ukutaka kujua kuwa tatizo si shule kupokea waliochujwa au wenye kiwango cha ufaulu wa chini, bado IMANI ya wazazi/walezi wao pamoja na walimu ni kuweza kuwasaidia watoto wao. Na ndio maana shule hii haiwezi kufa, AGAIN COME AND SEE, WILL GIVE YOU IN&OUT za strategies huku past ikiwa si kikwazo kwetu!!

  I invite you to promote ITENDE HIGH SCHOOL, knowing that we are doing all our best for the children regardless wamechujwa kwingine na kupokewa kwetu. Asilimia kubwa ya wanafunzi wa sasa si wakuchujwa kwingine, wanakuja wenyewe kwa kuzingatia MAMBO YA MSINGI!!!
   
 19. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Ndugu we mtata, nadhani hunielewi, go on brother thinking what you think right for this school!! Wanaojua juhudi zetu na mikakati yetu wataendelea, and this is a private school, hakuna anayelazimishwa, ukiwa mmoja wapo, ila tunaeleza n a tunafanya yale yamfanyayo mtoto kufaulu!! najua kama ulisoma lazima ulipata mojawapo ya div hizi; 1,2,3,4 AU 0. Think of the grade you got, then decide for your child/children which school to send them, but remember in this not all factors are constant!!! Na sidhani kila mzazi anawaza uwazavyo Juu ya shule hii! hakuna anayetaka kuwaibia watu hela, hii ni shule inaongozwa na wasomi na wenye uchungu pia, ONLY SOME FACTORS LIMIT what everybody wants!! na katika haki za mtoto ndugu yangu hata kama watoto hawa wako so dull, hawawezi kuachwa, na hakuna mzazi /mtoto /mwalimu anayependa hali ya kufeli.
   
 20. IPILIMO

  IPILIMO JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,772
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Sijui nikusaidiaje ndg, Ila THINK BEFORE YOU COMMENT!! hata wengine humu janvini watakuelewa!
   
Loading...