Utafiti nilioufanya nimegundua vijana wengi waliosoma shule za bei kubwa wanachelewa sana kuoa tofauti na waliosoma shule za serikali, hii ndio sababu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Hata mimi mwenyewe nimesoma shule za private lakini nina marafiki wengi waliosoma serikali, so nayaongea haya nikiwa nawajua wahusika.

Binafsi kwenye shule za msingi na o leve nimesoma za private, msingi nimesoma day ada ilikuwa laki 2 mwaka 2003 (kwa sasa ni milioni 1), o level sekondari ada iliku milioni 1 na nusu 2007 (kwa sasa milioni 3 na laki 2), A level nilisoma shule ya private ila hizi za ada ya kawaida

Marafiki zangu wengi wa shule ya msingi na o level hadi sasa hawajaoa, lakini marafiki zangu wengi wa A level na niliowajua wa shule za serikalini karibu wote wameoa tena mapema sana.

Nilichogundua ni kwamba wanaogopa watoto wao wataishi maisha ya chini kuzidi wao

Mtu anapiga hesabu kwamba yeye alisomeshwa private ya bei, anajiona kwa hali yake mtoto itabidi aende shule za serikali, hii inakuwa aibu sana kwake, yeye hajawahi kushika hata kidumu lakini akianza kufikiria mtoto wake aanze kubeba kidumu ni stress tupu.

Unakuta wazazi walikuwa wameajiriwa sehemu zenye mishahara mizito ama wana biashara nzuri lakini wao wapo ajira za mishahara ya laki 7 ama biashara za kawaida, ni stress juu ya stress wakianza kufikiria kuwapitisha watoto misoto ambayo wao hawakuwahi kuijua
 
Back
Top Bottom